Wanajeshi kambi ya Lwamishenye wavamia mtaa na kuua raia

KAUDO

Senior Member
Aug 10, 2011
138
67
Hadi muda huu watu wawili wamefariki dunia baada ya wanajeshi wa Kambi ya Lwamishenye mjini Bukoba kuvamia mtaa wa Anyama na kutembeza kipigo.

Pia muda mfupi uliopita polisi wamewatawanya wananchi waliofika kituo cha polisi Bukoba wakiandamana kupinga mauaji hayo.

Habari zaidi baadaye,niko kwenye mtaa husika kuongea na familia zilizopoteza ndugu zao.
 
Kaudo, Ahsante kwa taarifa lakini haijitoshelezi. Kwanini wanajeshi wamevamia mtaa?
 
Kazikazini issue,Kusini,usiseme!Magharibi nako kimenuka!!Mdau aliyeleta post inayosema Hakika JK ni Rais mwenye bahati sana Duniani hajakosea!!

Gap kubwa linazidi kujengeka kati ya polisi,jeshi na Wananchi!!!Tukianza kuviziana kuna kupona kweli!!!

Damu zote zisizo na hatia hakika zitakuwa mikononi mwako!!!!!
 
tupatie na picha kaka,ila angalia usijetafuta samaki barabarani, siunajua tena kamanda

Hadi muda huu watu wawili wamefariki dunia baada ya wanajeshi wa Kambi ya Lwamishenye mjini Bukoba kuvamia mtaa wa Anyama na kutembeza kipigo.

Pia muda mfupi uliopita polisi wamewatawanya wananchi waliofika kituo cha polisi Bukoba wakiandamana kupinga mauaji hayo.

Habari zaidi baadaye,niko kwenye mtaa husika kuongea na familia zilizopoteza ndugu zao.
 
watakua hao wanajeshi wametoka kulewa gongo nyakanyasi. Mtu mwenye akili zake hawezi kumua binadamu mwenzake hivihivi. kaeni machugamachuga, watawaibukieni hapo mjini kati.
 
watakua hao wanajeshi wametoka kulewa gongo nyakanyasi. Mtu mwenye akili zake hawezi kumua binadamu mwenzake hivihivi. kaeni machugamachuga, watawaibukieni hapo mjini kati.

Una uhakika na unachosema!!? Subiri taarifa rasmi!! usikurupuke.
 
Ilikuwaje tena jamani?Hawa jamaa siyo wa kuwatania kabisa aisee,wakifunga mtaa wanapiga hadi kuku.Poleni sana waathirika mungu awatie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu!!
 
hii ni one sided info..., subiri the other side watasemaje..., then uta-judge,,
Watz bado wanaogopa magandwa yale wale hamna kitu! Wananchi mkiamua mnawatandika tu! Narudia tena wakiwa hawana bunduki wale weupe kabisa! Wanajua uoga wa wananchi waende Tarime kama watapiga raia ovyo!
 
watakua hao wanajeshi wametoka kulewa gongo nyakanyasi. Mtu mwenye akili zake hawezi kumua binadamu mwenzake hivihivi. kaeni machugamachuga, watawaibukieni hapo mjini kati.

Machugamachuga? Lugha nyingine bana!
 
Back
Top Bottom