WanaJF tunaomuunga mkono Lissu sasa ni muda muafaka wa kumsaidia Lissu ashinde!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,090
Ndugu wana JF, kwa miaka kibao tumepiga makelele humu juu ya udhalimu, ufisadi, uonevu, na incompentency ya serikali za CCM hususan hii ya awamu ya tano

Na kama mnavyojua, Sisi wanachama wa JF huenda ni watu ambao tumo katika kundi la watu wenye elimu na tuna upeo mkubwa wa mambo katika nchi.

Sasa ni jukumu letu kuchukua hatua katika kipindi hiki cha lala salama kusaidia kuuangusha mbuyu ambayo mizizi yake imekuwa ikifyonza hatima njema ya wana wa nchi hii na kuwaacha wakiwa hohe hahe

Sasa mwana JF, ni muda muafaka sasa wa kuingia front, kuchukua hatua na kumsaidia Lissu kushinda

1. Ongea na Familia yako, washawishi walio kwenye himaya yako wamchague Lissu
Kaa chini, waelezee hali yako ya kiuchumi, waelezee hali ya mwenendo wa haki katika nchi, kama una wanafunzi waelezee mustakbali wao kielimu hasa makato ya bodi ya mikopo, waeleze kuhusu athari za kutopandisha mishahara itakavyoathiri hata pensheni yako. Waombe watu wa familia yako wampigie kura Lissu aje aboreshe maisha yao.

2. Wapigie simu ndugu, jamaa na marafiki huko kijijini kwenu, mijini na popote washawishi wampatie Lissu kura
Wanachama wa JF tupo wengi sana, Iwapo kila mmoja atamtafutia Lissu kura kumi tu basi CCM itakuwa na hali mbaya sana.

Hebu tuweke commitment, kila mtu aliyechoshwa na udhalimu wa serikali hii, awashawishi watu angalau kumi anaowamudu wampigie kura Lissu.

Ndugu zangu, hii ishu siyo ya Lissu peke yake, hii ngoma ni yetu sote. CCM wametupuuza kiasi cha kutosha, wametunyanyasa kiasi cha kutosha, sasa tunataka mabadiriko, Sasa ni jukumu letu kusaidia hayo mabadiriko!
 
Yaani tuandamane kwa ajili ya mtu anayeishi ubeligiji

Tena nishawishi familia yangu kumpigia kura msaliti wa Nchi! Hata shetani atanicheka

Tena ameshakata tiketi ya kurudi ubeligiji

Familia yake ameificha, mimi nikavunjwe mguu kwa kumpigania mtu aliyeshindwa Uchaguzi anatoa matusi
 
Yaani tuandamane kwa ajili ya mtu anayeishi ubeligiji

Tena ameshakata tiketi ya kurudi ubeligiji

Familia yake ameificha, mimi nikavunjwe mguu kwa kumpigania mtu aliyeshindwa Uchaguzi anatoa matusi

Mimi kila ninapopita napita na John Pombe Magufuli.

Nimeongea na watu6 leo 5 wanaume mmoja mwanamama mwenzangu.

Wale wanaume kulikua na kijana wa kama miaka25 akaniambia dada hakuna mtu mwenye akili timamu atamnyima kura Magufuli

Mwanaume mwingine wa kama miaka 45 akaniambia mdogo wangu wote hao wanaopiga kelele ni wanasiasa wachumia tumbo. Wafanye siasa tuu ila kura ni kwa Magufuli

Baada ya hapo tukaulizana kuhusu vikatio wakasema viko powaaa nikajiondokea

Wanaomuunga jpm mkono wengi wako mtaani na wameshafanya maamuzi
 
Yaani tuandamane kwa ajili ya mtu anayeishi ubeligiji

Tena ameshakata tiketi ya kurudi ubeligiji

Familia yake ameificha, mimi nikavunjwe mguu kwa kumpigania mtu aliyeshindwa Uchaguzi anatoa matusi
Kura yako ni ya muhimu sana kwa Mh: Tundu Lissu ktk kulikomboa taifa letu dhidi ya kupe wa kijani waliolinyonya kwa zaidi ya miaka 50.
Note: Usisahau kuhamasisha ukoo wako wote ili tuungane kulikomboa taifa letu pendwa kutoka kwa kupe hao wa kijani.
 
Katika hayo mawili nimefanikiwa 99%!
Mpaka sasa nimefanikiwa kupata wafuasi ambao walikuwa watumwa wa ccm wamebadili upepo sasa huwaambii kitu wakakusikia kuhusu Lissu.
Besides, mama yangu alijivua nafasi za uongozi wa wanawake ccm, bendera ya kijani nyumban akaishusha na kuchoma moto,, ukweni vivyo hivyo.
Mke wangu karudi kwao hivi majuzi ikiwa ni maandalizi ya kujifungua na pia kupata fursa ya kumpigia kura Lissu.
Kesho inshallah nitakuwa njiani kurejea kijijini kutia msumari wa mwisho kwenye jeneza la ccm
 
Mimi kila ninapopita napita na John Pombe Magufuli.

Nimeongea na watu6 leo 5 wanaume mmoja mwanamama mwenzangu.

Wale wanaume kulikua na kijana wa kama miaka25 akaniambia dada hakuna mtu mwenye akili timamu atamnyima kura Magufuli

Mwanaume mwingine wa kama miaka 45 akaniambia mdogo wangu wote hao wanaopiga kelele ni wanasiasa wachumia tumbo. Wafanye siasa tuu ila kura ni kwa Magufuli

Baada ya hapo tukaulizana kuhusu vikatio wakasema viko powaaa nikajiondokea

Wanaomuunga jpm mkono wengi wako mtaani na wameshafanya maamuzi
Naomba Mungu next time ukutane na mimi ili uweze kunishawishi nimpigie kura Magufuli
 
Yan tangu Jana machozi yananitoka, naamini Tundu Lissu anashinda sasa je watamtangaza?
Yan sijui matokeo yakitoka nitakuwa katika hali gani jamani Naomba mniombee
Jiandae kisaikolojia,unachokitazamia huenda kisiwe uhalisia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom