Wanajeshi wastaafu kulipwa mishahara ni haki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi wastaafu kulipwa mishahara ni haki?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kabindi, Feb 22, 2011.

 1. k

  kabindi JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nasoma gazeti la Tanzania Daima uk wa 6, kwamba wanajeshi wastaafu wana faraja kubwa hasa baada ya serikali kusikiliza maombi yao ikiwa ni pamoja na kuzikwa kijeshi na kuwalipa mishahara baada ya kustaafu!
  Naomba mnieleweshe kama wanajeshi ni taaluma nyeti kuliko taaluma nyingine kama Madaktari n.k?, hiyo Bajeti ya kuwalipa mishahara imepitishwa na nani na sheria ipi?! kwani kwenye mishahara yao huwa hawana makato ya uzeeni kama wafanyakazi wengine wa Serikali? Shule zetu za kata hazina walimu, Maabara na wala madawati! pesa tuwapatie Wanajeshi eti mishahara baada ya kustaafu???! Mimi naona si haki hata kidogo, naona kama ni janja ya CCM kuwajaza mapesa watu wa usalama ili waendelee kuwaibia kura milele! WATANZANIA TUKATAE UJINGA HUU!
   
 2. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 480
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Hakuna mwanajeshi analipwa mshahara baada ya kustaafu zaidi ya pension yake kama wastaafu wengine. Mkuu wa majeshi na team yake kuanzia Maj Gen kwenda juu ndo wanaendelea kupata mafao kama maafisa wakuu wa serikali wengine kama PM, majaji, rais, makamu etc. Huo ni upotoshaji na sio kweli tena hata hao wanaopata mafao yanakuwa based kwenye level ya mshahara wake wa mwisho so kwa wale waliostaafu zamani wkt mishahara haijawa mikubwa wanateseka sana japo walikuwa ma cdf etc. Ukisikia pension na mafao anayopata Gen Musuguri na Mboma unaweza kutokwa na machozi kwa jinsi tofauti ilivyo kubwa.
   
 3. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,067
  Likes Received: 1,607
  Trophy Points: 280
  Great Sinker.....!
   
Loading...