WANAJESHI wameanza kufyatuka kupaza sauti kudai mabadiliko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WANAJESHI wameanza kufyatuka kupaza sauti kudai mabadiliko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Sep 25, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Naona kweli sasa tunatafuta mwafaka wa kitaifa. Kila mtu anashusha dukuduku lake. Kila mmoja atoe malalamiko yake, kero zake, manung'uniko yake, kila kitu kiwekwe wazi, watalaam wa sheria wakae watuwekee katika utaratibu wa kisheria ili tupate katiba mpya. Ndiyo. Hii ni fursa ya kujiumba upya kama taifa. Tutafute na kuweka mwafaka wa kitaifa. Kila mwananchi ashiriki/ashirikishwe;

  Unanaweza kuona hapa, wanajeshi nao sasa wamepaza sauti kali za mabadiliko ya kimfumo (na kiutawala?). Mbali ya Habari Leo walioiweka habari hii front paje, stori ya namna hii imeandikwa pia na Gazeti la Mwananchi la leo. Tunazidi kukomaa kwenye hii critical point tuliyofikia ya mapambano haya ya vuguvugu la kudai haki, kupigania uhuru wa kweli na mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala.

  Soma habari nzima:

  =============
  Wanajeshi: Wabadhirifu wapigwe risasi hadharani

  HOJA ya adhabu kwa viongozi wanaotumia vibaya madaraka, ni miongoni mwa zilizotawala kwa Watanzania wengi wanaotoa maoni kwa ajili ya Katiba mpya, huku baadhi ya wanajeshi wakipendekeza kiongozi wa uraia anyongwe, mwanajeshi apigwe risasi hadharani.

  Wanajeshi hao wametofautina na wananchi uraiani, ambao wengi wanapendekeza kiongozi anayefanya ubadhirifu, aondolewe mara moja, ashitakiwe kabla ya kustaafu au hata baada ya kustaafu na wengine wakapendekeza magereza maalumu ya viongozi.

  Akitoa maoni mbele ya wajumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Mabadiliko ya Katiba katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 411KJ Ruhuwiko, askari Mwita Nyansango (26), alisema adhabu hizo zitarudisha uwajibikaji kwa viongozi.

  Mbele ya viongozi wakuu wa kambi hiyo, ambao waliombwa waruhusu wapiganaji hao wawe huru wakati wa kujieleza, Nyansango alisema viongozi wa sasa hawafuati maadili, wanatumia vibaya rasilimali za wananchi kwa kuwa Katiba iliyopo, haijaweka wazi namna ya kuwawajibisha.

  "Katiba ijayo iweke wazi, kuwa kiongozi anayepewa dhamana ya kuongoza jamii, ikiwa ni waziri kafanya ubadhirifu, napendekeza anyongwe ili iwe fundisho, akija mwingine ajue kuna kitanzi, kwa sisi wanajeshi, apigwe risasi.

  "Tunasikia mambo ya Dowans na Richmond na tunachukia kusikia yanaendelea, halafu wahusika wanapewa nafasi ya kujitetea na wakifika mahakamani, wanapigwa faini," alisema Nyansango ambaye ana elimu ya darasa la saba.

  Nyansango pia alisema askari wa JWTZ, Polisi, Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), hawapaswi kuitwa wanajeshi kwa kuwa majeshi ya ulinzi ni ya nchi kavu, anga na majini.

  Hoja hiyo ilifafanuliwa na Luteni Hassan Tagalile, ambaye ana Shahada ya kwanza, aliyetaka Katiba ijayo ifafanue kati ya JWTZ, Polisi, Magereza na JKT, ni chombo kipi ni jeshi la ulinzi na kipi chombo cha usalama.

  Sajini Amedius Haule (51), ambaye ni Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Songea Mjini, alipendekeza askari wa ngazi za chini ya koplo, wawe na mwakilishi bungeni, kwa madai kuwa wao ndio wanaokutana na machungu ya Jeshi.

  Koplo Abeli Mtanzamo (29), alipendekeza mawaziri wasitokane na wabunge, kwa madai kuwa akiwa waziri anafanya ubadhirifu akijua atajiuzulu uwaziri na kubaki na ubunge.

  Koplo Elina Mwakitinga mwenye Diploma ya Ualimu, alipendekeza sheria za Jeshi zitambuliwe na Katiba na wanaotunga wajulikane hadhi zao kielimu na kuongeza kuwa ana wasiwasi sheria za Jeshi kwa sasa si shirikishi na zimerithiwa tangu ukoloni na kutengeneza watawala na watumwa jeshini.

  Naye Koplo Shaban Mrope (33), alisema Tanzania ina madini mengi, lakini viongozi wameingia mikataba ya miaka mingi na kusababisha hata mtoto atakayemzaa, asifaidike.

  Alisema nchi ina maliasili nyingi na ilipaswa kutoa elimu na afya bure na kama Serikali imeshindwa kufuta mikataba hiyo na kuweka ya muda mfupi, ipishe Jeshi kwa muda lifute mikataba hiyo.

  Hoja hizo zilizotolewa jeshini, zilitolewa pia katika mikutano uraiani, ambako adhabu zilizopendekezwa zilikuwa tofauti. Kuhusu adhabu kwa viongozi wabadhirifu, mkazi wa kata ya Ruhuwiko, Songea Mjini, Anthony Leonard (26), alitaka Rais asiteue Jaji ili apate uhuru wa kutoa hukumu.

