Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,720
- 21,778
WANAKWAYA watatu wa Kanisa la African Inland Tanzania (AICT) Mlimani Sayuni wilayani Kahama, katika mkoa wa Shinyanga, wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya baada ya kutwangana makonde wakigombea kuimba katika Ibada.
Tukio hilo la aina yake lililohusisha kwaya mbili za Kanisa hilo za Zion na Emaus lilitokea Jumapili iliyopita baada ya wanakwaya hao kuoneshana umwamba wa kusukumiana makonde yaliyozua tafrani kubwa kanisani.
Inadaiwa vurugu hizo zilienea hadi kufika kwa waumini waliohudhuria misa hiyo kugawanyika makundi mawili na kukabiliana mtu kwa mtu pasipo kujali rika ama jinsi huku mabenchi ya kanisa yakitumika kama silaha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Dk. Helen Yesaya almaarufu kwa jina la Mama Membe, aliwataja wanakwaya waliolazwa kuwa ni Loyce Mussa (24) mkazi wa Nyahanga
na Veronica Thomas (31) mkazi wa Majengo waliolazwa wadi tatu na Kusekwa Mussa (24) mkazi wa Kata ya Kahama mjini aliyelazwa wadi namba nane.
Dk. Yesaya alisema mwanakwaya mwingine, Malago Thomas aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kushonwa nyuzi katika paji lake la uso, alichanika kwa kujeruhiwa na ubao.
Mapigano hayo yaliyoanza saa nne asubuhi na kudumu kwa saa mbili kabla hayajatulizwa na Polisi.
Ilimlazimu Mchungaji wa Kanisa hilo, Michael Balele akimbilie nyumbani kwake hatua chache kutoka kanisani hapo na kujifungia chumbani baada ya kundi mojawapo la wanakwaya kutaka kumuadhibu kwa madai ya kupendelea kundi lingine.
Polisi kutoka Kituo Kikuu waliofika kutuliza ghasia hizo walimuokoa.
Kwa mujibu wa habari kutoka Polisi zilizothibitishwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kahama, George Simba, chanzo cha mapigano hayo ni mgogoro wa siku nyingi uliosababisha mojawapo ya kwaya hizo kufungiwa kutoimba
katika kanisa hilo na kwamba siku hiyo wanakwaya wake waliamua kufunga vyombo vyao vya muziki na kutaka kulazimisha kuimba kwa nguvu, na ndipo vurugu zilipozuka kabla ya ibada kuanza.
Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, John Nkola akizungumza kwa simu, alisema tayari hatua za kichungaji zimechukuliwa kwa kuunda tume itakayofuatilia kwa umakini suala hilo kwa kukusanya vielelezo vyote vya mgogoro huo ili hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Jeshi la Polisi wilayani hapa, linawahoji baadhi ya wanakwaya wa pande zote mbili zilizopigana ili hatua zaidi zichukuliwe.
Jumla Maoni (0)