Wanajeshi (JWTZ) Wasaidie kufundisha maadili na Uzalendo Majeshi mengine ya Tanzania

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Salaam Wakuu,

1. Kipindi cha Kikwete, Wanasiasa walipelekwa JKT kujifunza Uzalendo na Maadili. Hii napendekeza iendelee kwa Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu wakuu, Wakuu wa Wilaya na Mikoa.

2. Polisi, Usalama wa Taifa na Askari wa amani, Waende JWTZ kujifunza kwanini Wanaogopwa lakini JWTZ ni rafiki wa raia.

3. Polisi, Usalama wa Taifa na Askari wa amani, Wajiulize kwanini JWTZ hawapokei Rushwa.

4. Vyombo vya Usalama vyote, Vijifunze JWTZ kwanini hawajihusishi na Siasa na kujipendekeza kwa Wanasiasa

5. Wanajeshi ni Kimbilio la Wananchi, nini siri ya Urembo? Majeshi mengine yakajifunze.

Majeshi yetu yangekuwa na Utii na weledi wa kama JWTZ, Nchi yetu ingekuwa Tajiri.

Majeshi yetu yajitathimini kwa manufaa ya Nchi ya Tanzania.
 
Ili uchukue rushwa nature ya kazi yako iwe kutoa huduma kwa wananchi moja kwa moja na ndo maana mahakama,tra,police,tanesco au uhamiaji rushwa ziko juu.sasa JWTZ waombe rushwa wapi vitani au.tunaweza kupima uadilifu wao wakipewa kazi kama za wenzao.same inaenda kwa siasa.
 
Duniani kama mtu hakujui atakuheshimu sana!!!
Polisi, magereza, zimamoto na uhamiaji
Laiti wangekuwa wanafanya majukumu yao bila kuwaingilia wananchi/raia moja kwa moja na hasa kugusa mpaka uchumi kupitia tozo mbalimbali, raia/wananchi wangewapenda sana,

Sasa niende JWTZ kulipia huduma gani au wanitoze faini kwa majukumu gani, ndio maana inaonesha wanaonekana wametulia.

Nimeandika kikubwa sana kwa uelewa.

Sent from my iphone using JamiiForums mobile app
 
Hiyo Elimu ianzie JWTZ kwanza, kwa maoni yangu mimi Wanajeshi wetu hawajui hata jukumu lao ni nini kwenye jamii, wanapiga raia ambao wanapaswa kuwalinda kila mara, ninaishi eneo ambalo kuna Wanajeshi wakimaliza mafunzo tu ya kivita ambapo wanafundishwa kupigana na adui wanakuja uraiani kuleta fujo na kuanza kupiga raia, kwa nini ?

Ni mara ngapi raia anakamatwa na Wanajeshi na kupewa adhabu kwa kuwa tu kapita eneo la Jeshi ni nani kawapa Mamlaka ya kuadhibu raia ambao wako kuwalinda?
Kwenye nchi ya haki adhabu hutolewa na Mahakama tu .

Hivyo kwangu mimi Wanajeshi wetu wanahitaji Elimu sana tu, kujua majukumu yao kwenye jamii ni yapi, Mwanajeshi hata barabarani ubabe tu, Sheria za barabarani hawatii kwa nini ?

Hakuna kitu hapo, ningependekeza tuanze kufanya IQ testing kabla ya kumkubali raia yoyote kuwa Mwanajeshi au Polisi , …
 
Hao wanajeshi wako hawafanyi kazi uraiani wao kazi yao ni kulinda mipaka, badili sheria waanze kukamata watu uone
 
Salaam Wakuu,

1. Kipindi cha Kikwete, Wanasiasa walipelekwa JKT kujifunza Uzalendo na Maadili. Hii napendekeza iendelee kwa Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu wakuu, Wakuu wa Wilaya na Mikoa.

