Wanajeshi kutoonekana kuanzia 28 Oktoba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajeshi kutoonekana kuanzia 28 Oktoba?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ibrah, Oct 11, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nilibahatika kuwapa lift Askari wawili wa JWTZ waliokuwa wanatoka kazini huko Monduli. Kwa kuwa kuna joto la Uchaguzi Wajeshi hao walikuwa na interest sana kujua tutampigia kura nani kwa Urais hapo 31 Oktoba. Rafiki yangu aliwajibu kuwa wao (Wanajeshi) ndiyo wenye hatma ya kuamua na sio wapiga kura maana hata tukimpigia kura mpinzani kama wao Wajeshi hawataki haitasaidia kitu.

  Mjeshi mmoja wao akasema hakuna kitu kama hicho na kwao hakiwezekani. Ndipo yule rafiki yangu akajibu kuwa 'tutampa Dk Slaa'! Yule mwanajeshi akafurahi sana akasema ndiye anayefaa kuwa Rais maana Dk Slaa ndiye Rais wa Wanajeshi wa vyeo vya chini na Kikwete ni Rais wa wa Askari wanaoanzia na nyota moja! Alisema wao kama Askari wa chini wana malalamiko kuhusu maduka ya Free Duty ya Jeshi maana yanawafaidisha baadhi ya maofisa wa vyeo vya juu na hayana nafuu yoyote kwa Askari.

  Mwenzake alitutahadharisha kuwa tusishangae kutowaoana Wanajeshi wa JWTZ ifikapo tarehe 28 Oktoba uraiani maana huenda wote wakamwa makambini; hata wanaoishi uraiani wataweka kambi Jeshini hadi baada ya Uchaguzi.

  Hivyo Wadau, msishangae mtakapoona kuwa Askari wa JWTZ hawaonekani kuanzia tarehe hizo.
   
 2. dazenp

  dazenp Senior Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 101
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  thanks for the info IBRA this info helps alot.........but is it true that they say kuwa wao wanatamani kumpigia Dr Slaa......inanipa moyo sanaaaa na ninafarijika kujua hilo ila kwa upande mwingine inanishtiua.....kwa kuwa naona kama wanaweza kuwa mashushu wa kijeshi wanatafuta info.....as i have heard wote wapo makambini tayari.....wakilishwa maji ya bendera
   
 3. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu yeyote mchambuzi wa mambo hapaswi kupuuza taarifa lakini katika uchambuzi huo idadi ya watu haitakiwa kuwakilisha watu wote. Hiyo sauti ya wanajeshi wawili isiwakilishe wanajeshi wote wa vyeo vya chini. Tutakuwa tunarudi kulekule ambako baadhi ya wanajamiiforums wanalalamika kwamba tafiti za REDET na Synovate zinachukua watu wachache ( 2000 au 2600) hivyo haziwakilishi wapigakura 19,000. Ni sawa na kukutana na wafanyakazi wawili wa bandari wakasema watamchagua kikwete kisha ukasema wafanyakazi wote wa bandari watamchagua kikwete.
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  FM, kitu muhimu hapa ni kuwa kauli ya Shimbo isitutishe wananchi kwa JWTZ ni Jeshi la Wananchi na Wananchi wenyewe ndio sisi na wao JWTZ. Itakuwa jambo la kushangaza sana ikiwa JWTZ itaapambana na Wananchi kwenye zama hizi.
   
 5. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kipindi hiki ni cha kampeni mengi yatasemwa bila utafiti wa kutosha.
   
 6. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kauli ya shimbo haitakiwi kututisha hasa kama ilitolewa kwa nia njema ya kulinda amani ya nchi na si vinginevyo.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Najua habari kama hii inamchoma sana mtu kama malaria sugu.

  Lakini ndiyo ukweli wenyewe.

  Hata JK anajua.
   
 8. FIKRA MBADALA

  FIKRA MBADALA Senior Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kipindi hiki kila mwananchi anafanya utafiti binafsi, usije furahia kauli ya wanajeshi hao kumbe na wao walitumia mbinu ya kijeshi kwamba kama unataka kupata taarifa wakati mwingine unatakiwa kuwa sehemu ya adui yako. Kama unataka kupata habari sahihi za kupendwa kwa kikwete jifanye ni mkereketwa wa Dr Slaa na ukitaka kupata za Dr Slaa jifanye mkereketwa wa Kikwete. Huu ni utafiti mzuri usiowaongoza watu kwenye jibu linalohitajika. Usikute wanajeshi hao walikuwa kwenye utafiti wa kupata ishara za awali za kukubalika kwa wagombea wa urais lakini wewe ukadhani wanamtaka Dr Slaa.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  we unatafiti kipi miaka 2 jf post 40 si bora ukanywe kahawa tu unafuata nini hapa
   
 10. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  crap
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Kama vile hii stori umeikatiza njiani bana, hii tamu sana hii....kwa kweli napenda kuona wanajeshi wenye mtazamo tofauti na sio huu wa kutishana.

