Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
Mjadala wa Dowans umezidi kuendelea. Wazungumzaji wamekuwa wengi. Kila mtu anatoa mawazo yake. Kila mtu anatoa msimamo wake. Mtanzania wa kawaida haelewi nini cha kufanya. Mjadala wa wasomi unamuhusu nini? Kinachomuhusu yeye ni ugumu wa maisha zidisha mara tano!!
Humu jamvini ni post baada ya post, Dowans! Dowans! Dowans! Mpaka watalipwa sisi tunapiga story tu! Mawazo yanayotolewa ya nini kifanyike yanaishia hewani!!
Watu wanataka kuandamana lakini hakuna tarehe inayopangwa, hakuna maandalizi yanayofanyika! Inakuwa kama tumepigwa butwaa.
Najiuliza, hivi mtu akibakwa mara kwa mara anaishia kulia tu bila kupiga kelele? Je anafika mahali anabaki kumwangalia mbakaji bila kuomba msaada? Eti akipiga kelele atakosa mtu wa kumuoa au akiolewa watu hawatamchangia!!
Huu ni upunguani. Humu jamvini tunaongeleshana, tunajibizana na kushauriana lakini hujui unamshauri nani, unajadili na nani na matokeo yake ni yapi. Hapo ndipo ugumu wa utekelezaji wa mapendekezo unapotokea!! Inakuwa ni kupiga story tu!!
Unafiki unachomoza, uoga unadhihirika!
Nafikia mahali naanza kuvisualize posts zitakazo andikwa siku Dowans wanalipwa! Lakini itakuwa too late!! Tutakuwa tushabakwa tunabakia kulalamika na kumuachia Mungu amlaani aliyetubaka!!
Tukubaliane cha kufanya, tarehe ya kufanya, mahali pa kufanya na jinsi ya kufanya. Kama hatuwezi basi tuharakishe walipwe maisha yaendelee. Kama huwezi kuzuia kubakwa basi tembea na kinga mbakaji akija mpe atumie usipate maambukizo na mwambie amalize haja yake haraka wewe uwahi kufanya mambo mengine!!
Kwa kitakachopendekezwa nitashiriki. Kama ni kwa mkoa Arusha nitashiriki kikamilifu.
KUMBUKA.
1. Hatupingi sheria kwamba ukishtakiwa na ukashindwa kesi unatakiwa kulipa.
2. Hatupingi kwamba tumesaini treaty/convention iliyoanzisha ICC.
Tunapinga;
1. Mkataba feki kati ya Richmond na Tanesco kuidhinishwa na kutoa haki kwa Dowans hata kama tumechelewa kupinga.
2. Tunapinga uharaka wa kulipa deni hilo. Na pia matisho kwamba tutanyimwa misaada. Sasa kama ni misaada si watusaidie kulipa hilo deni? Si msaada pia? Au?
3. Tunapinga kauli mbalimbali kwamba Dowans lazima walipwe bila kujaribu kuweka pressure ili kujua ukweli wa kilichojiri mpaka tupo hapa tulipo.
Tunataka;
1. Aliyeisajili Richmond nchini bila kujiridhisha uhalali wake awajibishwe. Tumjue ni nani na hatua gani zimechukuliwa.
2. Tunataka aliyeshiriki mazungumzo na Richmond i.e vikao nk awajibishwe na atueleze aliifahamuje hiyo kampuni na alifanya due diligence search akagundua nini mpaka wakasaini mkataba.
3. walioshauri kuvunja mkataba na kupongezwa na PM watoe maelezo kwa nini walitushauri vibaya na ikiwezekana tuwafungulie mashtaka kwa professional negligence na kudai fidia.
4. Waliotuwakilisha huko ICC au hotelini watueleze wameshindwaje kesi hii. Ni uwezo mdogo au walifanya makusudi?
5. Dowans hatuna hela za kuwalipa sio kwamba hatutaki peke yake. Mdaiwa hafungwi jamani. Na sheria inakataza kushika mali za serikali sasa tusipolipa inakuwaje? Mbona Omar Bashir amegoma kwenda the Hague na bado anaendelea na maisha? Huu wema wetu utatuponza!
Tufike mahali tuamue na tutende! Hakuna cha kusubiri!