WanaJF! Kwa mwenye kujua vizuri hili a2juze wengine kwn Mi naona haiwezekani:

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,216
Nimekaa na washkaji wangu hapa tunabadilishana mawazo kutokana na hali halisi ya maisha yalivyo: Sasa mmoja kati ye2 anavuta sigara,mwenzangu akachukua kile kiberiti akatoa njiti akawa anachokonolea sikio,ndipo mwenye kiberiti akamdakia na kumpa tahadhari asirudie siku nyingine na akimwonya ya kwamba ile baruti iliyowekwa kwenye njiti ya kiberiti ni rahisi kulipuka ndani ya sikio na akatoa mfano ya kwamba miaka kidogo ya nyuma kuna jamaa wake kapatwa na jambo kama hilo na jamaa akaendelea kuchonoa sikio lake lakini ametusisitiza hilo ya kwmb msipendelee kwn ni soo sana. NAMI NIKASEMA NGOJA NIWAJUZE KAMA KUNA ANAYEWEZA KU2FAFANULIA. Nawasilisha!!!!
 
Mhm, baruti kulipuka si mpaka ipate msuguano wenye kusababisha joto kali ama?
 
ili iripuke ni lazima isuguliwe kwenye rough dry surface so kwenye masikio kuna nta kazi yake kurainisha ngoma ni vigumu hilo swala kutokea.
 
ili iripuke ni lazima isuguliwe kwenye rough dry surface so kwenye masikio kuna nta kazi yake kurainisha ngoma ni vigumu hilo swala kutokea.

Ama labda ule uchafu utokao sikio ndiyo lenye uwezo wa kufanya mlipuko. Lakini bado ni ngumu si rahisi kivile.
 
.....Sasa mmoja kati ye2 anavuta sigara,mwenzangu akachukua kile kiberiti akatoa njiti akawa anachokonolea sikio,ndipo mwenye kiberiti akamdakia na kumpa tahadhari.....!!
Kwa kuwa ni tahadhari ni sawa kwa sababu nyingi moja wapo ni hatari ya kuweza kudhuru ngome ya sikio endapo litafanyika kosa lolote. Kuhusu baruti kulipuka hilo haliwezekani labda kwa sababu ilikuwa ni story za kijiweni.
 
Kwa kuwa ni tahadhari ni sawa kwa sababu nyingi moja wapo ni hatari ya kuweza kudhuru ngome ya sikio endapo litafanyika kosa lolote. Kuhusu baruti kulipuka hilo haliwezekani labda kwa sababu ilikuwa ni story za kijiweni.

Mkubwa! Nilihakikishia ya kwmb hili haliwezekani,jamaa akaniapii akidai imemtokea rafiki wake wa karibu na kwa bahati mbaya alitaka kumpigia jamaa jirani na aliyetokewa na tukio na kw bahati mbaya majira ile mtandao wa VodaCom ikawa haitoki. Ila ngoja kama nitamtia machoni kesho nitamwambia aseme na aliyepatwa na mkasa then nitawajuza wadau.
 
Mkubwa ci umesema mlikuwa kijiweni!
That why,maana story za kijiweni uwa ndo kawaida.cku inapita.
 
Kwa njiti za viberiti vya sasa siyo rahisi kulipuka. Hata hivyo zamani tulikuwa na viberiti ambavyo njiti zake unaweza kuwashia kwa kutumia sakafu,soli ya viatu au sehemu yeyote yenye friction hata kidogo!
 
Njiti haiwezi kulipuka. Nta ya masikio haiwezi kufanya reaction yoyote na baruti. Hizo ni imani tu, mbona nilipokuwa mdogo nilisikia kuwa ukiingiza ufunguo masikioni utasikia ngoma inadunda, pia nilikuwa naamini maji yakiingia sikioni yanaweza kutokea kwenye sikio lingine.
 
niliwahi kusikia hii kitu, ila sina uhakika kama ilikuwa kweli au uzushi. Ila kuna thread ililetwa hapa ikihusisha jambo hili na maumivu makali ya kichwa. Hivyo ni vyema kuacha haya mazoea
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom