WANAJESHI wameanza kufyatuka kupaza sauti kudai mabadiliko

Brother acha kujidhalilisha....!

Mbona hiyo ni sehemu ya job description yake, au hujajua tu. namkubali sana jamaa maana yeye hajali anaandika nini wala wananchi watamchukuliaje. Ni kama vile dafu limewekwa sehemu ya kuwazia.
 
Chadema wamekuwa watu wa kurukia matukio na kuyatolea matamko sasa huyu msemaji wa Chadema amekuwa msemaji wa Wanajeshi, kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa Wanajeshi walichosema wanataka mabadiliko ya kiutawala Chadema wachukue nchi.
Hivi wewe Ritz alichokosea Makene ni nini? yeye ametoa tafsi yake kwa kile alichokisoma kwenye gazeti na ndio maana kuepusha kueleweka vibaya ameweka na source ya taarifa iliyomfanya akatafakari kwamba kengele ya mabadiliko imeanza kusika hata kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na ikiwa hivyo basi kazi ya kuleta mabadiliko itakuwa rahisi,hiyo ndio ilikuwa tafsiri ya Makene.kwani wewe ulivyosoma hiyo habari ya kwenye gazeti umetafsiri nini?
Ila kikweli nimefarijika sana kuona majeshi yetu nayo yanachukia ufisadi na hii ni dalili nzuri ya kupata ukombozi wa nchi kutoka mikononi mwa mafsiadi waliojificha kwenye CCM
 
Hiyo ni mbinu mojawapo ya kujificha na kisha baadaye kumshambulia adui kimya kimya inaitwa camouflage. Si kuna msemo unaosema mchawi mpe mwana alee, sasa mwana anataka kupewa mchawi eti amlee! Baba yao hao watoto (wanajeshi wa 411 KJ) ni mjeshi.Hiyo 411 KJ nafikiri hii itakuwa Makutopola manake nakumbuka mambo ya mabogi wakati ule nipo 841 KJ pale Mafinga.

Kwa malezi mazuri anayowapa siku hizi toka ameingia Ikulu na kuwa amiri jeshi mkuu, nani atathubutu kumsaliti. Baba anakumbatia mafisadi, wengine wakiwa ni watumishi wa jeshi wastaafu, unakumbuka issue ya Iddy simba na Jenerari Mboma kuhusu sukari? Ni juzi juzi tu hapa huyu afande wa Suma JKT na wenzake sijui eti wamevunja sheria na kanuni za kilimo kwanza kwa kula pesa za mwenye pesa bila kumwomba, sasa wanashughulikiwa.

Wanajeshi wamefungwa midomo kwa kupewa nyongeza katika mishahara yao kimya kimya, mapololo kibao (mgawo wa chakula),mikopo toka kwenye mabenki, madaraka serikalini (wakuu wa wilaya na mikoa) kwa waliostaafu na kukumbukwa na afande mkuu.Mwanajeshi gani huyo anayeweza kumrudi baba yake ambaye naye ni mjeshi? Si mnasema mtoto wa nyoka ni nyoka au kageuka tena kuwa kamongo?
 
Naona watu wameacha mada na kuanza kumkimbiza mwehu. Achana uyo mwakilishi wa mashetani apa jf!
 
Mi nawaunga mkono 100% na sioni sababu ya kuwabeza mawazo yao na kuwaita wanafika kwa sababu hayo ni mawazo ya baadhi ya wanajeshi na sio wote na wamesema hivyo baada ya kuona madudu yaho mnayoyasema na zaidi wakaongezea kuwa na wanajeshi nao wapigwe risasi wazi wazi, kwa kujua baadhi yao na wakubwa zao wanahusika katika ufisadi huo.
 
Wanajamvi,

Nimekuwa nikitafakari juu ya hali halisi kuhusu mstakabali wa nchi yetu. Kweli Mwenyezi Mungu aliipendela Tanzania akatupa utajiri wa asili yaani madini,mafuta gase,wanyama mito, bahari,misitu na zaid ardhi yenye rutuba!pia aliendeleea kwa kuweka watu (watanzania)wapole na wanyenyekevu, ili kusudi waweze kufaidika na zawadi za asili alizotupati.

