Wanakwaya watwangana kanisani!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,722
21,775
WANAKWAYA watatu wa Kanisa la African Inland Tanzania (AICT) Mlimani Sayuni wilayani Kahama, katika mkoa wa Shinyanga, wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya baada ya kutwangana makonde wakigombea kuimba katika Ibada.

Tukio hilo la aina yake lililohusisha kwaya mbili za Kanisa hilo za Zion na Emaus lilitokea Jumapili iliyopita baada ya wanakwaya hao kuoneshana umwamba wa kusukumiana makonde yaliyozua tafrani kubwa kanisani.

Inadaiwa vurugu hizo zilienea hadi kufika kwa waumini waliohudhuria misa hiyo kugawanyika makundi mawili na kukabiliana mtu kwa mtu pasipo kujali rika ama jinsi huku mabenchi ya kanisa yakitumika kama silaha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Dk. Helen Yesaya almaarufu kwa jina la Mama Membe, aliwataja wanakwaya waliolazwa kuwa ni Loyce Mussa (24) mkazi wa Nyahanga

na Veronica Thomas (31) mkazi wa Majengo waliolazwa wadi tatu na Kusekwa Mussa (24) mkazi wa Kata ya Kahama mjini aliyelazwa wadi namba nane.

Dk. Yesaya alisema mwanakwaya mwingine, Malago Thomas aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kushonwa nyuzi katika paji lake la uso, alichanika kwa kujeruhiwa na ubao.

Mapigano hayo yaliyoanza saa nne asubuhi na kudumu kwa saa mbili kabla hayajatulizwa na Polisi.

Ilimlazimu Mchungaji wa Kanisa hilo, Michael Balele akimbilie nyumbani kwake hatua chache kutoka kanisani hapo na kujifungia chumbani baada ya kundi mojawapo la wanakwaya kutaka kumuadhibu kwa madai ya kupendelea kundi lingine.

Polisi kutoka Kituo Kikuu waliofika kutuliza ghasia hizo walimuokoa.

Kwa mujibu wa habari kutoka Polisi zilizothibitishwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kahama, George Simba, chanzo cha mapigano hayo ni mgogoro wa siku nyingi uliosababisha mojawapo ya kwaya hizo kufungiwa kutoimba

katika kanisa hilo na kwamba siku hiyo wanakwaya wake waliamua kufunga vyombo vyao vya muziki na kutaka kulazimisha kuimba kwa nguvu, na ndipo vurugu zilipozuka kabla ya ibada kuanza.

Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga, John Nkola akizungumza kwa simu, alisema tayari hatua za kichungaji zimechukuliwa kwa kuunda tume itakayofuatilia kwa umakini suala hilo kwa kukusanya vielelezo vyote vya mgogoro huo ili hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya wahusika.

Jeshi la Polisi wilayani hapa, linawahoji baadhi ya wanakwaya wa pande zote mbili zilizopigana ili hatua zaidi zichukuliwe.

Jumla Maoni (0)
 
Hawa ni kuwapa kadi wakaanzishe kanisa lao kabisa yaani hakuna kurudi
makanisa atuwezi lea wazinzi,na mabondia tena hii ni laana sasa
 
Duu, Ngosha wamenifurahisha sana. Miaka ya 80 pale Tabora karibu na geti la Kuingilia hospital ya Mkoa wa Tabora (Kitete Hospital), Wapendwa walijenga kanisa lao. Siku moja walipokosana (ugomvi wa muda mrefu) unaambiwa zilichapwa si kawaida. Power Mabula alikuwa anabeba watu na kuwatupa nje. Ugomvi akaja kuuamulia Kulola na kuwarudisha wote pamoja maana walishaanza kujenga kikanisa pembeni.
 
Mkuu ngosha o'Sikonge kwa mayo wane umenikumbusha mbali sana,hivi huyu power Mabula bado yuko hai?
 
Huyo Kulola na yeye si ameshakuwa na ugomvi mara nyingi tu?Ama sasa ilikuwa zamu yake kuamulia?teh teh te!
 
Mambo mengine bwana, so amazing!Sasa kama wanakwaya wanapigana hizo nyimbo zao na hayo mapambio ya kumsifu Bwana yatasikika kweli?unaweza kukuta chanzo ni mchungaji kula kondoo mmoja wa Bwana ambaaye ni mmoja wa waimbaji wa kwaya mojawapo! Kwanini mchungaji alikimbia badala ya kuamua ugomvi huo?
 
Waingie kwenye bongo fleva ambako hamna muda wa kugombea kuingia.
Ukiwapa tu hela kidogo ma dj wa cloudz utapata airtime hata kama wimbo wako ni mbaya na hauna ujumbe wowote wa maana .
 
Nafirikiri shetani anatafuta wafuasi kila kukicha. sasa wasipokaa na kutafakari nini kimewafanya wapigane kanisani wakati ni mahali patakatifu na tena walikuwa wakimwabudu Mungu kwa sala na nyimbo. watakuwa wanapotea zaidi.

Maana kama kweli walifungiwa kuimba maana yake kuliwa na sababu najua hata muumini anapokosa anatengwa na kanisa ila pale anapojirudi na kutambua makosa yake hutubu na kumrudia Mungu na kanisa humkaribisha kwa mikono miwili. lakini huwezi kulazimisha kurudi kanisani kwa nguvu ikiwa hujatubia kile kilichokufanya utengwe na kanisa.

So naamini wote wamepotoka wameoza hakuna hata mmoja aliyetenda vyema.
Bwana Yesu apewe sifa.
 
Mkuu ngosha o'Sikonge kwa mayo wane umenikumbusha mbali sana,hivi huyu power Mabula bado yuko hai?

