Wanajeshi wa tanzania wako juu ya sheria???!!!

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Matukio ya wanajeshi kupiga raia yamekua yakiongezeka kadri siku zinavyosonga mbele bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi yao. Hapo nyuma waliwahi kupiga wafanyakazi wa dawasco walipokwenda kutimiza majukumu yao ya kikazi katika kambi moja ya jeshi. Jana mlimani tv iliripoti jinsi wanajeshi wa kambi ya kunduchi walivyopiga na kuwajeruhi raia kwa madai ya kuvamia eneo la jeshi. Diwani wa kunduchi alifika kambini hapo kwa lengo la kuongea na mkuu wa kambi ili kuwaokoa raia waliokuwa wamekamatwa lakini aliambulia maneno ya kashfa na kuambiwa asipeleke siasa jeshini na kuambiwa yeye ndiye anayewatuma. Baadaye alifanikiwa kuongea na mkuu huyo. Licha ya mlimani tv jana kuonesha picha za raia waliopigwa na kujeruhiwa vibaya, leo msemaji mmoja wa jeshi amenukuliwa katika taarifa ya habari ya jioni ya bbc idhaa ya kiswahili akisema hakukuwa na tukio lolote la kupigwa raia. Je hii ni sawa???
 
mkuu si wanajeshi tu walioko juu ya sheria...mkuu mwenyewe-gamba kuu pale ikulu yupo juu ya sheria, Rz1 yupo juu ya sheria, Tendwa, Rostam, EL, Karamagi, Chenge, Hosea hadi mgambo nao wamo...orodha ni ndefu...walio juu ya sheria. Kiufupi system nyingi sasa hivi zipo corrupted, zinanuka!! tangu juu hadi chini kabisa. Sheria zinawabana wakulima ni vichaa tu sasa hivi. Ndio maana Dk Slaa anasema Nchi haitawaliki tena!!
 
Kwa kifupi haya mambo ya kijinga kijinga wanayofanyiwa wananchi wa Tanzania wa kulaumiwa ni wananchi wenyewe. Wamezidi uduanzi kwani wangekuwa wakali ujinga huu ungeshaisha zamani. Hii style ya kuishi kama nyumbu wa mbuga za Manyara, unamwona mwenzako/wenzako wanafanyiwa unyama na wewe/sisi tunakaa kimya ni uduanzi.... Mpaka tutakapochangamka mambo hayatabadilika.. Tuache unyumbu..
 
ndugu ungetafasiri sentez zako naona zimejaa ghadhabu na hasira...lol
 
Back
Top Bottom