Cha ajabu watu tuliowapa dhamana ya kusimamia na kupanga utumiaji mzuri wa mali asili hizi,hawana utu, ni wauwaji, wezi, wanyang'anyi, mafisadi, wasiowajibika, wenye kujilimbikizia mali,wapenda sifa na wenye kulewa madaraka na kutudhalau sie tuliowapa dhamani hii. Tanzania iliyokuwa sehemi tulivu isiyo na matabaka,yenye amani, leo hii imekuwa tanzania yenye matabaka ya hali ya juu,isiyothamini uhai,yenye watu wa juu na wachini!!!!mpaka Mungu anatushangaa.

tanzania si nchi huru tena,bali inawakoloni wanaotutawala kwa mabavu i hali sie wenyewe ndiyo tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Matabaka yamejenga chuki, baina yetu, wafugaji na wakulima hawaelewani, wafanya biashara na waajiliwa hawelewani, yote hii ni kwasababu ya utawala mbovu ambao umejaawatu watu waasi wasikuwa hata na hofu ya mungu,wamejetengenezea miungu na pengine wao wenyewe wanajifanya miungu watu.

Ushauri wangu kwa watanzania wote,tuwakatae hawa vuongozi wasiokuwa na utu. kwa wale watu wa bariadi,tunaongozwa na wabunge vivuli kwa mda mrefu na wamekuwa wakitumia umasikini wetu na mabavu na wakati mwingine kupoteza maisha ya watu sababu ya kujiona wapo juu ya sheria. Nawomba tuungane oamoja kuhakikisha majimbo yote mawili yanaondoka kwenye mikono ya hao mafisadi na tuwe na viongozi wenye uzalendo!

wenu
bariadi2015
 
kweli kabisa!lakini huko bariadi hawajahitaji mabadiliko,wapo kimya utadhani hao wabunge wao wanafanya kitu.ngija tusubiti landa watakutafuta ili muunganishe nguvu kuyangia hayao magamba mawili.
 
mamajack umenena vyema,kweli hali ya mabdiliko huku kwetu haina ari kivile,lakini vijana wasomi walioko huko mijini ndio wanapaswa kusaidia hayo mabadiliko,maana wazee wao huku wanataabika,
kwa mfani tulipimiwa viwanja vyetu ili tupate hat milik za kimila kwa g'harama ndogo,hat zipo ila kipata kama huna milion+ hupewi,na tumezuiliwa kuendeleza maeneo yetu.NAAMINI KWA PAMOJA TUTALETA MABADILIKO.
 
Wacha kujidhalilisha sio kila kitu kichosemwa na Pro-Chadema wenzako unakiunga mkono mungu amekupa akili zifanyie kazi wapi wanajeshi wamepaza sauti wakidai mabadiliko.

Naye Koplo Shaban Mrope (33), alisema Tanzania ina madini mengi, lakini viongozi wameingia mikataba ya miaka mingi na kusababisha hata mtoto atakayemzaa, asifaidike.

Alisema nchi ina maliasili nyingi na ilipaswa kutoa elimu na afya bure na kama Serikali imeshindwa kufuta mikataba hiyo na kuweka ya muda mfupi, ipishe Jeshi kwa muda lifute mikataba hiyo.

Huyo aliyetoa maoni hayo hapo kwenye RED anamaanisha nini?
 
Hakika uzalendo haujali nyazifa wala cheo,nimefurahishwa sana na mapendekezo ya wanajeshi wetu yaliyotolewa katika gazeti la mwananchi,hii inaonyesha uzalendo wa kwa nchi yao na namna wanavyo kelwa na dhuluma,uporaji ,ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma unaofanywa na viongozi wachahce wasio minifu.Ni hatari sana kuona wanajeshi wetu wanalalamika kwa ufisadi na unyonywaji.

