WanaJF waliojitoa na kutokuwa na imani na serikali ya JK

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
141
8
WanaJF waliojitoa na kutokuwa na imani na serikali ya JK, Hasara nitakuwa wa kwanza kutokana na yanayoendelea katika uongozi wake, na kuwa na washauri wabaya.

Nimejitoa kuanzia leo.
 
hili gurudumu nipo nalo hadi mwisho wa safari, kama ww unajitoa mzee ina maana wengine wakutayarishie njia, haya bana ! mie nilijitoa then nikajiweka tena ! teh teh

sijitoi ng'o, manufaa ya taifa, hasara za taifa ni za wote na sio serikali peke yake, serikali na wananchi wake wangekuwa wananufaika sasa hivi UNGEFIKIRIA KUJITOA ??
 
...hata kama unafika mwisho wa safari likiwa kipara, hali njiani kwenye safari ulipewa uhuru wa kuchagua 'gurudumu jipya'?!

Huu si utakuwa kama ushabiki wa ndondi sasa. Yakuwa, hata kama mwananandodi wako ana masumbwi ya kidemu, lonyo lonyo na haonyeshi kumudu hata round ya pili, wewe bado unashangilia tu na kumpa moyo (wa kinafiki)....hureee hureee hureee, unaweza unaweza kushinda, vumilia tu mwaya round ya tatu hiyooo... nakila konde kutoka kwa mshambuliaji wake linakuwa lina mpelekesha chini....By the time una realise kuwa mwanadondi wako hana lolole; kasha zimia, na yuko 'muhimbili wodi ya mifupa' kupasuliwa mguu!!

...ni muhimu basi kubadilisha hilo 'gurudumu' lako pale unapopewa hiyo nafasi, lasivyo 'mwanandondi' wako atapasuliwa 'kichwa' na kujikuta nchi yetu haina maendeleo milele kwa kung'ang'ania tu 'status quo'.

SteveD.
 
kama kujitoa angejitoa nyerere na mababu zetu kipindi hicho mambo yapo rough kichizi ila sasa njia imekuwa smooth wewe unajitoa, haya mzee kwaheri adios wasalimie huko uelekeako !
 
FD,

Kujitoa ni dalili za uvivu na kukata tamaa kuwa mmepotea mwituni, basi hakuna la kufanya. Je tumwachie nani atafute njia? Ili mpate njia, ni lazima kuendelea kuitafuta tu, hadi ipatikane, muelekee mnakotaka.

"A real man should be judged on his stance during problems."

Tungekuwa baharini ungeomba kushuka kwa kuwa meli imepotea?
 
hili gurudumu nipo nalo hadi mwisho wa safari, kama ww unajitoa mzee ina maana wengine wakutayarishie njia, haya bana ! mie nilijitoa then nikajiweka tena ! teh teh

sijitoi ng'o, manufaa ya taifa, hasara za taifa ni za wote na sio serikali peke yake, serikali na wananchi wake wangekuwa wananufaika sasa hivi UNGEFIKIRIA KUJITOA ??

...Jamani nikiwaambia kada mpinzani karidhika ktk maisha ya kifisadi mtakataa?? anayekataa anyooshe mkono.

Lakini kuna masuala mengine huwa nayatupia macho zaidi ya kisiasa....
 
sasa mzee, mie nampa changamoto kijana asikate tamaa wewe unasema nimeridhika, inakuwaje mkuu hapa ? au meseji not delivered ? ebu soma tena nilichoandika halafu utaelewa ! hao mafisadi wametokea wapi tena mzee ? au wewe mmoja wao ?
 
KADA MPINZANI......

hahhhaahah unanikumbusha ile nyimbo sijui ya DDC au JUWATA kuwa nahodha alijitupa baharini baada ya kuona mawimbi makaili,jamaa wanafikiria ameliwa na PAPA wa baharini.
 
WanaJF waliojitoa na kutokuwa na imani na serikali ya JK, Hasara nitakuwa wa kwanza kutokana na yanayoendelea katika uongozi wake, na kuwa na washauri wabaya.

Nimejitoa kuanzia leo.
vitendo ni bora zaidi ya maneno.kama umeona maneno hayakuleta mabadiliko unayotaka ,jaribu vitendo.kama hilo ndio lengo basi u have my full support.yapo mengi ambayo tukiyafanya tutaonekana kwamba tunapigania haki zaidi ya mijadala ya jf.dont get me wrong guys! naipenda jf na naithamini jf na naamini kama tutaitumia vizuri basi italeta mabadiliko katika jamii.N:B ila kuna wakati inabidi tuwe more real kuliko kuwa fiction all the time. good luck hasara. i might be next. who knows? lakini DONT GIVE UP THE FIGHT.
 
KADA MPINZANI......

hahhhaahah unanikumbusha ile nyimbo sijui ya DDC au JUWATA kuwa nahodha alijitupa baharini baada ya kuona mawimbi makaili,jamaa wanafikiria ameliwa na PAPA wa baharini.

si ndo hapo, sasa sijui atamuachia nani hawa MAFISADI. sasa jamaa wakiamua kuendelea kutafuna nchi na yeye kaamua kulala mbele sijui itakuwaje kwetu sisi walalahoi !
 
sasa mzee, mie nampa changamoto kijana asikate tamaa wewe unasema nimeridhika, inakuwaje mkuu hapa ? au meseji not delivered ? ebu soma tena nilichoandika halafu utaelewa ! hao mafisadi wametokea wapi tena mzee ? au wewe mmoja wao ?

...mheshimiwa kada
nilikuwa nakuchokoza mkuu ili uendelee kuchangia ila ni kweli kwamba kama mtu akijitoa je atamuachia ukombozi??????

ngoma ni kugangamala mpaka kieleweke
 
FD,

Kujitoa ni dalili za uvivu na kukata tamaa kuwa mmepotea mwituni, basi hakuna la kufanya. Je tumwachie nani atafute njia? Ili mpate njia, ni lazima kuendelea kuitafuta tu, hadi ipatikane, muelekee mnakotaka.

"A real man should be judged on his stance during problems."

Tungekuwa baharini ungeomba kushuka kwa kuwa meli imepotea?

Hee kumbe FD ni Hasara...................makubwa!!..........au nimepitwa na hiyo post ya FD kujitoa...........maana sijaiona!!
 
Oh, Ogah, asante umenikosoa...si FD, ni Hasara huyo amejitosa baharini eti hana imani na kingozi...samahani FD, si wewe niliyetaka kumuelezea.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom