Wanajeshi wa Rwanda wawaua wanamgambo wa Kijihadi Msumbiji

Vikosi vya Rwanda vilivyotumwa kusaidia kukabiliana na waasi vimewauwa wanamgambo wa kijihadi wasiopungua 30, maafisa wa usalama nchini Msumbiji wanasema.

Maafisa hao wanasema wanajeshi walikuwa wakiifanya oparesheni ya usalama katika msitu wa karibu na mji wa bandari wa Palma walipokutana na wanamgambo hao. Karibu wanajeshi 1,000 wa Rwanda walipelekwa nchini Msumbiji mapema mwezi huu.

Jumuia ya maendeleo ya mataifa ya kusini mwa Afrika (SADC) imepeleka wanajeshi wake nchini humo na vikosi vya Ureno vinasaidia kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji. Karibu watu 800,000 wamefurushwa makwao kutokana na ghasia hizo zilizodumu miaka minne.

Maelfu ya watu wameuawa na wengine wengi kukatwa vichwa.
Baada ya hapo Rwanda itapeleka wanajeshi wake Nigeria kuwafurusha Boko Haram..😀😀
 
Kuweni wapole, al-shabab, ninavyowajua, watakuwa vichwa viko busy to plan retaliation. Subiri huo muziki unaokuja ndani ya Rwanda
Hakuna Jambo baya Kama kufanya PR ya mauaji...Mimi najua TZ imefanya makubwa huko lakini hutasikia majisifu....
 
Kuweni wapole, al-shabab, ninavyowajua, watakuwa vichwa viko busy to plan retaliation. Subiri huo muziki unaokuja ndani ya Rwanda

Tumefikia hatua ya kuwaogopa magaidi kisa watakuja kutushambulia hahahah,ni sawa na kumuacha mkeo agongwe na njemba hapo mtaani kisa jamaa ni libaunsa ukilizingua na wewe litakutembezea pumbuhhh.
 
Back
Top Bottom