Wanajeshi wampiga trafiki kikatili, wadai kucheleweshwa Ubungo Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi wampiga trafiki kikatili, wadai kucheleweshwa Ubungo Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Makaayamawe, May 20, 2009.

 1. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanajeshi wampiga trafiki kikatili wadai kucheleweshwa Ubungo Dar

  [​IMG]

  Kikundi cha askari wa usalama barabarani wakimsikiliza Mkuu wa kituo cha usalama barabarani mkoa wa Kinondoni, ASP Awadhi Haji (katikati) akiwasiliana kwa radio mara baada askari aliyekuwa akiongoza magari katika makutano ya Ubungo, Sajini Thomas Mayapila (kulia) kupigwa na askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) waliokuwa wakitoka Mwenge kwa mabasi, kwa madai ya kuwachelewesha safari yao.Na Mwandishi Wetu

  ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), jana walimshambulia na kumpiga askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Thomas Mayapila, wakidai aliwachelewesha kupita eneo la Ubungo.

  Tukio hilo lilitokea jana asubuhi wakati Thomas akiwa kazini kuongoza magari katika makutano ya Barabara za Morogoro, Sam Nujoma na Mandela, Ubungo, eneo ambalo kwa kawaida huwa na misululu mirefu ya magari nyakati za asubuhi na jioni.

  Tukio hilo lilitokea saa 1:35 asubuhi wakati trafiki huyo akiendelea na kazi yake ya kuongoza magari katika eneo hilo, akionekana kutofahamu kuwa kulikuwa na magari matatu ya JWTZ yaliyokuwa yakitokea Barabara ya Sam Nujoma na kuelekea Buguruni.

  Tofauti na siku ambazo JWTZ huwa na shughuli rasmi, magari hayo matatu- 1931 JW08,1908 JW08 na Land Rover Defender lenye namba 2994 JW08- hayakuwa yakiongozwa na gari lenye king'ora wala ishara yoyote.

  Baada ya magari hayo kupita eneo la makutano ya barabara hizo, maarufu kama Ubungo Mataa, wanajeshi wawili walishuka mmoja akiwa na cheo cha staff sargent ambaye alishika mkanda wake mkononi na dereva wa basi, na kumtupia maneno ya vitisho trafiki huyo na baadaye kuanza kumpiga makofi na ngumi.

  Hata hivyo, trafiki huyo alionekana kuwa mkakamavu baada ya kutumia mbinu nyingi za kujihami, zilizowafanya wanajeshi wengine washuke kwenye magari yao na kwenda kumchangia.

  Wingi wa wanajeshi hao waliokuwa wakimgombea mithili ya kunguru kwenye mzoga, ulimshinda polisi huyo na akajikuta akiangushwa chini na kukanyagwa shingoni mithili ya kuku anayesubiri kuchinjwa.

  Wakati wakiendeleza ukatili huo, wanajeshi hao walikuwa wakimkejeli trafiki huyo na kazi yake, kana kwamba si chochote na kudai alikuwa akiwachelewesha kwenda kutekeleza majukumu yao, huku polisi huyo akihoji uhalali wa kumvamia na kumpiga.

  "Kwa nini mnanipiga na mimi nipo kazini kama ninyi, niambieni sababu ya kunipiga... na mimi ninatimiza wajibu wangu hapa. Nimeajiriwa na serikali kama nyinyi," alilalama Sajenti Thomas wakati akipigwa na wanajeshi hao.

  Umati uliokuwa ukishuhudia kipigo hicho ulikuwa ukimshangilia trafiki huyo kwa ujasiri wake wa kujihami na kuwazomea wanajeshi hao kabla ya askari mwenye cheo cha Luteni Kanali kutokea na kuamuru askari wenzake kumwacha trafiki huyo. Wote wakaingia kwenye magari yao na kuondoka eneo hilo.

  Tukio hilo lililodumu kwa takriban dakika 18, lilisababisha magari yaliyokuwa kwenye msululu kutosogea na hivyo kuongeza msongamano kwenye eneo hilo linalohitaji uongozi wa ziada nyakati za asubuhi na jioni wakati watu wakielekea makazini na kurejea nyumbani.

  "Ni kama sinema ya bure kuona mwajiriwa mmoja wa serikali anatimiza wajibu wake halafu mwajiriwa mwingine wa serikali anatokea na kuingilia utendaji huo na kumhukumu.Hii inatushangaza sisi wananchi tunaoamini kuwa wote wapo kututumikia," alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

  Dakika chache baada ya askari hao kuondoka, walifika trafiki wengine sita wa vyeo tofauti akiwemo mrakibu msaidizi wa polisi, Awadh Haji ambaye ni mkuu wa kituo cha usalama barabarani cha Kinondoni.

  Haji alimpa pole Sajenti Thomas na kumshauri aende kando ya barabara kujipumzisha na baadaye Thomas aliondolewa eneo la tukio na afande Haji akiongozana na wenzake wawili waliotumia gari aina ya Toyota Chaser namba T370AZR na kuacha wananchi wakiwashangilia.

  Baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo walisema wako tayari kutoa ushahidi iwapo trafiki huyo atakwenda mahakamani na kuwashtaki askari hao.

  "Unajua si mchezo, umepambana na askari wote wale waliokuwa wanataka kukuonea duh, unastahili pongezi na kuongezwa cheo. Tutatoa ushahidi wetu ukienda mahakamani, tupo tayari," alisema mmoja wa mashuhuda kabla ya Sajenti Thomas kuondolewa eneo la tukio.

  Mwananchi ilitaarifiwa kuwa trafiki huyo aliandika maelezo yake kituo cha Oysterbay.

  Tayari Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na JWTZ wameunda tume ya pamoja kuchunguza tukio hilo kwa siku moja, anaripoti Ummy Muya.

  Kamanda mwandamizi wa polisi wa kanda ya Dar es salaam, Suleiman Kova, akiwa ofisini alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea nyakati za asubuhi, lakini mpaka anazungumza na Mwananchi bado tume hiyo haikuwa imemkabidhi taarifa za tukio hilo.

  “Ni kweli leo asubuhi kulitokea tukio hilo la wanajeshi kumpiga askari wa usalama barabarani katika eneo la Ubungo, lakini hatufahamu ni nini hasa kilichosababisha wanajeshi hao kufanya kitendo hicho,” alisema.

  “Wananchi wema walinifikishia taarifa kwa njia ya simu wakati wa tukio. Kutokana na kuwa na mahusiano mazuri, tumeunda tume ya pamoja ambayo mpaka leo jioni (jana) taarifa itakuwa tayari.”

  Wakati huohuo, Kamanda Kova alithibitisha kukamatwa kwa watu watatu ambao wanasadikika kuwa walipanga njama za kwenda kuiba katika duka moja la kubaidishia fedha Mei 8 eneo la Kariakoo.

  Kamanda Kova alisema waliwakamata watu hao Jumapili iliyopita na kuwataja kuwa ni Abdallah Mohamed, 25, mkazi wa Yombo Kisiwani, ambaye Kova alikutwa na bastola aina ya Chinese inayotumiwa na vyombo vya dola ambayo inasadikiwa mtuhumiwa aliifuta namba. Mtuhumiwa mwingine, kwa mujibu wa Kova, ni Hatibu Ibrahim, 29, ambaye ni mkazi wa Mtoni Kichangani na Hassain Mzava, 39, maarufu Mzungu ambaye anaishi Yombo.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wanajeshi wengine bongo wako barbaric na hawana discipline, huyu anatakiwa kuwa court marshalled.

  Ila jeshini kuna ushabiki wa kitoto sana wa jeshi vs Polisi, I doubt atawajibishwa.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  May 20, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Wapumbavu sana hawa wanajeshi. Mano a mano hawaziwezi ndondi hawa. Kinachowapa jeuri ni kutembea kwa makundi makundi
   
 4. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  No one is above the law,they should be disciplined!
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hawa Wanajeshi wana tabia mbaya sana.

  Labda ni kwasababu hawajapata kasheshe siku za karibuni

  ndo maana wanatamani kupiga watu ovyo. Ile ya Comoro

  ilikuwa ndogo mno.

  Ngoja waende Darfur tu, huenda wakirudi huko hamu

  zitakuwa zimewaisha!
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mtihani huo Kamanda Kova.
   
 7. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  Sidhani kama kuna haja ya kuunda tume wakati lililotokea ni kosa la wazi la uvunjaji wa sheria. Sheria inapaswa ifuate mkondo wake kwa kuwakamata wahusika na kuwafikisha mahakamani. Zaidi ya yote;
  1. Kosa la kumshambulia Polisi (Assault) inatakiwa lipewe uzito wa hali ya juu Tanzania na hukumu kali kwa wahusika itolewe, bila hivyo polisi watakuwa wanafanya kazi yao kwa woga.
  2. Askari walioshiriki kumpiga huyo Polisi inapaswa wachukuliwe hatua kali za kisheria (mahakamani) na pia adhabu kali kutoka jeshini (kama kuvuliwa vyeo, kufukuzwa kazi n.k.) ili kudhibiti vitendo kama hivi vya kihuni visije kujirudia.
  3. Askari wote wa JWTZ waliokuwepo kwenye tukio hilo hata kama hawakushiriki kumpiga huyo polisi, lakini walishindwa kuchukua hatua kuwadhibiti wenzao wanatakiwa nao wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.
   
 8. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Na hii nayo ni breaking news?? Jambo limetokea jana asubuhi na watu wameshaipata kwenye vyombo vya habari jana hiyo hiyo lakini plp wanakimbilia hapa kuleta habari as breaking news mweh....... I love Tanzania
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Amiri Jeshi Mkuu watafutie mfupa wa kutafuna vijana hawa!.
  Vita ya ukombozi imeisha lakini Somalia ipo.Wapelekwe huko kama Ethiopia walivyofanya.
   