2. Polisi, Usalama wa Taifa na Askari wa amani, Waende JWTZ kujifunza kwanini Wanaogopwa lakini JWTZ ni rafiki wa raia.

3. Polisi, Usalama wa Taifa na Askari wa amani, Wajiulize kwanini JWTZ hawapokei Rushwa.

4. Vyombo vya Usalama vyote, Vijifunze JWTZ kwanini hawajihusishi na Siasa na kujipendekeza kwa Wanasiasa

5. Wanajeshi ni Kimbilio la Wananchi, nini siri ya Urembo? Majeshi mengine yakajifunze.

Majeshi yetu yangekuwa na Utii na weledi wa kama JWTZ, Nchi yetu ingekuwa Tajiri.

Majeshi yetu yajitathimini kwa manufaa ya Nchi ya Tanzania.
View attachment 2023974
Mabeyo aanza kumfundisha Sirro kwanza.
 
Jwatz wako mbali na pesa kuliko majeshi mengine sababu awatoi huduma.Hivyo lzm wawe hivyo.
 
Salaam Wakuu,

1. Kipindi cha Kikwete, Wanasiasa walipelekwa JKT kujifunza Uzalendo na Maadili. Hii napendekeza iendelee kwa Mawaziri, Wakurugenzi, Makatibu wakuu, Wakuu wa Wilaya na Mikoa.

2. Polisi, Usalama wa Taifa na Askari wa amani, Waende JWTZ kujifunza kwanini Wanaogopwa lakini JWTZ ni rafiki wa raia.

3. Polisi, Usalama wa Taifa na Askari wa amani, Wajiulize kwanini JWTZ hawapokei Rushwa.

4. Vyombo vya Usalama vyote, Vijifunze JWTZ kwanini hawajihusishi na Siasa na kujipendekeza kwa Wanasiasa

5. Wanajeshi ni Kimbilio la Wananchi, nini siri ya Urembo? Majeshi mengine yakajifunze.

Majeshi yetu yangekuwa na Utii na weledi wa kama JWTZ, Nchi yetu ingekuwa Tajiri.

Majeshi yetu yajitathimini kwa manufaa ya Nchi ya Tanzania.
View attachment 2023974
Hiyo mbona inafanyika sana jeshini kipindi cha jkt kwa mujibu?
 
JWTZ ni jeshi lenye nidhamu ya hali ya juu na hakuna Mtanzania yeyote katika nchi hii anaweza asijue hili,jeshi hili linafanya kazi nzuri yenye kutukuka huko nje kwa sababu ya nidhamu yake ya hali ya juu,ili jeshi letu limefeli kitu kimoja tu ndani ya TAIFA letu kuwaachia sana wanasiasa kuendelea kuifinyanga nchi kwa ufisadi na Rushwa za kutisha huku watanzania wakiendelea kuteseka huko AFRIKA MAGHARIBI MAJESHI YA HUKO HAYAJAVUMILIA KABISA VITENDO VYA KIJINGA NA KIPUMBAVU VYA UFISADI WA KUTISHA NA RUSHWA ZA KUTISHA.TUMESHUHUDIA WANASIASA WALAFI WAKIONDOLEWA KWENYE UONGOZI ILI KULINDA MAADILI YA UONGOZI YALIYO MEMA.HAPO JESHI LETU LIJITAFAKARI TENA SIO KIDOGO.
 
Yes/No JWTZ wajibu wao mkubwa ni kulinda mipaka ya nchi yetu,je hii kazi inafanyika vema?mmmm nchi imekua ni hub ya human trafficking syndicates,drugs cartels wanatumia bandari zetu bubu kusafirisha drugs (sijui ile case ya drugs pale kilwa imeishia wapi),ningependa nami tuige mfano wa Botswana na Zambia wa kuwa na check points zinazolindwa na Jeshi(Botswana wapo superb na check points hizi na waliosafiri kwa njia ya barabara ndani ya nchi hii wataafikiana nami)Zambia mmmm kuna wanajeshi nao wanachukua rushwa!ingawa serikali mpya imeondoa road block nyingi tu na kubakisha check points only.
 