Sitaki kuongelea kwa kina matokeo ya malalamiko ya wanajeshi hao nini, lakini kwa kifupi nasema inapelekea ukusefu wa ari ya kufanya kazi kwa wanajeshi wetu wote,POLISI,JWTZ,MAGEREZA,JKT,ZIMA MOTO hasa ngazi za chini ambao hasa ndiyo wanaolipwa ujira mdogo, huku wakishuhudia viongozi wanao walinda wakijilipa mishahara,malupulupu na kujilimbikizia mali kwa njia haramu.Mimi si shangai kusikia wanataka mafisadi wanyongwe na wengine wapigwe risasi hadharani. Hayo ni kwa wanajeshi kama lilivyo andikwa katika gazeti la mwanchi leo tarehe 28.09.2012.

Sasa tujiulize
;Je,
nani asiyejua umasikini uliokisili kwa wafanyakazi wa umma hasa ngazi za chini wanavyonyanyasika?Je, nani anapingana na mimi kuwa wakulima hawana uhakika wa bei wala soko la mazao yao ?Vipi kuhusu wafanya biashara na wafanyakazi wa sekta zisizo rasmi?

Bila shaka Watanzania wengi watakubaliana na mimi kuwa wanaofaidika na nchi hii ni kikundi cha watu wachache sana huku Watanzania wengi hawana hata uhakika wa kupata mahitaji muhimu ya binadamu.Hii inaonyesha kuwa wanaishi maisha ya kinyama kwa vile hawana uhakika wa kupata mahitaji muhimu ya binadamu.Je, tunategemea maendeleo gani au maisha yapi kwa Taifa la watu waligawanyika na kuishi maisha ya kukata tamaa na matokeo yake ni nini?

Aidha napendekeza tume ya kukusanya maoni ya katiba iendelee kutembelea na kukusanya maoni kwa wananchi huku ikizingatia kwamba wafanya kazi wengi hawapati muda wa kutosha kutoa maoni yao kulingana na ratiba zao kazi zinawaabana pia miiko na ukiritimba kutoka kwa viongozi wao wa ngazi za juu katika idara mbalimbali,hivyo ni bora wakatafuta namna nyingine ya kuwezesha kutoa maoni ya katiba , kama vile njia ya barua kwa sanduku la posta, mitandao n.k.Njia hizi ni muhimu kwa vile watu wengi hawapati muda wa kuhudhuria katika mikutano hiyo ya maoni ya katiba kutaka na sababu mbalimbali. Kama njia hizo zipo, basi waendelee kuzitangaza maana hazijulikani kwa watu walio wengi hasa vijijini ambako hata uhkika wakusikiliza redio au Tv haupo, mbaya zaidi ndiko wanakoishi Watanzania walio wengi.
.
Izingatiwe kuwa matumaini yaliyopo sasa ni katiba ijayo,hivyo tume inapaswa kujua kuwa inadhamana kubwa sana kwa Tanzania ya sasa na ijayo. Nahitimisha kwa kusema kuwa maoni yanayotolewa na wananchi yasipuuzwe na kuwekwa kapuni na baadaye tukajikuta tunongozwa kwa katiba yenye kulinda maslahi ya watu wachache, pia nashauri viongozi waliopo madarakani kuheshimu dhamana zao na kuithamini Tanzania na Watanzania ubinafsi kwao iwe mwiko kwao

 
Chadema wamekuwa watu wa kurukia matukio na kuyatolea matamko sasa huyu msemaji wa Chadema amekuwa msemaji wa Wanajeshi, kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa Wanajeshi walichosema wanataka mabadiliko ya kiutawala Chadema wachukue nchi.
SIO TU viongozi wabadhirifu wanyongwe, bali hata wanafamilia au ukoo waliotajilka kifisadi kupitia nafasi za wazazi wao au jamaa zao pia wanyongwe hadharani na mali zao kufilisiwa.
 


