Wanajeshi wapiga raia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi wapiga raia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MndemeF, May 10, 2011.

 1. M

  MndemeF Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna habari kuwa wanajeshi wa jeshi la la wananchi wa Tanzania(JWTZ) kutoka kambi ya Kunduchi wamewapiga na kuwajeruhi vibaya baadhi ya wananchi waishio karibu na kambi hiyo iliyopo karibu na machimbo ya kokoto ya Kunduchi. Kila upande wa wahusika hao yaani wapiganaji na raia wanajaribu kutoa sababu za kuvutia upande wao. Kwa vovote iwavyo kwa upande wangu mimi sidhani ni halali kwa wanajeshi kupiga raia wasio na silaha na kuwapa adhabu kubwa za kijeshi. Ningependa kutoa rai ifutayo Kwa wanajeshi wetu.

  MOJA: Kumbukeni kuwa hamtakuwa wanajeshi milele yote siku ikifika mtarudi na kuwa raia wa kawaida mtakuja kukaa mtaani na sisi, je tuwatenge? Kulikuwa na wababe zaidi yenu leo wapole tupo nao mtaani.

  PILI: Pamoja na kuwa mnaishi kambini lakini mara nyingi huduma nyingi mnapata uraiani, je mkija huku na siye tukatae kuwauzia? Si tunakunywa wote mtaani ingawa mna club zenu za bia za sawa na bei ya bure?

  TATU: Kumbukeni kuwa IDDI AMIN alipigwa kirahisi na majeshi ya Tanzania kwa msaada mkubwa kutoka kwa raia wa kawaida wa Uganda ambao walichoka na unyanyasaji wa vikosi vya Amin.

  NNE: Hata raia pia wanajua kutumia silaha pale wanapochoka na manyanyaso. Kwa taarifa yenu kama hamjui asilimia kubwa ya waasi wa LIbya wanaopigana dhidi ya Gaddafi ni raia wa kawaida lakinileo wanarusha maroketi na kutumia silaha nzito nzito hata kufikia kuwarudisha nyuma makomandoo shupavu wa Gaddafi.

  HITIMISHO: Tunataka jeshi lenye nidhami lenye kuzingatia utawala wa kihseria. Hivi lini mmesikia wanajesi wa marekani wamepiga raia? Ushauri wangu kweni ni huu, kama mmechoka kukaa makambini ni heri mkamuomba amiri jeshi mkuu awape ruhusa muende huko Somalia au Afghanistan mkalinde amani.
   
 2. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lazima wapigwe kwani wote wapambe wa ccm.
   
 3. Unyanga

  Unyanga JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hakuna haki kwa sababu kila mtu anamuonea mwenzake kwa nafasi yake, poleni wananchi wa kunduchi muda si mrefu haki yenu itasimama na mtashinda vita vyote vya uonevu kwa ssababu dunia hii hakuna mtu aliyetawaloa na kunyanyasa wenzake milele na sikun zote lazima washuke chini na wao waonewe:A S cry::A S cry:
   
 4. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wanajeshi mnawapiga wananchi(ndugu zenu)mnaowalinda?au ndio kusema Tanzania haina jeshi!!!?acheni uonevu pls
   
 5. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  wanajeshi wa bongo wanadhani ni ujiko kuwafanyia ubabe raia
   
Loading...