Duniani kama mtu hakujui atakuheshimu sana!!!
Polisi, magereza, zimamoto na uhamiaji
Laiti wangekuwa wanafanya majukumu yao bila kuwaingilia wananchi/raia moja kwa moja na hasa kugusa mpaka uchumi kupitia tozo mbalimbali, raia/wananchi wangewapenda sana,

Sasa niende JWTZ kulipia huduma gani au wanitoze faini kwa majukumu gani, ndio maana inaonesha wanaonekana wametulia.

Nimeandika kikubwa sana kwa uelewa.

Sent from my iphone using JamiiForums mobile app
Mafunzo Yao yana wafanya wawe na maadili nikupa mifano mitatu, kuna ndugu yangu alikojoa eneo la jeshi aka kamatwa na Askari mmoja alikuwa na elfu hamsini mfukoni akataka kumuonga elfu 20,000 Askari akaikataa je angekuwa polis angeikataa?, Kipindi cha magufuri wanajeshi walikuwa Wana linda korosho Bandarin walikuwa wanafatwa wakubali tu makontena ya funguliwe mzingo uchukuliwe wao walipwe pesa mbona walikuwa Wana kataa je wangekuwa polisi wange kataaa kuiba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa katiba yetu Tanzania ina Majeshi Manne
Mleta mada amesema majeshi mengine, hajaainisha Polisi tu
Unapotoa mifano hiyo, tolea pia kwakuzingatia Magereza na Zimamoto.

Sent from my iphone using JamiiForums mobile app
 
Kwa katiba yetu Tanzania ina Majeshi Manne
Mleta mada amesema majeshi mengine, hajaainisha Polisi tu
Unapotoa mifano hiyo, tolea pia kwakuzingatia Magereza na Zimamoto.

Sent from my iphone using JamiiForums mobile app
Polisi ndiyo jeshi linalo ongoza kwa matendo mabaya. Mpaka Raia wa kigeni Wana sema polis wetu Wana penda rushwa Sana ndiyo maanza mzungu akipata tatizo anaenda kumuuliza security wa kampuni binafsi ana amini ata pata msaada kuliko kwenda kwa polisi akaombwe rushwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jwtz wanajiheshimu na hawana maujinga kama majeshi mengine na wao wamenyooka straight forward na hawataki utani. Mimi mtu akiniambia eti uhamiaji, police ni jeshi nakataa maana wao ndio wahalifu number one wanaokula rushwa na uchafuzi mwengine
 
Pia kuna tetesi miaka ya sasa huwezi kupata nafasi ya kuwa mwanajeshi wa jwtz bila kuhonga au kuwa na undugu au urafiki na wahusika wa huko jeshini

Kwahiyo hata huko jwtz siyo salama sana

Wakati huo huo huo kwa kuwa Tanzania hakujatokea vita kwa miaka mingi tangu Ile ya kagera ni vema kuangalia namna bora ya kuwatumia wanajeshi wetu watusaidie kwenye vitu kama ujenzi wa mashule, vyuo vikuu na hospitali badala ya kukaa tu kupiga gwaride mwisho wa mwezi mshahara kama kawaida

Pia wanaubabe wa kishamba mtaani, wanaweza kukupiga tu kama umewaibia kitu bila kukufikisha au kuripoti polisi kwanza (wanajichukulia sheria mkononi)

Mtaani wakitongoza mwanamke akawakataa inakuwa vita utadhani kuna sheria imewaruhusu wakitongoza lazima wakubaliwe!

Bado kuna shida hapa Tanzakiza
 
Siku hizi wameacha kufanya usafi huko mitaani wakisikia siku hio Kuna kongamano la Katiba mpya?
 
Back
Top Bottom