Wanajeshi wa JWTZ wako juu ya sheria za nchi?

Mkulima wa Kuku

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,270
534
Kuna tabia naiona siku hizi kwenye maeneo yenye msongamano wa magari utakuta wakija wanajeshi wanapandia kwenye maeneo ambayo wewe ukijaribu tu umekwisha lakini wao wanavunja kwa makusudi sheria. Ina maana wao ndiyo wenye haraka pekee au wako juu ya sheria za nchi na viongozi wanawaogopa? Polisi najua kwa hakika wanawaogopa 100%. Nauliza tu.
 
ndiyo umejua leo kwa taarifa yako hii ni dunia nzima ukitaka unafuu kajiunge nao salute kwenu magwanda
 
Wanajeshi wetu wanajiona wao ndio wao.

Sema kuna Mwanajeshi mmoja alitokea kunipenda sana akawa ananipeleka kambini kwao kufanya mazoezi
 
swali gumu sana hili ngoja waje wenyewe...ila kwa uelewa wangu majukumu yao ni hayo, ya polisi ni ulinzi wa raia na mali zao, majeshi mengine pia yana majukumu yao kama zimamoto, na magereza.
Ugumu wake upo wapi?

Nenda kwenye Website yao ukaone majukumu ya JWTZ na wakati huo huo usisahau msaada alio omba IGP Mangu kwa Jeshi hilo.
 
Kuna tabia naiona siku hizi kwenye maeneo yenye msongamano wa magari utakuta wakija wanajeshi wanapandia kwenye maeneo ambayo wewe ukijaribu tu umekwisha lakini wao wanavunja kwa makusudi sheria. Ina maana wao ndiyo wenye haraka pekee au wako juu ya sheria za nchi na viongozi wanawaogopa? Polisi najua kwa hakika wanawaogopa 100%. Nauliza tu.

Ningekushauri Mkuu Liandike Mahala Hata Katika Karatasi Hiki Ulichokiandika Halafu Wavizie Hao Hao WANAJESHI Wakiwa Humo Njiani Halafu Wape Hili Swali Lako Naamini Watakupa JIBU Zuri Tu Na LILILOTUKUKA Kwani Ni Watu WAUNGWANA, WAKARIMU Na WAPOLE Kushinda Hata MALAIKA.
 
Wewe hujui wanajeshi ni raia daraja la kwanza???? Hujui wakati wewe unalala na kujimwagia mimate mashavuni wenzako ni kazi tu??? Bakabaka kuipata si mchezo waheshimu vijana wa hicho chombo.

Kwakuwa Wao Ni Daraja La Kwanza Kwahiyo Hata Wakikuambia Wewe Uiname Waku " Juma Nyosso " Kidogo Utakuwa Tayari Mkuu?
 
Wanajeshi wetu wanajiona wao ndio wao.

Sema kuna Mwanajeshi mmoja alitokea kunipenda sana akawa ananipeleka kambini kwao kufanya mazoezi

Kama Hutojali Sana Mkuu Hebu Tufafanulie Hapo Uliposema " Alitokea Kukupenda Sana " Halafu Na Hapo " Akakupeleka Kambini Kufanya Nae Mazoezi " Kwani Nimepatwa Na UKAKASI Kidogo Na Haya Maneno Ukizingatia Mimi Ni Mtoto Wa PWANI Kabisa Ambapo Kiswahili Chetu Huwa Na Maana Nyingi Sana. Nitashukuru!
 
Alinipenda sana (no homo) labda kwenye mabano ningetengeneza mazingira kama hayo.

Poa najua unatania tu.

Ni hivi, alitokea kunikubali sana alipokuwa akiniona nikiwa mazoezini, ikafikia mpaka kunichukua kwenda kufanya mazoezi kambini kwao, yeye akiwa kama Mwalimu wangu wa mazoezi.

Ikawa desturi yangu kwenda kufanya mazoezi kambini mwao.

Ni hivyo tu
 
Kuna umuhimu wakuwapeleka jkt walau kwa wiki mbili tu,aliyepita huko hawezi kuanzisha mada za kizembe hivi
 
Back
Top Bottom