Wanakijiji waomba malipo ya minara ya simu iliyopo kijijini kwao wapewe kwa ajili ya ujenzi wa zahanati

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Wakazi wa kijiji cha Mazwe, wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wameomba viongozi wa Minara ya simu ya Tigo na Airtel walioweka minara yao kijijini hapo tangu 2013 malipo ya minara hiyo iwanufaishe wanakijiji wa kijiji hicho kwa kujenga zahanati kutokana na kuwa malipo hayo hayafiki katika ofisi za kijiji bali malipo hayo yanaenda kwa mkuu wa makazi ya wakimbizi ilihali minara ipo katika ardhi ya Kijiji Chao na haiwanufaishi.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Msonela Saimoni amesema kuwa tangu 2013 hadi 2018 malipo ya minara hiyo,Kiasi cha shilingi milion tatu na laki saba ilikuwa inaenda kwa mkuu wa makazi.

Lakini mwaka 2018 mwishoni uongozi wa kijiji wakaingia mkataba na wa watu wa Tigo Airtel ili malipo hayo yarudi kijijini kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Kijiji na kweli baada ya kupata malipo hayo wakaanza ujenzi wa zahanati huku wakisaidiana na nguvu kazi ya wananchi lakini mwaka 2020 malipo hayo yalisitishwa hadi na leo bila maelezo yoyote na hivyo kufanya ujenzi wa zahanati ya Kijiji kukwama kutokana na kuwa wananchi kukosa uwezo wa kuendeleza ujenzi wa zahanati hiyo peke yao.

Wakazi wa kijiji hicho wamesema kutokana Kukosekana zahanati kijijini hapo imekuwa ikiwalazimu kwenda hadi makao makuu ya kata ya Ipwaga ilipo zahanati.,na imekuwa ni hatari zaidi kwa akina mama wanaojifungua na wale wagonjwa wa huduma ya kwanza kutokana na Umbali uliopo.

Uongozi wa kijiji umeomba serikali kuangalia namna ya kurudisha malipo hayo ya minara ili uwanufaishe wananchi wa kijiji hicho katika ujenzi wa miundombinu kijijini hapo ikiwemo ukamilishaji wa zahanati hiyo.
 
Ninavyo Juan Mimi mnara unapowekwa ndipo mhusika analipwa
Mfano ikipita katika eneo lako Kuna kiwango unalipwa kwa kipindi chote inakuwa Kama umekodisha sehemu husika
 
Back
Top Bottom