Wanakijiji wapendekeza wabunge wanaolala bungeni wamwagiwe maji ya baridi na wachapwe viboko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanakijiji wapendekeza wabunge wanaolala bungeni wamwagiwe maji ya baridi na wachapwe viboko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nhassall, Oct 12, 2012.

 1. n

  nhassall Senior Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Burhani Yakub, Muheza.
  WAKAZI wa Kata ya Misalai Tarafa ya Amani Wilayani hapa,wamependekeza kuwepo kwa kipengele cha adhabu ya kumwagiwa maji ya baridi nakisha kuchapwa viboko kwa mbunge atakayesinzia akiwa kwenye kikao bungeni.
  Wamependekeza pia kwamba adhabu hiyo iambatane nakutoruhusiwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo pamoja na kuzuiwa kugombea tenakipindi kingine mara muda wake utakapomalizika.
  Walitoa mapendekezo hayo kwa wajumbe wa Tume ya maoni yamarekebisho ya Katiba ilipofika Kijiji cha Misalai kukusanya maoni ya wananchiwa Tarafa ya Amani Wilayani Muheza.
  Shukrani Said (23) ambaye ni mkulima wa Kijiji cha ZiaraiKata ya Misarai wilayani hapa alisema kutokana na baadhi ya wabunge kuonekanamara kwa mara kupitia runinga inayoonyesha vikao vya Bunge kuonekana wakiwawamesinzia kuna kila haja ya Katiba mpya kuwekwa vifungu vitakavyowabanawasilale bungeni.
  “Wabunge hatukuwatuma waende wakalale, matokeo yakezinapitishwa sheria zinazotubana, tuliwachagua waende wakatuwakilishe, kwa hiyokuwe na kipengele cha adahabu ya viboko,” alisema Shukrani na kusisitizakuwa adhabu hiyo inavyofanyika ionyeshwe kwenye runinga.


  Richard Lutangilo wa Kijiji cha Bulwa Wilayani hapa alisemapamoja na adhabu ya viboko, Katiba iongeze kipengele cha kumwagiwa maji kilambunge atakayesinzia na kama haitoshi asipewe ruhusa ya kuhudhuria vikao vitatumfululizo na pia asiruhusiwe kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo mara kipindichake cha miaka mitano kinapomalizika.
  “Hili la viboko likiwekwa kwenye Katiba litaleta umakini wawabunge wetu kwani tunawaona inatuhuzunisha sana sisi wapiga kura tunapowaonawakiwa wamelala fofofo bungeni wakati vikao vikiendelea,” alisemaJackob Zephania.
  Hadi Mlowe (50) mkazi wa Kijiji cha Mgambo Wilayani hapaalipendekeza umri wa wagombea wa nafasi ya ubunge uanzie miaka 45 kwa kuwaamebaini wabunge vijana ndiyo chanzo cha kukosekana kwa nidhamu ndani yaBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  “Napendekeza katiba mpya iweke ukomo wa umri wa kuanzia kwanafasi ya ubunge ili kuondokana na chombo hiki muhimu kukosekana kwa nidhamutunasikia jinsi wabunge vijana wanavyoropoka linaonekana kama ni Bunge lakihuni,” alisema Mlowe.
  Cleopas Mutabuzi (50) mkulima wa Kijiji cha Misalaialipendekeza madaraka ya Rais yapunguzwe hasa katika kuteua mawaziri, ambapoalitaka waajiriwe na Tume ya Utumishi kwa kufuata taaluma zao nasiyo kuchaguliwa kisiasa.

  Kadhalika nafasi ya Spika, naibu Spika na Katibu wa Bunge laJamhuri ya Muungano wa Tanzania alipendekeza zisitokane na wabunge baliwaajiriwe kupitia Tume ya Utumishi na baadaye majina yao yapitishwe bungeni kwaajili ya kupewa baraka na wabunge.

  Kamati hiyo ya kupokea maoni ya marekebisho ya Katiba ilikuwa wilayani hapa kwa muda wa siku tatu ambapo iliendesha mikutanoMajengo, Kwafungo, Mkuzi, Misozwe, Amani na Misalai.
  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii kiboko. Kapteni Komba, Wassira, Sitta na Mzee wa Kiraracha watakuwa wameiona hii.
   
 3. p

  pilau JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ............. Jamani hii itakuwa safi sana. tena sana ...... nakumbuka waliowahi kulala bungeni na kupigwa picha ni Stephen Wassira na Salome Mwambu... hiyo ipitishwe bila ya kupingwa............
   
Loading...