Wanajeshi wa tanzania wako juu ya sheria???!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi wa tanzania wako juu ya sheria???!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by samirnasri, May 10, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Matukio ya wanajeshi kupiga raia yamekua yakiongezeka kadri siku zinavyosonga mbele bila hatua zozote za kisheria kuchukuliwa dhidi yao. Hapo nyuma waliwahi kupiga wafanyakazi wa dawasco walipokwenda kutimiza majukumu yao ya kikazi katika kambi moja ya jeshi. Jana mlimani tv iliripoti jinsi wanajeshi wa kambi ya kunduchi walivyopiga na kuwajeruhi raia kwa madai ya kuvamia eneo la jeshi. Diwani wa kunduchi alifika kambini hapo kwa lengo la kuongea na mkuu wa kambi ili kuwaokoa raia waliokuwa wamekamatwa lakini aliambulia maneno ya kashfa na kuambiwa asipeleke siasa jeshini na kuambiwa yeye ndiye anayewatuma. Baadaye alifanikiwa kuongea na mkuu huyo. Licha ya mlimani tv jana kuonesha picha za raia waliopigwa na kujeruhiwa vibaya, leo msemaji mmoja wa jeshi amenukuliwa katika taarifa ya habari ya jioni ya bbc idhaa ya kiswahili akisema hakukuwa na tukio lolote la kupigwa raia. Je hii ni sawa???
   
Loading...