Wanajeshi wa Uturuki wakamatwa wakihusishwa na Gulen

PaulElias

Member
Dec 20, 2016
23
52
Wanajeshi 34 wa Uturuki walikamatwa katika mji mkuu Ankara kwa madai ya kuwa na mahusiano na imamu wa Kiislamu Fethullah Gulen, ambae serikali inamlaumu kwa jaribio la mapinduzi mwezi Julai tarehe 26.

Kati ya wanajeshi hao ni kutoka kikosi cha polisi, shirika la habari la Anadolu limeripoti, wakati wengine ni kutoka jeshi la anga, jeshi la majini na wanajeshi wengine. Kukamatwa kwa wanajeshi hao kunafuatia msako katika majimbo 22 nchini humo.

Gulen, imam mzaliwa wa Uturuki na mshirika wa zamani wa Rais Recep Tayyip Erdogan ambaye anaishi Marekani, amekana kwamba anahusika na jaribio hilo la mapinduzi. Kwa mujibu wa data rasmi, zaidi ya wanajeshi 40,000 wamekamtwa.
 
Back
Top Bottom