Wanakijiji wadai kunyimwa chakula kisa upinzani

wikolo

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
801
195
2nd December 2012


Wakazi zaidi ya 40 wa kijiji cha Makao wilayani Meatu mkoani Simiyu wanaokabiliwa na njaa wametishia kumshitaki Mwenyekiti wa kijiji hicho kwa tuhuma za kuwanyima chakula cha msaada kwa madai kuwa ni wapinzani.
Walidai kuwa Mwenyekiti wa kijiji Anthony Philipo, aliwanyima chakula hicho kilichotolewa na wawekezaji walioko kijijini hapo kwa madai kuwa ni wanachama wa Chadema.
Walidai waliwanyima chakula na kuagizwa wakaombe msaada Chadema ama kwa mbunge wa chama hicho Meshack Opolukwa (Meatu).


Wananchi hao walisema baada ya wanakijiji kutoa malalamiko kuwa wana njaa katika mkutano wa hadhara walikubaliana kuwaomba msaada wawekezaji wa vitalu vya uwindaji na maeneo ya upigaji picha wanyamapori waliowekeza kijijini Makao.


Walisema kampuni za wawekezaji zilikubali maombi yao na kuchangia zaidi ya Sh. milioni 36.
Kabla ya kutimiza azma yao wameupa uongozi wa kijiji hicho siku saba ili kujibu tuhuma za ubaguzi wa itikadi zilizosababisha kuwanyima chakula ambacho ni haki ya msingi ya mwanadamu.


Akizungumza kwa niaba ya walalamikaji wenzake Shadrack Ntuli wa kitongoji cha Senta Makao alisema wamefedheheshwa na kitendo hicho cha ubaguzi ambacho ni kinyume cha haki za binadamu.

Aliongeza kuwa kaya 47 ziliathirika na ubaguzi huo zilipoambiwa kuwa ni wafuasi,washabiki na wanachama wa Chadema.


Mtuhumiwa Philipo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Makao alipohojiwa na NIPASHE Jumapili, alikiri kuwa wananchi wa kijiji hicho wana njaa na wameomba chakula cha msaada kwa wawekezaji lakini akakanusha madai kuwa walibaguliwa na kunyimwa chakula.


Alisema hawajabaguliwa bali ni wavamizi ndani ya kijiji cha Makao hivyo hawakusitahili kupewa mgao huo.
Alisema serikali yake ilipokea magunia 100 ya mahindi na mifuko 400 ya sembe ambavyo viligawiwa kwa wanakijiji hicho chenye kaya zaidi ya 420 na kwamba chakula kilitolewa kwa kufuata rejista ya wakazi wa kijiji hicho.


Akizungumzia madai hayo mbunge Opulukwa alisema amewasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Meatu Rosemary Kirigini ili kupata hatima ya wananchi hao ambao wanakabiliwa na njaa.

“Uongozi wa Chadema umemwandikia barua mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Makao Anthony Philipo ambaye ni diwani wa kata hiyo, nakala kwa mkuu wetu wa wilaya …. ikimpa siku saba kueleza sababu na kigezo alichotumia kuwabagua kiitikadi wananchi wake…”


Chama cha wanasheria kinachotetea haki za binadamu cha Pingo’s Forum kimelaani kitendo hicho na kuahidi kuwasaidia wanakijiji hichokupata haki yao.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

My Take: Hivi kumbe siasa zetu zimeshaanza kutufikisha katika hali hii? Unahudumiwa kulingana na ukada wako? Hapa naanza kuona tatizo kwani tuendako siko.
 

MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,047
2,000
Ubaguzi wa aina hii upo maeneo mengi sana hapa Tanzania. In general tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiri. Ni tabia ya viongozi wa CCM kufanya hivi ili kuzorotesha upinzani.
 

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
16,665
2,000
Ubaguzi wa aina hii upo maeneo mengi sana hapa Tanzania. In general tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiri. Ni tabia ya viongozi wa CCM kufanya hivi ili kuzorotesha upinzani.
CDM kwa sera za kulumu tu bila kufanya lolote hamjambo.

Sasa hebu pigeni jaramba la mchango, wanachama wenu wanalala njaa.
 

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,890
2,000
Hili sio ngeni, CCM wana sera za visasi na kukomoana sana. Kila mahali kuna makovu ya ubabe wa CCM na haikuanza leo, iko hivi toka awamu ya kwanza!

Dawa ni wananchi kuvumilia na kuhakikisha inapokuja nafasi ya wao kufanya maamuzi kupitia kura basi wanakuwa makini mno. Pamoja na haya tunaamini Mh Lissu, Mh Mnyika na wengine mchukue hatua kuibana serikali kandamizi ili wananchi wapewe huduma stahiki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom