Wanamalumbano ITV watia mchanga kitumbua cha 'urais' cha Lowassa, wauchana mwenge wa uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanamalumbano ITV watia mchanga kitumbua cha 'urais' cha Lowassa, wauchana mwenge wa uhuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MJASIRIA MALI, Oct 26, 2012.

 1. M

  MJASIRIA MALI Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana niliangalia Malumbano ya hoja ya ITV na kufurahia sana baadhi ya hoja ya wachangiaji ambao walinifanya nilete mada hii hapa. Mada ilikuwa ni Changamoto ya maambukizi mapya ya ukimw kwa vijanai; kipi kifanyike. nitafafanua hoja za wachangiaji watatu.

  1 Mikael Aweda
  Wachangiaji wengi walihusisha umaskini na ukosefu wa ajira na kuongezeka kwa maradhi ya ukimwi akiwepo Mikael Aweda aliyesema tatizo maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi haliwahusu watoto wa vigogo ambao wanasoma katika shule nzuri na baada ya hapo wanapata ajira za nzuri na za uhakika. Akaendelea leo nimepata meseji yenye majina ya watoto wa vigogo walioajiriwa BOT ambao haya mambo ya ukimwi unatokana na umaskini hayawahusu. Alisema, watoto wa maskini ndio wanaohangaika na wanafeli kwa kusoma katika shule mbovu, kupata kazi mpaka atoe hongo ikiwepo ngono inayoleta ukimwi, wengi hawapati kazi. Ni watoto wa maskini ndio wanaofanya ngono inayowaletea ukimwi kutokana na maisha magumu yanawakumba. Hawana la kufanya.
  Nini kifanyike?

  AWEDA alipendekeza vijana wapatiwe ajira. Wanasiasa waache kuwadanganya watanzania kuwa ukosefu wa ajira ni bomu litakalolipuka huku wao wakiwa hawafanyi lolote. Maneno matupu hayavunji mfupa. Kama wanadhamira ya kweli wangeshafanyizia kazi madai yao hayo. Badala yake hakuna walifanyalo zaidi wanawadanganya tu wanatanzania kwa maslahi yao. Japo kuwa hakuwataja mwanasiasa, lakini nina uhakika hapa anamlenga mzee wa Monduli Mh Lowasa ambaye amekuwa akipigia kelele suala la ajira. Na hapa aweda alikuwa anatia mchanga ktk kitumbua cha urais cha mzee wa Monduli kwa kujua au kutojua.

  2 Stena Kajema
  Duce ( sina hakika na spelling ya majina yake)

  Huyu mwanadada mrembo aliongea kwa ufupi na hakuwa na ujasiri sana lakini alikuwa na hoja nzuri sana kwamba Mwenge wa uhuru uwekwe Benchi kwa sababu unachagia kuongezeka kwa maambukizi ya ukimwi.

  My take, Japokuwa hakufafanua lakini maeneo yanakokesha mwenge wa uhuru ndiko kunakofanyika ngono nyingi na kusababisha maambukizi mapya.

  3 NGOYI aka mwananchi wa kawaida ( Jina la pili limenitoka)

  Huyu bwana Ngoy alidai kuwa ugonjwa wa Ukimwi ni kama mgodi na watu wengi wameufanya dili ndio maana ukimwi ni ugonjwa pekee unaoitwa mradi wa ukimwi. Hata baadhi ya marais wameanzisha taasisi za ukimwi NA si malaria. Malaria inaua watu wengi kuliko ukimwi kwa mbali. Lakini kwa kuwa malaria haina wafadhili hakuna anayehangaika. KWA maoni yake ukimwi ni Mgodi wa fedha na wengi wamejiajiri humo na wanaendesha magari mazuri kwa miradi ya ukimwi wala hawataki uishe.
   
 2. M

  MORIAH Senior Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu Aweda sasa naona ameaumua kupigania Chadema yale kwa staili ya liwalo na liwe. Huko anakoenda sina la kusema. Binafsi niliangalia kipindi.
   
 3. G

  Gurti JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona mimi sioni tatizo mkuu, si ni kweli Lowasa anaimba bomu la ajira na hafanyi lolote ila anatumia hoja hiyo kusaka urais. Hofu yako ni Aweda kushughulikiwa? Mimi sidhani, wawaache akina Mbowe waanze kumfikiria Aweda, Mwache awachape ktk majukwaa ya JF na ITV. Hawatamdhuru madara yake madogo sana.
   
 4. Jangakuu

  Jangakuu JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  mimi nimemkubali , Ngoyi, kwamba baadhi ya viongozi ukimwi wameufanya mtaji, mfano mzuri presida awamu ya 3
   
 5. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Duhu jamaa sijui ndiye aweda hii thread nmeisoma mpaka naona kama nmepoteza tym yangu kubrowse cz anachoandka juu akiendan na cha ndan lowasa anahuska vp na matatzo hayo?je ni rais wa nchi kwa sasa? au ni waziri mkuu kwa sasa? ata ukitumwa na wabaya wa lowasa tafta ajenda ya kukufanya ulipwe na wanaokutuma sii hii...more dan worse topc
   
Loading...