Wanajeshi wa Mali wauawa siku chache baada ya Ufaransa kutangaza kuondoka

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,037
20,337
Jeshi nchini Mali limesema wanajeshi wake wanane wameuawa na watano hawajulikani walipo baada ya kushambuliwa na waasi katika eneo la kaskazini-mashariki la Archam.

Mapigano hayo yanakuja siku chache baada ya Ufaransa na washirika wake kusema kuwa wanaondoa vikosi vyao kutoka Mali.

Taarifa ya jeshi ilisema kuwa katika kukabiliana na shambulio hili la hivi punde zaidi, jeshi la anga la Mali liliwaua wanamgambo 57.

Ilisema kuwa wanajeshi hao walikuwa wakitafuta maficho ya waasi walipoviziwa na "watu wasiojulikana wenye silaha".

Kumekuwa na wasi wasi wa kieneo na kimataifa kuhusu usalama wa Mali kufuatia kutimuliwa kwa wanajeshi wa Ufaransa, pamoja na uthibiti wa mamluki wa Urusi katika eneo hilo.

Wiki hii pekee, wenyeji waliliambia shirika la habari la AFP kwamba raia 40 wameuawa katika eneo moja la Archam ambako makundi hasimu ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Islamic State, yanaendesha harakati zake.

Mali imekuwa ikikabiliana na machafuko ya wanajihadi kwa miaka mingi, na kusababisha maandamano makubwa mwaka 2020 dhidi ya Rais wa wakati huo Ibrahim Boubacar Keïta ambaye aliondolewa madarakani na viongozi wa mapinduzi wakiahidi kurejesha usalama.

Tangu wakati huo viongozi wapya wa kijeshi wa nchi hiyo wamekuwa na msururu wa kutoelewana na mkoloni wa zamani , Ufaransa, hali iliyowafanya kukataa makubaliano ya kufanya uchaguzi wa kidemokrasia mwaka huu na kumfukuza balozi wa Ufaransa alipopinga.

Ilifikia kilele kwa Mali kuamuru Ufaransa kuondoa wanajeshi wake wote, baada ya karibu miaka 10 kupambana na tishio la wanajihadi.

Wakiungwa mkono na wanajeshi kutoka mataifa mengine ya Magharibi, ujumbe wa pamoja wa Mali - unaoitwa Kikosi Kazi cha Takuba - sasa utahamia umbali mfupi kuvuka mpaka hadi Niger, ukisalia karibu na kambi yao ya sasa.

Rais wa Niger alisema siku ya Ijumaa kwamba mipaka ya nchi hiyo huenda ikawa hatarini zaidi kwa shughuli za wanamgambo wa kijihadi kufuatia kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa na washirika wao kutoka Mali.

Mapema wiki hii yeye na viongozi wengine wa Afrika Magharibi walikutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kabla ya tangazo la kuondolewa kwa vikosi kutoka Mali, ambapo walikubaliana kuwa wanajeshi hao watahamia nchi za eneo hilo.
 
Kwani hayo majeshi ya kukodi kutoka RUSSIA, yameshindwa kuwasaidia!!Afrika bana yaani majeshi ya nchi kama UFARANSA, unayaona hayana maana unaenda kukodi majeshi toka makampuni binafsi!!!
 
Kwani hayo majeshi ya kukodi kutoka RUSSIA, yameshindwa kuwasaidia!!Afrika bana yaani majeshi ya nchi kama UFARANSA, unayaona hayana maana unaenda kukodi majeshi toka makampuni binafsi!!!
Ufaransa ilikuwa hailindi amani Mali; wale walikuwa wanalinda maslahi yao waliojitangazia kuyapoka tangu enzi wa ukoloni. Are you hearing? Nenda sehemu kama Maidugri utapata jibu.
 
Afrika bana, yaani tunashindwa kujitawala na kujilinda alafu tunakodi majeshi cha kuhuzunisha wale IS nao wanatumika kuharibu usalama na umoja wa nchi kadhaa afrika bila sababu.

Yaani utawasikia 'TUMEHUSIKA' wanajimambwafy without sense!.
 
Kuna mtu juzi katoka ufaransa. Ufaransa ni kupe mwenye hila kuliko kupe wengine wengi.
 
Afrika bana, yaani tunashindwa kujitawala na kujilinda alafu tunakodi majeshi cha kuhuzunisha wale IS nao wanatumika kuharibu usalama na umoja wa nchi kadhaa afrika bila sababu.

Yaani utawasikia 'TUMEHUSIKA' wanajimambwafy without sense!.
Ndio Afrika yetu hii
 
Hili kundi IS lina2miwa/fadhiliwa na nani?
 
Wakati wenzetu wana hangaika kuitafuta amani, huku kwetu watu wachache wanaichezea tu kwa manufaa yao!

Yaani wanalazimisha watu wawe MAGAIDI eti! 🤔
 
Wakati wenzetu wana hangaika kuitafuta amani, huku kwetu watu wachache wanaichezea tu kwa manufaa yao!

Yaani wanalazimisha watu wawe MAGAIDI eti! 🤔
Siku ikipotea amani ndio tutaanza kuitafuta kwa Tochi na siku tunao waita Magaidi wakiwa tutaanza kujitafuta.
 
Siku ikipotea amani ndio tutaanza kuitafuta kwa Tochi na siku tunao waita Magaidi wakiwa tutaanza kujitafuta.
Mistakes nyingi wanazofanya Waafrika ni kudhani kwamba kuna watu somewhere wanajali sana maslahi yao na kwamba wanaweza kujitolea mali na damu ili kuwapatia usalama! Pathetic!

Afrikkkkkka should and must be by Africans!
 
Back
Top Bottom