Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,991
- 144,327
Tukiwa safarini katika basi dogo kutoka sehemu moja ya kijiji chetu kwenda sehemu nyingine,tulifika mahali tukapaki gari ile tupate msosi na pia tuweze kuchimba dawa kabla ya kuendelea na safari.
Wakati baadhi ya wenzetu wakiendelea kupata msosi,sisi tulikaa kakikundi na tukawa tunapiga story za hapa na pale.Tukiwa katikati ya mazungumzo hayo ya muda mfupi,jamaa mmoja aliekuwa anaperuzi simu yake ya mkononi,akagusia swala la mwenyekiti liliokuwa gumzo pale kijijini kwa siku kama mbili au tatu hivi na hapo mada ikabadilika na mjadala ukawa juu ya sintofahamu iliyokuwa imemkumba mwenyekiti wetu.
Kila mtu aliongea lake alilokuwa analijua ama kusikia kuhusu mwenyekiti, ila katika wote waliongea,kuna mwenzetu mmoja alisema kuwa yeye alikuwa katika enep la tukio na walikuwa sehemu wakimsubiri mwenyekiti apite na msafara wake ila cha ajabu msafara wa mwenyekiti haukupita na badala yake alipita mawinguni na kwamba hawakuambiwa hata kilichotokea.
Mimi sikutaka kumuamini sana mwanakijiji yule ila tulipofika safari yetu na mimi kuingia mtaani,nikakuta story ni ile ile katika maeneo mengine ya kijiji na hata katika mitandao habari ikawa ni ile ile.
Sasa kwa wale wadau wanaotoka katika kijiji hiki (kijiji X) na wanaoofahamu hii issue,mnaweza kutueleza ni nini kilimpata mwenyekiti wetu kama habari ile ilikuwa na ukweli kiasi kwamba ilibidi apitishwe mawinguni faster faster kama inavyodaiwa na hawa wanakijiji wenzetu?
Je,walihofia ile mvua na kuhisi njia ya barabara isingefaa kama baadhi ya wanakijiji walivyodhani au kulikuwa na sababu nyingine ambayo haikuwekwa wazi?