Bila shaka Watanzania wengi watakubaliana na mimi kuwa wanaofaidika na nchi hii ni kikundi cha watu wachache sana huku Watania walio wengi hatuna hata uhakika wa kula ukiachia mbali mahitaji muhimu ya binadamu.Hivyo maana nyingine tunaishi maisha ya kinyama kwa vile hautana uhakika wa kupata mahitaji muhimu ya binadamu, na hii haijalishi wakulima,wafanyakazi(serekalini na sekta binafsi), wafanya biashara na wabangaizaji.Je, tunategemea maendeleo gani au maisha yapi kwa Taifa la watu waligawanyika na kuishi maisha ya kukata tamaa?
Bila shaka matumaini yaliyopo sasa ni katiba ijayo,hivyo tume inapaswa kujua kuwa inadhamana kubwa sana kwa Tanzania ya sasa na ijayo.

Aidha napendekeza maoni yanayotolewa na wananchi yasipuuzwe na kuwekwa kapuni na baadaye tukajikuta tunongozwa kwa katiba yenye kulinda maslahi ya watu wachache.
Mkuu, hiyo red ingawa umeiandika kimakosa, lakini hivyo ndivyo tulivyo hasa Watania-ji. Tunafanya utani katika kila kitu. Inakuwaje nchi ya watu karibu milioni 45, tuseme milioni 30 wenye umri kati ya miaka 18-45, ambao wana uwezo wa kuamua hatima ya maisha yao, tunawaachia watu hawazidi laki moja kutuendesha kwata? Kama sio utani ni nini? Siku tukiacha utani tutaacha kuwa Wadanganyika au Watania kama wewe unavyosema.

Na hapo kwenye green, nisingependa kukuvunja moyo lakini ninakuhakikishia kuwa asilimia kubwa ya maoni ya wananchi yatawekwa kapuni kwani hii si mara ya kwanza kwa TZ kutoa maoni. Fuatilia tume zote zilizoundwa kwa nia ya kuchukua maoni ya wananchi, kipi kilitekelezwa?

Kwa mimi ambaye tayari nimeshapigwa mara kadhaa, chochote sasa kinachotoka kwa chama tawala ninakiona kama geresha tu ya kutakakuomba fedha kwa wafadhili na kuwafurahisha, lakini linapokuja suala la maslahi, huangaliwa la maslahi ya wachache/watawala kwanza. Kwa kukata tamaa kwangu, kama kweli wanajeshi wana nia ya kuweka hali sawa na kuturudisha kwenye msitari, nisingejitia kama wao wakachukua nchi kwa muda. INATOSHA! Hatuwezi kuendelea kuivumilia zaidi hali hii.

 
Jamaa kuna wakati anaposti bila kufikiria sijui ni kwanini.Yani yumo humu kikazi zaidi na kwahiyo siyo analytical wala hatumii critical thinking.Ni kama anasubiri tu kitu kikibandikwa ambacho ni kinyume na ufisadi basi anaasume ni ccm vs cdm.Ukimweleza anachukia.
have mercy on him .anakurupuka maana bosi wake akiona hajakoment anakatwa mshahara ,jana ananiambia nina multiple id kha namwambia sema kumbe kakurupuka shame on him ,hizi ni akili zakushikiwa yeye kila anayempinga eti ni chadema hii ni kazi yakula maandzi na chai ya rangi asubuhi asubuhi akili inashuka chini chakula kinapanda juu.
 
mbona mimi ninayo katiba mpya hayo maoni mnatoa ya nini???????????
 
Mkuu yote uliyoyasema ni ya kweli, hakika wewe ni SUTI YA WASIO NA SAUTI( A VOICE OF THE VOICELESS).Kwa hatua tuliyonayo sasa inatupasa tuelewe kuwa kila Mtanzania ananafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika nchi hii, cha msingi inatupasa tuchukue hatua sasa kila mtu kwa nafsi yake na kwa pamoja kama Watanzania wenye kuitakia mema nchi yao tupaze sauti na tuchukue hatua kusema UFISADI NA UNYONYAJI SASA BASI
 
Back
Top Bottom