Wanajeshi wakisaidia kumvusha mtoto kuepuka wataliban

dem boy

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
5,847
14,509
Mtoto mdogo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja ameonekana siku akivushwa na wanajeshi wa Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kabul nchini Afghanistan leo.

Tukio hilo limetokea wakati ambapo wazazi pamoja na wakazi nchini humo wakijaribu kunusuru maisha ya watoto wao kwa kuwakabidhi mikononi mwa wanajeshi wa kimarekani huku wakiamini itakuwa ni sehemu salama kwa watoto hao kuwa watalindwa dhidi ya ghasia za wanamgambo wa Taliban.
1629799239621.png
 
Propaganda za wa marekani. Na binadamu tulivyo na akili ya ku sahau tumeshasahau zamani tu.

Kabla ya Taliban kuchukua Nchi miezi michache tu iliopita kuna Askari amefungwa huko Marekani kwa kutoa Siri za jeshi, Marekani walikuwa wakituma drones kuua Raia wa Afghanistan kimakusudi (sio wapiganaji), jamaa kutokana na guilt aliosikia akaiba zile document na kuwapa waandishi wa habari.

Toka vita Vya wa marekani na washirika wake vianze Middle East na Afghanistan/Pakistan watu Takriban milioni 38 wamekimbia Nchi zao na watu kama laki 8 wamefariki na vita wengi wakiwa wananchi wa kawaida, Marekani na washirika wake wamekuwa wakipiga mabomu Tena makubwa Makubwa kwenye makazi ya watu na kuvunja kabisa majengo.

Hio ni idadi kubwa kushinda vita vya kwanza vya Dunia, na ni ya pili nyuma Ya vita kuu ya pili ya Dunia, yote haya tunayasahau leo propaganda za hapa na pale eti mtu anamuona US ndo mtu mzuri.
 
Hao marekani ni watu wabaya,na ni magaidi.

Na hao hao ndo wanatoa misaada,aisee
Ovyo kabisa hao Taliban, ni mashetani flani tu, hata wanyama wa porini wanawazidi kwa utu. Maanake hakuna kiumbe chochote chini ya jua ambacho hakijui thamani ya mtoto na kwamba watoto ni wa kulindwa kwa gharama yeyote ile.
14079513_fbimg16295557562617293_jpegceab63cbe92a7914ef17352325124f45.jpeg
15504919_web1_kabul.babies-1.jpg
Hawa hapa ni wanajeshi wa US Marine Corps wakiwa kazini, ndani ya uwanja wa ndege wa Hamid Karzai, Kabul. Licha ya hatari silaha zao zipo chini, ili waweze kuwashughulikia hawa watoto wa kiafghani ambao walikabidhiwa na wazazi wao.
 
Ovyo kabisa hao Taliban, ni mashetani flani tu, hata wanyama wa porini wanawazidi kwa utu. Maanake hakuna kiumbe chochote chini ya jua ambacho hakijui thamani ya mtoto na kwamba watoto ni wa kulindwa kwa gharama yeyote ile.
14079513_fbimg16295557562617293_jpegceab63cbe92a7914ef17352325124f45.jpeg
15504919_web1_kabul.babies-1.jpg
Hawa hapa ni wanajeshi wa US Marine Corps wakiwa kazini ndani ya uwanja wa ndege wa Hamid Karzai, Kabul. Licha ya hatari silaha zao zipo chini, ili wawaze kuwashughulikia hawa watoto wa kiafghani ambao wamekabidhiwa na wazazi wao.
Huyo ni mwanajeshi wa marekani na sio jeshi la marekani, Jeshi la marekani linaua Raia kila siku lakini haimaaanishi hakuna wanajeshi wenye Roho nzuri.

Tukumbushane ilikuwa je Tena wakaenda kuvamia Afghanistan?
 
Mtoto mdogo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja ameonekana siku akivushwa na wanajeshi wa Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kabul nchini Afghanistan leo.

Tukio hilo limetokea wakati ambapo wazazi pamoja na wakazi nchini humo wakijaribu kunusuru maisha ya watoto wao kwa kuwakabidhi mikononi mwa wanajeshi wa kimarekani huku wakiamini itakuwa ni sehemu salama kwa watoto hao kuwa watalindwa dhidi ya ghasia za wanamgambo wa Taliban.
View attachment 1906105

Hii kitu haowaumizi roho na akili hao watalaban? Kwanini wasijenge Taifa lenye kufuata masharti ya kidini, lakini salama na huru kwa kila mwananchi?
Lipo tatizo kubwa sana kwa hawa jamaa na jinsi wanavyoelewa dini
 
Huyo ni mwanajeshi wa marekani na sio jeshi la marekani, Jeshi la marekani linaua Raia kila siku lakini haimaaanishi hakuna wanajeshi wenye Roho nzuri.

Tukumbushane ilikuwa je Tena wakaenda kuvamia Afghanistan?
Walitoroka waafghani wangapi wamarekani walipovamia nchi yao? Wapiganaji wa Taliban wapo nje ya uwanja wa ndege, wakipiga risasi hewani. Bila kuzingatia kwamba kuna watoto ndani ya umati wanaojaribu kuutawanya. Hao watoto watakumbuka nini kuhusu watawala wapya wa nchi yao?
r
b8258d3d-1626-4bca-bcd8-11541a6eec4a-AP_US_Afghanistan.JPG
 
Back
Top Bottom