  Congrats
   
 12. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Huyu Askari huyu hana nidhamu, hajaiva bado anatoa siri za Gesi kwa Raia, AROO!.
   
 13. W

  We know next JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nadhani kama ni tetesi ni nzuri kuifanyia kazi na wala haina ubaya wowote either kama ilikuwa ya Kishushu au ya kiukweli. Ila tu mie naipokea kwa mitazamo miwili;

  1. Inawezekana kabisa ikawa ni muendelezo wa ile mipango ya Shimbo, kuwatisha raia, ikiwa kama kweli Wanajeshi wote hata wanaoishi uraiani, watarudishwa kambini, hofu inawezakujitokeza kwa baadhi yetu, kwani tutaambiwa hao wamepelekwa kwenda kujiandaa na vurugu kama sio vita. Sasa hali kama hiyo kwa watanzania tuliowengi, inaweza kututisha. Ingawa binafsi sitakuwa na wasiwasi wowote.

  2. Inawezekana kweli kabisa kuwa Wanajeshi pia wamechoka, jamani si huwa tunasikia watu wameasi? kwa jinsi walivyojieleza hao wajeshi, mie sioni kama kweli hawajaiva na kwamba wanatakiwa wasitoe siri za jeshi. Ukweli ni kwamba wamechoka na kwamba wanafahamu kabisa kuwa raia wema si adui ila ni wapiganaji kama wao ktk vita hii ya uchaguzi. La muhimu nikujaribu kuwaelimisha watanzania wenzetu kuto iogopa hali hiyo in case inatokea.

  Mwisho kama ndivyo hali ilivyo huko Makambini basi hapo hali inogile.
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  JK nusuru taifa jitoe bila zengwe tutakukumbuka kwa hilo lakini hayo mengineyo unayoyatafuta ujue utakwama. Hayana baraka ya Mwenyezi Mungu
   
 15. I

  IMBOMBONGAFU Senior Member

  #15
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we subiri.tutawavunja miguu,mumeanza kulidharau Jeshi nyie.Hili Rinchi ovyo kabisa maraia yameanza kutukana majeshi tutawafunja miguu yenu hiyo.. mbafuuuu.
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Majibu yako yanafanana na nyimbo za taarabu za uswazini. Huna hoja umekimbilia idadi ya posts.
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Na ashitakiwe kijeshi anatoa siri za jeshi.
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi hata MAASI ya KIJESHI yakitokea, ni hawa wa vyeo vya chini huwa wanafanya.

  Hawa Maafisa wa JESHI mara nyingi huwa MATAWI na wako juu kabisa wanakula kuku zao.

  Ni hawa Maafisa wasio na nyota kurudi chini ndiyo wana-Vumilia Vumbi Vichakani.
   
 19. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Nimependa tahadhari yako! Nilitaka niandike Aisee Una Akili wewe, nikaona labda utafikiri nakutusi, but you just made a very important observation, not everything you hear means what you hear!
   
 20. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hivi ndugu zangu mnadhani wanajeshi wanatoka mbinguni??? Si wanatoka miongoni mwetu wananchi na tunaishi nao maisha ya kawaida!! Kama ni karaha na shida inayosababishwa na uongozi mbovu wa kikwete nao pia wanaipata. Sasa kwa nini wao wanajeshi wasimpigie debe mgombea anayeonekana atawaondolea shida zao. Mimi ninaamini kabisa kwamba asilimia kubwa ya wanajeshi, polisi na magereza watakuwa wamechoshwa na uongozi wa kisanii wa kikwete kwani nao ni sehemu ya watanzania. Kwa taarifa yenu ndugu zangu hata usalama wa taifa ukiondoa wakubwa wanaofaidika, nao wamechoka sana ndiyo maana performance ya rais ni hovyo kuliko marais wote walioongoza nchi hii.

  Haki ya watanzania mwaka huu italindwa na Mungu mwenyewe. Hata ccm ikifanya mbinu za aina gani lazima iabike mwaka huu kwani imewanyanyasa watanzania kupita kiasi.
   
Loading...