 10. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Tanzania bana kiboko, sasa tume ya nini tena? Wamempiga polisi, mashahidi kibao na sababu ya kumpiga ishasemwa wazi lakini wanaunda tume ya kuchunguza.
  Huyo Lt. Col alitakiwa aweweke chini ya ulinzi mpaka MP waje lakini naye kwa makusudi kawaachia wapande basi.
  Hakuna kesi hapa.
   
 11. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hii "Breaking News" ili break lini?

  Jamani, sio lazima useme "breaking news" ndio habari iwe na mshiko. JF tutaonekana tuko nyuma kihabari, na mbali na maeneo ya matukio. Hii nyeti mjini ni old news ya siku tatu sasa. Traffic hakupigwa leo wala jana. Breaking news ni kwako wewe Makaayamawe, acha kutiatia chumvi habari Mkuu.
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tukio hili la aibu ni dalili za wazi kuwa Wanajeshi wana upungufu wa nidhamu. Vile vile wanadhani kuwa kazi zao ni muhimu kuliko za wengine, au wanafikiri nchi hii haina sheria na wao wako juu ya sheria zote. Nadhani pia ni dalili ya ukosefu wa wa subira kwa hali ya juu.

  Wanajeshi hao hawatafanywa lolote, hata kama zitaundwa tume 100. Hali hii ya uvunjivu wa sheria kwa makusudi inaanza kuwa jambo la kawaida kwenye taasisi mbalimbali.

  Sijui kwanini wananchi hawakumsaidia askari yule wa barabarani, na badala yake wakabaki kumshangilia. Angeweza kuuawa pale katikati ya barabara bila msaada wowote. Watu wanabaki kusema wako tayari kuwa mashaidi. Wakifuatwa kutimiza ahadi zao sidhani kama wataonekana tena.

  Mambo haya ni ya aibu sana. Rank zetu za utawala kimataifa ziko chini sana. Inabidi serikali kuweka utawala bora wa kweli. Askari polisi wetu wanafanya kazi katika mazingira magumu halafu wenzao wanakuja na kuwashambulia kama vibaka!!!!!!!!! Mambo gani haya?
   
 13. Lyampinga

  Lyampinga Senior Member

  #13
  May 20, 2009
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Tume ya nini tena, kwanza hii ni police case, hii ni assault kwa police officer, halafu hifwate na displinary action to these silly soldiers from their seniors na hii lazima hiwe demotion ya vyeo ya hawa wanajeshi wanaochukua sheria mikononi
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kawaida yao, maji hawalipi wakikatiwa maji wanapiga dawasco halafu polisi inaunda tume, leo wamepiga traffic tume inaundwa kuchunguza. Is it relly necessary ? No one is above the law.
   
 15. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #15
  May 20, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa kila kitu Tanzania lazima kiundiwe tume, usishangae wezi wakuku wakikamatwa mtaambiwa waundiwe tume ili mradi tu watu fulani fulani waonekane wanafanya kazi mweh....
   
 16. Lyampinga

  Lyampinga Senior Member

  #16
  May 20, 2009
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Hii kitu ni very straight forward, wanajeshi wamekuwa accused of assaulting a police officer, why not arrest them as what would happen to other citizens, hizi double standard zinatoka wapi. Tume, tume za nini zote hizi, kazi wanataka walipane posho ya kila kikao cha hiyo tume halafu waje waseme hakuna hatua zozote zitazochukuliwa wakati ushaidi wa watu hupo na watu walikuwa wanashangilia wakati yule polisi anapigwa
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  OK,lets face it wanajeshi wana makosa ..lakini tukiangalia ktk large picture, kitendo cha askari wa usalama barabarani, iwe popote pale, kuongoza magari wakati taa za kuongoza zipo ni kitendo ambacho ni very un-scientific and un-economical..
   
 18. Lyampinga

  Lyampinga Senior Member

  #18
  May 20, 2009
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  This is another issue, kuna matatizo ya umeme na taa zetu za dar they dont do justice kwenye njia nyingine, barabara kama ya morogoro rd taa zinaruhusu magari for less than three minutes, sasa na hile foleni ya jioni bila traffic officer magari yataenda vipi
   
 19. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #19
  May 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Si kweli bwana kulingana na trafic zetu bongo na barabara zenyewe zilivo, na peak hours! Afu taa zetu bongo hazina sensor/detector kama za wenzetu mkuu

  Mfano asubuhi kusema mataa ndo yaongoze na ile mida ya jioni si sawa mkuu, kwani kunakuwa na magari mengi toka ama kwenda mjini kwa kipindi fulani, hivyo trafic ni muhimu kipindi hicho.

  Kwa wanajeshi,
  Kwakweli ubabe wao umezidi, yaani wao wanajiona wako juu ya sheria ni miungu watu, wakiamua kupiga watu ni twende tu? hivi kweli hilo ndo jeshi la wananchi?

  Kwa mwendo huu, hilo ni jeshi la wenyewe si la wananchi tena!
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nadhani nchi nyingine especially zilizoendelea wana traffic load kubwa tu kuliko sisi na yet sijaona wakitumia traffic police kwenye intersection. mambo ya umeme au muda wa magari kuruhusiwa ni suala tu la kutafuta na ku-install right technology will do the trick..hamna uchawi.
   
Loading...