Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 55,881
- 29,255
Wanajeshi wadaiwa kutembeza kipigo kwa raia, 10 taabani
Na Mwandishi Wetu,Tanga
BAADHI ya askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Maramba mkoani Tanga wanadaiwa kutembeza kipigo kwa wakazi wa eneo hilo ambapo watu 10 wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga, Bombo.
Wanajeshi hao zaidi ya 20 wakiwa wamevalia sare za kazi, wanadaiwa kuwavamia wananchi hao wa Mramba na kuwapiga kwa kutumia marungu na magongo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Bw.Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 25 mwaka huu saa 5 usiku huko Maramba wilayani Mkinga.
Kamanda Sirro, alisema wanajeshi hao pia wanadaiwa kuharibu mali za wananchi hao ikiwa ni pamoja na kuvunja vioo vya magari mawili, moja ni Toyota Hiace lenye namba za usajili T 130AHZ na lori lenye namba namba T871ASM .
Kamanda Sirro alisema chanzo cha vurugu hizo ni ugomvi uliotokea Agosti 24 mwaka huu ya saa 7 usiku eneo la Maramba 'B' kwenye ukumbi wa disko ambapo askari wa JKT aliyefahamika kwa jina la Bw. Godfrey Mwita (23)alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe kichwani na mfanyabiashara Bw. Peter Gabriel (18), mkazi wa Maramba.
Alisema chimbuko la ugomvi huo ni mwanamke waliyemkuta hapo ukumbi. Baada ya kutokea vurugu hizo, Bw. Peter alikamatwa, kufungwa pingu na kupelekwa kwa mlinzi wa amani wa eneo hilo ambapo baada ya muda mfupi aliachiwa huru.
Ilildaiwa kuwa kitendo cha kuachiwa mfanyabiashara huyo kiliibua hasira kwa askari hao na kuamua kulipiza kisasi kwa wakazi wote wa eneo hilo.
Kamanda Sirro aliwataja waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni Bw. Ali Husein (50), Bw. Dustan Maghembe (37), Bi.Tabu Mustafa (56), Bw. Juma Athman (38) na Bw.Wales Mbwana (59).
Wengine Bw. Baltazar Christopher (45), Bi. Mwanaisha Adam (28), Bi. Saumu Dua (19),Bw. Charles Mbaga(26) Bw. Musa Mohamed (21).
Kamanda Sirro alisema hadi sasa Polisi hawajafanikiwa kumkamata mtuhumiwa yeyote kuhusiana na tukio hilo na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasi (FFU) wamepelekwa eneo hilo kudhibiti vurugu hizo.