  Alipendekeza kuwapo magereza ya viongozi na kuhoji; "kwa nini hakuna kiongozi aliye gerezani? Au wao hawaharibu?" Kijana huyo alisema kama rasimu ya Katiba mpya itakuja na kipengele ambacho taasisi ya urais inaruhusiwa kuteua Jaji, hatapiga kura na kama kutopiga kura ni kosa, yuko tayari kwenda jela.

  Mkazi mwingine wa kata hiyo, Pascal Ndunguru (64), aliyependekeza mbunge asiwe waziri, alimhoji kiongozi wa wajumbe hao wa Tume, Profesa Mwesiga Baregu aeleze kwa nini amekuja kusikiliza wananchi bila kufuatana na mbunge wao.

  "Profesa, wewe umefika hapa, yuko wapi mbunge wetu? Tunasikia ni waziri na hicho ndicho hatutaki kusikia, mbunge asiwe waziri atutumikie wananchi," alisisitiza.

  Simon Haule (80), mwenye elimu ya darasa la nne, alipendekeza Rais akitoka madarakani asipewe mshahara hadi kufa, bali alipwe pensheni kama mstaafu katika utumishi wa umma.

  =========

  CHANZO ni Gazeti la Habari Leo: Wanajeshi: Wabadhirifu wapigwe risasi hadharani
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,949
  Trophy Points: 280
  Wanajeshi wa jwtz wamependekeza mafisadi wanyongwe na hii ipitishwe kwenye katiba mpya.
  Maoni hayo waliyatoa jana mbele ya tume ya mabadiliko ya katiba mpya,iliyofika kuchukua maoni kwenye kambi ya 411 KJ mjini songea

  Source. Mwananchi tar 25/09/12 uk wa 12
   
 3. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pendekezo hilo liwe la kwanza kupita yote.
   
 4. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Chadema wamekuwa watu wa kurukia matukio na kuyatolea matamko sasa huyu msemaji wa Chadema amekuwa msemaji wa Wanajeshi, kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa Wanajeshi walichosema wanataka mabadiliko ya kiutawala Chadema wachukue nchi.
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Ulikuwa ni mjadala wa katiba mpya mkuu,umeisoma linki?
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu acha kukurupuka anaelezea kilichosemwa na wanajeshi sasa unataka uwasemee wewe gamba?
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Nimeisoma maoni yao yalikuwa dhidi ya mafisadi wanataka wanyongwe sio kuwa wanadai mabadiliko.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu jmushi1 achana nae huyu kalewa gahawa ndio muda wao wa vijiweni
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Ally Kanah

  Ally Kanah JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 1,433
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kalewa gahawa wee inaonekana uko VIROBA vya kutoshaaaaa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Ulisema hivi...
  Ndo maana nikakuuliza kama uliisoma linki.Sijui ume conclude vipi kwamba ni msemaji wa chama cha kisiasa?Ama umeassume?
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,616
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Jamaa kuna wakati anaposti bila kufikiria sijui ni kwanini.Yani yumo humu kikazi zaidi na kwahiyo siyo analytical wala hatumii critical thinking.Ni kama anasubiri tu kitu kikibandikwa ambacho ni kinyume na ufisadi basi anaasume ni ccm vs cdm.Ukimweleza anachukia.
   
 12. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,787
  Likes Received: 6,115
  Trophy Points: 280
  Hatari kweli kweli hii! Itabidi kuwa na siku za "mapumziko" kitaifa kwa ajili ya kuzika.

  Now, more than 80% ya wanachama wa CCM (5,000,000?) ni mafisadi. Suppose, 30% tu ya hao 80% watatiwa hatiani na hizo adhabu kutekelezwa ndani ya wiki moja baada ya hukumu. Bwa ha ha ha ha ha!

  Hii maana yake, ndani ya wiki moja tutapiga risasi na kuzika mafisadi 30% x 80% x 5,000,000 = 1,200,000. Nashauri wazikwe kwenye makaburi ya jumla au wachomwe moto watatumalizia tu ardhi na muda hawa.
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wacha kujidhalilisha sio kila kitu kichosemwa na Pro-Chadema wenzako unakiunga mkono mungu amekupa akili zifanyie kazi wapi wanajeshi wamepaza sauti wakidai mabadiliko.
   
 14. by default

  by default JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  tumia ubongo kufikiri usitumie masaburi mkuu
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Nadhani humjui Tumaini Makene, ni nani Chadema, kwa kukusaidia ni msemaji wa Chadema kachukuwa nafasi ya Regia Mtema (R.I.P) ndio maana nimejibu hivyo wewe bila kujua umerukia kumjibia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Wanajeshi wametoa maoni yao kutaka mabadiliko ya kimfumo na kiutawala. Lakini Ritz kwa akili yake ya kuku akishasikia neno mabadiliko anajua ni Chadema kuibadili ccm katika utawala wa nchi. Na kwakuwa mkate wake anaupatia ofisi za lumumba kwahiyo anakurupuka tu kuandika bila kutafakari kutokana na kihoro cha watoto kwenda msalani!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #17
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Labda wanajeshi watamnyonga mtu kabla hata katiba haijabadilishwa. You never know what can happen wanajeshi wakiwa excited.
   
 18. we gule

  we gule Senior Member

  #18
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kuwanyonga mafisadi sio Mabadiliko?
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Tumaini Makene, naona umeifanyia edit habari yako baada ya kuona umechemka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Luno G

  Luno G JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 22, 2012
  Messages: 1,883
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  sasa hayo sio mabadiriko?
   
Loading...