Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Status
Not open for further replies.

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Wakati Membe akitamba kuwa alienda mbele ya kamati ya maadili ya CCM kuwafunda na kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali, Kinana amegoma kufika mbele ya kamati hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Kinana ameona ni kama kudharauliwa kwa kuitwa kuhojiwa mambo ambayo kimsingi ni malalamiko aliyotoa kuhusu namna alivyokuwa akipakwa matope na mtu anayejiita Cyprian Musiba. Inaelezwa kuwa aliyetakiwa kuitwa ni Musiba na siyo Kinana.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ndani ya chama, Kinana jana ijumaa alitakiwa kuwepo mbele ya kamati hiyo ya maadili lakini alisubiriwa hadi jioni na hakuna taarifa yoyote rasmi iliyopatikana juu ya kutokuhudhuria kwake mbele ya kamati hiyo.

Aidha hakutuma ujumbe wowote wa udhuru kuelezea kuhusu yeye kushindwa kufika mbele ya kamati hiyo kama ilivyopangwa.

Tusubiri tuone.
 
Komredi Kinana kaona utoto kwenda, hata wakimpa adhabu ya kumfuta uanachama bado ni alama tosha ya CCM hata asipokuwa na kadi! Sio watu Kama Bashite,Kitila, Waitara, Bashiru, Pole pole ambao hata hadhi ya ushabiki wa chama hawana hata wakiwa na kadi!

Kwa Membe it's ok kwenda bado ana future ndani ya Chama. Nahisi soon Komredi Mangula ataomba kujiuzulu kupisha siasa za 'kihuni' ndani ya Chama.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom