Wanajeshi wa Msumbiji wauawa na Wanamgambo

Wakiuawa wa Tanzania hutokaa upate habari!

Hazisaidii kujenga zaidi ya kutia hofu wananchi.. Nashangaa hata hao Msumbiji wanaruhusu vipi taarifa kama hizo kuvuja. Ilitakiwa wazike kisha warudi kupambana kimya kimya. Suala ni kukamilisha misheni ndio kubwa askari kufa vitani ni ushujaa.

Uliona Kibiti, kuna magaidi ulisikia wamekufa wangapi?
 
Kwanini raia washirikiane na waasi? Unahitaji kujua jibu la swali hilo na kuanza kuishuhulikia hio sababu kabla haijawa too late.
Sababu zipo nyingi, pengine hofu ya kuwataja wanajua watachinjwa, na pengine ni kukataa tamaa ya maisha na kudhani kuna njia ya mkato kufikia mafanikio hasa vijana wa leo. Sababu ni nyingi mno.
 
Alichomaanisha kiongozi ni kwamba

Hao wanamgambo ni kama hawana sare na wanakaa na raia hivyo kupigana nao ni vigumu kwa sababu hujui Raia nani na mwanamgambo nani
Wanavaa sare za kijeshi labda uniambie saa wanavizia wanaenda na nguo za kiraia mkuu
 
Wanamgambo wanavaa nguo kama raia, wanaficha silaha majumbani mwa raia au nyumba za ibada za raia.
Sindikiza na picha kabisa
images%20(3).jpg
images%20(4).jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajeshi 25 wa vikosi vya usalama Msumbiji wameuawa huku wengine 15 wakijeruhiwa baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa Kiislamu katika kijiji cha Matambalale eneo la Muidumbe.

Kundi la maafisa wa kijeshi lilikuwa linashika doria eneo hilo wakati wa tukio Jumapili, kulingana na vyombo vya habari vya eneo.
Katika moja ya uvamizi, kanali na meja wamefariki dunia, vyanzo vimenukuu vyombo vya habari vya eneo.

Waathirika walikuwa sehemu ya kundi lililotumwa kuimarisha usalama baada mashambulizi ya wiki iliyopita ambapo nyumba zilichomwa moto na wakaazi kuuawa.View attachment 1640754

Bado jeshi halijathibitisha au kukanusha taarifa hizo.
View attachment 1640754View attachment 1640755
Mashambulizi ya miaka mitatu yamesababisha mauaji ya zaidi ya 2,000 na kusababisha wengine 500,000 kutoroka makazi yao katika eneo la Cabo Delgado, kulingana na takwimu rasmi.
Hao mgambo sio wale waliopelekwa Pemba?
 
Hakuna jeshi hapo.
Inabidi wakasaidiwe. Badala ya kulinda kijiji wanaenda kulala sehemu 1.
 
Umewahi kujiuliza kwanini hao Boko Haram hawana nguvu sana maeneo ya kusini mwa Nigeria ambako hakuna watu wengi wa imani yao?
Au kwanini kusini kwa Msumbiji hawana nguvu?
msumbiji walipo jimbo la cabo delgado kuna madini ya ruby, gesi na mafuta, nigeria boko haram wapo niger delta kwenye mafuta, sudan kusini kuna vita sababu ya visima vya mafuta, hao waasi wanakaa sehemu kwenye utajiri wa madini, gesi na mafuta! waasi wa congo wako eneo lenye utajiri wa madini!
 
Kibiti na Somalia kuna nini?
Au Kenya kule kuna nini?
 
Hazisaidii kujenga zaidi ya kutia hofu wananchi.. Nashangaa hata hao Msumbiji wanaruhusu vipi taarifa kama hizo kuvuja. Ilitakiwa wazike kisha warudi kupambana kimya kimya. Suala ni kukamilisha misheni ndio kubwa askari kufa vitani ni ushujaa.

Uliona Kibiti, kuna magaidi ulisikia wamekufa wangapi?
Kupata habari za ni nini kinaendelea katika nchi yako ni haki ya kikatiba wala siyo suala la mtu fulani kuamua kuwa upate habari hii kwa sababu haitii hofu na usipate habari hii kwa sababu inatia hofu.Ni haki ya mwananchi kujua kinachoendelea katika nchi yake.Nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria na wala siyo kwa mujibu wa mawazo na akili za mtu mmoja,hakuna sheria inayosema kuwa mwananchi anatakiwa kupewa tu habari ambazo hazitii hofu.
 
Wakuu nilikuwa nauliza wale watoto wa kike waliotekwa na Boko Haram kwenye shule ya boarding walirudi wote??????? Lile swala liliisha vipi?????????

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Wale siku walipotoka walikuwa wazee na wengi wao walikuwa washajukuu,walipelekwa kanisani kusherehekea.Hillary Clinton na kampeni zake akanyamaza.Wazee wale wala hawakuwapeleka wakuu wa majeshi huko walikoshikiliwa ili kuwakamata wahalifu.Haiwezekani kundi lote lile likashindwa kutoa maelezo ya maeneo walilokuwa wakiishi ili jeshi lifuatilie.
 
Wakuu nilikuwa nauliza wale watoto wa kike waliotekwa na Boko Haram kwenye shule ya boarding walirudi wote??????? Lile swala liliisha vipi?????????

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Walitekwa watoto 300 mpaka Sasa wameshaachiliwa watoto 70+ ila Kuna taraifa kutoka kwa hao walioachiliwa kuwa wenzao huko porini baadhi hawataki kurudi makwao.. Zingine ni porojo
 
Somalia ni vita vya koo, huko kibiti wale walikuwa vibaka tu
Eti unasema Kibiti walikuwa nani?
We jamaa naona una ushabiki au una upande flani kiitikadi kwenye hili suala.

Koo za Somalia zinavuka hadi Kenya kuteka na kuuwa makumi ya watu kwenye hotel, vituo vya polisi na maeneo ya kibiashara au vyuo vikuu?

Koo hizo hizo zinaenda kulipua pubs huko Uganda!!

Kibiti walidhibitiwa mapema, masalio yao ndiyo hao wamekimbilia Msumbiji wanasumbua watu.
Tuwape sifa zao vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, bila wao sasa hivi tungekuwa tumepoteza watu wengi sana.
 
waliachiwa wote, sema wengi wao walikataa kurudi walikuwa wameshaolewa na kuanzisha familia, kwa hiari yao wakakataa kuacha familia zao.
Hakuna maneno 'kwa hiyari yao'
Walisha haribiwa kisaikolojia na kuwa radicalized tayari.

Ni kama leo nimteke mtoto bikra na hatumii pombe au madawa ya kulevya. Kisha nimfundishe kutumia ulevi huo pamoja na ngono, akishakuwa kaathirika na uraibu(addiction) nimuachie..., Lazima atarudi tu kwangu kuendelea kupata hivyo vitu vilivyo mharibu.
 
Hiyo ndio point walishajazwa mambo ya ajabu
 
Back
Top Bottom