WanaJF umeshawahi ku-date na Mpenzi wa mtandaoni ilikuwaje?

Last Night

Member
Jun 19, 2021
20
65
Wacha niwape story yangu kwanza. Nakumbuka huko Facebook nilipata mbaba mmoja hivi tukawa tunachati wee mwisho wa siku tukapanga tuonane.

Basi tukatoka out tukaagiza kuku mzima ndizi tano na ugali juu. Mimi nikala ndizi moja na kama vipande viwili vya nyama basi yule baba akafukia ugali wote na yule kuku alafu akaagiza tena kuku mwingine wa kuchoma tukafungiwa na zile ndizi.

Akaagiza na matunda ndizi, machungwa na nanasi kwenye mfuko tukaenda zetu lodge.

Usiku wa manane nimelala nasikia mtu anakula chwakashwakachwaka kama mchwaa aisee nilishangaa kumbe ni huyo mbaba amekula vyote kama ana funzaa tumboni uwiii yani nilishangaaa .

Kesho nilivyoondoka nikamlima bonge la block.
 
Sijawahi na sina mpango huo. Vipi umeelezea tu upande wa kula. Vipi kuhusu show yake ya sita kwa sita. Alikula kilafi kama alivyokuwa anakula chakula?
 
Back
Top Bottom