Wanajikosha ili tuwaone kuwa hata wao wanachukia ufusadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajikosha ili tuwaone kuwa hata wao wanachukia ufusadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinyambia, Jan 21, 2011.

 1. k

  kinyambia Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari zenu wanaJF, jana nilishtushwa baada ya kuona taarifa ya kuwa UVCCM eti na wao wanatoa tamko kuhusu sakata la Dowans. Cha ajabu zaidi ikawa si Dowans pekee bali hata Bodi ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu mara hata Maaskofu na Mashehe, wanashangaza zaidi kwa kusema hivi hata hivi " Tunakiomba (sisi UVCCM) chama cha mapinduzi (wao siyo tena sehemu ya chama) kiwashughulikie wale wote waliohusika yaani kamati ya Mwakyembe +Sita kama spika Au Lowasa + hao wenzake waliohusika."
  Nimejiuliza Maswali mengi sana na sijapata jibu lakuniridhisha kuhusu hili tamko la UVCCM, moja labda wamo kwenye chama hiki wakisubiri kuna siku watapata ulaji wa uongozi wa juu wa serikali au kichama sasa wameona ccm inaelekea kufa na hakuna matumaini tena wameamua kumwaga mboga.
  pili, Labda ni janja ya ccm kuteka mjadala wa Dowans ili kuonyesha kuwa hata wao wanaguswa na ishu yenyewe ili tuache kuifuatilia.
  tatu, walikuwa wapi muda wote huo, na hata hivyo kikwete ni Mwenyekiti wao ambaye ni raisi kwanini wasiende kumwambia hayo na kuwataja hao wanaohusika vibaya na Dowans badala ya kuja kwenye Media.
   
Loading...