Aisee nina miaka mingi sijamsikia Power Mabula. Na sifahamu wala alikuwa akiishi wapi. Huu ugomvi ulivuma sana Tanzania/Tabora kwani ilikuwa ni kinyume cha watu tulivyowafahamu Walokole. Labda bado anaishi. Ngoja Ze greti Sinka waje hapa watoe habari.
 
Huyo Kulola na yeye si ameshakuwa na ugomvi mara nyingi tu?Ama sasa ilikuwa zamu yake kuamulia?teh teh te!

Mkuu,
Alichokuwa akikifanya Askofu Lazaro pale TAG ni kitu kilichokuja kuleta ugomvi serikalini, makanisa na misikiti ukiachilia mbali huduma za jamii na kifamilia. Misaada ilikuwa ikija imeandikwa kwa jina lake, basi yeye alikuwa hahangaiki sana, anatia ndani. Hata ije kwa jina la Askofu wa TAG tu, pia alikuwa akitia ndani. Ikija imeandikwa TAG basi alipeleka kanisani.

Hii ilianzisha ugomvi mkali sana kati ya Mchungaji Kulola na Lazaro. Tatizo ni kuwa Kulola alikuwa ni more popularna wafuasi kibao (hasa Ngosha). Ila sema Lazaro alikuwa Askofu. Hii ilipelekea ugomvi kuwa mkali sana na nafikiri nusura wajitenge pia. Nafikiri AG kutoka USA ndiyo walikuja kuweka mambo sawa.

Kweli UFISADI Tanzania umeanza siku nyingi na ni jamii nzima iko hivyo. Inabidi aje kiongozi abadili akili na mawazo yetu.
 
Shukran kwa maelezo mkuu,nilikuwa bwana mdogo enzi hizo ila nakumbuka kuhusiana na mgogoro huo kwa mbali kwani serikali nadhani pia ilijaribu kusulisha nyakati flani flani,nilikuwa sijui sababu ni Askofu Lazaro kuzima misaada.
NB:Ngosha ndio kina nani hao mkuu?Do you mean wasukuma?
 
huyo mchungaji akae nao vizuri sosi aitakuwa nyimbo;jamani mnaojua wanakwaya kuna mambo kule ndani;hata vidosho vya wachungaji vinatokeaga kule
 
Aisee nina miaka mingi sijamsikia Power Mabula. Na sifahamu wala alikuwa akiishi wapi. Huu ugomvi ulivuma sana Tanzania/Tabora kwani ilikuwa ni kinyume cha watu tulivyowafahamu Walokole. Labda bado anaishi. Ngoja Ze greti Sinka waje hapa watoe habari.

Sikonge, Power Mabula bado yuko hai. Siku hizi ni Mchungaji katika mojawapo ya Makanisa ya Kipentekoste.
 
Sikonge, Power Mabula bado yuko hai. Siku hizi ni Mchungaji katika mojawapo ya Makanisa ya Kipentekoste.

Nashukuru kwa kunifahamisha. Nakumbuka hata jamaa mmoja aitwaye Malekwa (Mgogo) wa kanisa la Anglican alikuwa mrusha Mkuki maarufu sana wa kimataifa na yeye mara ya mwisho kumuona Arusha, alikuwa akielekea kuwa Mchungaji.
 
Nafirikiri shetani anatafuta wafuasi kila kukicha. sasa wasipokaa na kutafakari nini kimewafanya wapigane kanisani wakati ni mahali patakatifu na tena walikuwa wakimwabudu Mungu kwa sala na nyimbo. watakuwa wanapotea zaidi.

Maana kama kweli walifungiwa kuimba maana yake kuliwa na sababu najua hata muumini anapokosa anatengwa na kanisa ila pale anapojirudi na kutambua makosa yake hutubu na kumrudia Mungu na kanisa humkaribisha kwa mikono miwili. lakini huwezi kulazimisha kurudi kanisani kwa nguvu ikiwa hujatubia kile kilichokufanya utengwe na kanisa.

So naamini wote wamepotoka wameoza hakuna hata mmoja aliyetenda vyema.
Bwana Yesu apewe sifa.

Huh. BWANA YESU APEWE SIFA HAPA KWA LIPI SASA?? KWA WATU KUPOTOKA NA KUOZA!!?
 
Hivi USHOGA umesharuhusiwa makanisani? na waumini wameshaanza kulawitiana?
 
Ilimlazimu Mchungaji wa Kanisa hilo, Michael Balele akimbilie nyumbani kwake hatua chache kutoka kanisani hapo na kujifungia chumbani baada ya kundi mojawapo la wanakwaya kutaka kumuadhibu kwa madai ya kupendelea kundi lingine.

ha haaaa haaaaa haaa.
 
Hivi kumwimbia Mungu ni mpaka uwe mbele za watu? Paulo na sila waliimba gerezani mpaka uwepo wa mungu waliyemwimbia ukaifungua milango ya kanisa. Sasa nyimbo za injili za siku hizi ni uchuuzi mtupu. Ni ajira ya kisanii kama sanaa nyingine tu. Wakati wa uzinduaji wa kile wanachoita album watamwita hata shetani kuwa mgeni rasmi ilimradi tu ana uwezo wa kuchangia fungu zito. Halafu wanadai kuwa wanamwimbia Mungu. Mungu yupi mnaemwimbia wakati kinachoonekana ni kulitumbuiza fisadi mlilialika ili kulichuna? Hilo fisadi ndio mungu? Ama kweli hilo fisadi ndio mungu wenu na pesa zake ndio nguvu zinazowavuvia upako!! No wonder mnatandikana makonde kwa kuhisi kuukosa ulaji.
 
Back
Top Bottom