Wanakijiji Waua Mamba 300 Indonesia Kulipiza Kisasi

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Image copyrightREUTERS
_102542315_7ee6f1ff-a327-4041-9016-248523395882.jpg

Image captionMamba wakubwa na wadogo wote waliuawa
Kundi la wanakijiji limewaua karibu mamba 300 kwenye makao ya wamyama katika mkoa wa West Papua nchini Indonesia.

Muuaji hayo yalikuwa ni ya kulipiza kisasi kifo cha mwanamume mmoja ambaye aliuawa na mamba mmoja eneo hilo.

Maafisa na polisi wanasema kuwa hawakuweza kuzuia mauaji hayo lakini watafungua mashtaka.

Kuuliwa kwa wanyama wanaolindwa ni hatia na inaweza kusababisha kifungo nchini Indonesia.

Mwanakijiji huyo aliuawa siku ya Ijumaa asubuhi wakati alikuwa akitafuta mboga eneo la kuzalia mamba.
Mfanyakazi alisikia mtu akiitisha msaada na alipofika huko aliona mamba akimshambulia mtu.

Baada ya mazishi siku ya Jumapili, mamia kadhaa ya wanakijii wenye hasira walielekea eneo la makao ya wanyama wakiwa wamejihami kwa visu, chuma, nyundo na sururu.

Vyombo vya habari vinasema kuwa wanakijiji walilishambulia ofisi kwenye makao ya wanyama na kisha kuelekea kuwachinja mamba wote 292.


BBC
 
Hongera yao kwa ujasili, wanasema nguvu ya mamba kumai. Wapewe wafanye kitoweo ukanda huo hao ni chakula safi
 
Duhhhhhh hiyo ndiyo mathara ya watu kuwa wengi kuliko ardhi hapa kwetu jiwe linataka watu tuzaliane tufyatue tufyatue tufyatue madhara yanayotokea watu wanakuwa wengi. Sasa nawaambie watanzania zaaneni tuu mpka mjae kwenye mapori ya akiba
 
Back
Top Bottom