Mwanajeshi alieasi Korea abainika kushambuliwa na Minyoo

panamo

Member
Nov 25, 2016
64
58


Maisha ndani ya jeshi la korea kaskazini bado ni ya kutatanisha, na vikosi vya jeshi la korea kaskazini vimeendelea kupata shida mbali mbali ikiwemo njaa, parasite (wadudu washambuliao mwili wa binadamu) pamoja na magonjwa, hali inayowaondolea kabisa morali ya kufanya kazi wakiwa kama wanajeshi wa jeshi la Korea kaskazini.

Kim Eun-jung mbae alikuwa ni junior officer wa jeshi la korea kaskazini akitumikia jeshi kwa muda wa miaka 10, kabla ya kukimbilia Korea ya kusini kupitia China aliiambia gazeti la The Times kuwa, maisha ndani ya PLA yalikuwa ni mabaya na yasiyo ya kufurahisha.

Ms Kim alisema, mabuti waliyopewa vikosi vya jeshi la Korea kaskazini yalikuwa yamejaa matundu, hali ambayo iliwaweka hatarini na wadudu mbalimbali. “Kila mmoja alikuwa anaumwa ndani ya jeshi, muda wote,” alisema “Wamechukua kile ambacho kingekuwa miaka kumi bora kwa uzuri ktk maisha yangu"

Chakula ni kidogo sana na ni kile kisichokuwa na ubora kabisa. Na pia aliongezea kuwa walilazimishwa kufanya kazi mara mbili kwa mwaka bila ya kupumzika.
Mis Kim aliiambia Gazeti la The Times kuwa mbolea ilikuwa ni kiasi kidogo sana, kwahiyo vikosi vilichukua kinyesi cha binadamu jambo ambalo liliweza hatarisha zaidi usambaaji wa wadudu washambuliao mwili wa binadamu.

Wakati hayo yakijili, mwanajeshi wa jeshi la Korea kaskazini Mr Oh Chung-Sung ambaye alipigwa risasi tano na wanajeshi wenzake mpakani mwa Korea kaskazini na kusini akiwa anatambaa kwa kujificha, bado anaendelea kupatiwa matibabu nchini Korea kusini ambako wapasuaji mahili waliweza kumhudumia mapema baada ya tukio hilo, aidha Daktari wa upasuaji Dr Lee Cook-Jong aliiambia CNN kuwa madaktari wamepigana kumpatia matibabu, na walimkuta mwanajeshi huyo kijana wa miaka 24 akiwa amejawa na Minyoo, ambayo mingine ilifikia urefu wa sentimita 27.

Dr Lee alisema “Uchunguzi umeenda sawa lakini minyoo ni weupe, wanene, warefu na pia ni wagumu sana, na minyoo hawa walitoka katika utumbo wa Mwanajeshi huyo aliyekimbia Korea kaskazini”

Mwanajeshi huyo bado anasumbuliwa na ugonjwa wa TB na Hepatitis B, Pia ataendelea kuwa na makovu maishani mwake pamoja na Msongo wa mawazo ikiwemo Utumbo wake kupasuka sehemu mbalimbali kutokana na risasi tano alizoweza kupigwa mpakani mwa eneo lenye ulinzi mkali la Joint Security Area "JSA" [Demilitariled Zone] ambapo ni eneo pekee wanajeshi wa pande zote mbili yaani Korea Kaskazini na Korea Kusini huwa wanaonana ana kwa ana.
 
Hawa ndiyo wanaotaka mapambano na mzee yule wa USA!

Hatari sana kama kweli.
Au ni trick ya kumvimbisha kichwa Trump?
 
Hawa ndiyo wanaotaka mapambano na mzee yule wa USA!

Hatari sana kama kweli.
Au ni trick ya kumvimbisha kichwa Trump?
jambo baya ni kuwa Korea kaskazini inajifuta kwenye internet, taarifa zake nyingi ni zakitatanishi.
 
Hizo ni kasumba za kimagharibi. Kuna watu ambao kazi yao kubwa ni kukubali tu kila kinachosemwa na Wamagharibi.

Kwa kifupi, huu ni uzushi.
 
USA kwa propaganda ndio mwenyewe.
Vita ikianza anachukua homeless na kuwapa mafunzo wiki tatu tu na kuwapeleka front line
Iraq ni moja wapo walikuwa kibao hasa blacks
 
Hiki ndio kitawaangusha mbele ya fitina za wamarekani, uzalendo hauna nguvu mbele ya tumbo na mateso, dhiki ni mbaya sana.
 
Back
Top Bottom