Wanakijiji 12 mbaroni kwa kufunga barabara

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461

JESHI la Polisi wilayani Kalambo mkoani Rukwa, limewakamata na kuweka mahabusu kwa muda usiojulikana wakazi 12 wa Kijiji cha Ntatanda kwa tuhuma za kufunga barabara inayounganisha nchi za Tanzania na Zambia.

Wananchi wamekamatwa, baada ya kuchimba mashimo na kuweka magogo na kusimika bendera zao katikati ya barabara na kuzuia msafara wa mkuu wa wilaya hiyo.

Tukio hilo lilitokea jana na kusababisha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Julieth Binyura kushindwa kuendelea na ziara aliyokuwa akiifanya katika vijiji vilivyopo mpakani kwa lengo la kutatua kero mbalimbali.

Akiwa kijijini hapo, alikuta vijana12 wakiwa na majembe, mapanga na sururu, wameziba barabara kwa kuweka magogo ili kuzuia magari yasipite.

Kutokana na hali hiyo, alilazimika kuliita gari la polisi na kuagiza wakamatwe na kuwafunguilia kesi mahakamani ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Akizungumza baada ya kusitisha kwa muda msafara wake,Binyura kitendo hicho hakikubaliki kutokana kwani wangeweza kusababisha ajari.

‘Kitendo walichokifanya cha kuzuia barabara kwa kuweka magogo,kitendo kibaya hawa walikuwa na nia mbaya kama gari lolote lingepita lingeweza kupata kupata ajari, mashimo na magogo haya kweli ndugu zangu mnaweka barabarani,’’alihoji.

Baada ya kukutana na hali hiyo, msafara wake ulilazimika kusitishwa kwa muda na kuanza kufanya mahojiano na vijana hao.

‘’Tumewakamata wote na watahojiwa, kisha kufikishwa mahakamani ili wakaeleze kwanini waliamua kufanya kitendo kama hiki, wameishi hapa miaka mingi na hakuna ajali mbaya ambazo zimewahi kutokea.

“Kama zingekuwa zimetokea wangetoa taarifa kwa viongozi husika ili waweze kuweka matuta, lakini kufanya hivi. Aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuacha tabia ya kujichululia sheria mikononi,badala yake watoe taarifa kwa viongozi wa serikali za vijiji na kata pindi panapokuwa pametokea tatizo la aina yoyote kwa lengo la kuepukana na matatizo yasiokuwa ya lazima.

‘’Nawaomba wananchi muache tabia ya kujichukulia shera mikononi, ikiwamo kuchimba barabara bila kuzingatia athari zinazoweza kutokea,’’alisema Binyura.

Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, JulisTete alikemea vikali kitendo hicho na kusema hakikubaliki na kuahidi kuwaelimisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara juu ya athari za kujichukulia sheria mikononi.

‘Kitendo hiki nakilaani tena kwa nguvu zote,walichofanya wananchi wangu ni uvunjifu wa sheria na hakikubariki hata kidogo’’alisema

Alisema wananchi hao walilazimika kufanya hivyo kwa kile walichodai wamechoshwa kuona mifugo yao, ikiwamo nguruwe na kuku kugongwa na magari mara kwa mara yanayofanya safari zake kutoka Kaseshya kwenda nchini Zambia.

Chanzo: Mwananchi
 
wanafuga wanyama alafu wanategemea wakale barabarani,,kwa mtindo huu ndio wasigongwe.
 
Back
Top Bottom