Wanajeshi 66 wameuawa Sudan Kusini

Fede Masolwa

JF-Expert Member
Oct 26, 2013
528
123
Afisaa mkuu msimamizi wa hospitali ya kijeshi ya Juba, Brigedia Gen Dr Ajak Bullen,ameambia shirika la redio la Miraya mjini Juba kuwa wanajeshi 66 wameuawa katika mapigano ya siku mbili.

SOURCE ;
http://www.bbc.co.uk/swahili/
 
Mkuu ukifungua page ya bbcswahili.com wameandika tuu hii habari bila kufafanua wanajeshi kutoka wapi.

120416152201_sudan_304x171_afp_nocredit.jpg

Afisaa mkuu msimamizi wa hospitali ya kijeshi ya Juba, Brigedia Gen Dr Ajak Bullen,ameambia shirika la redio la Miraya mjini Juba kuwa wanajeshi 66 wameuawa katika mapigano ya siku mbili.

  • Watafanyiwa mazishi ya pamoja
Wakati huohuo afisaa mmoja wa serikali amesema kuwa watu 26 wameuawa katika mapigano ya siku mbili mjini Juba.
Zaidi ya watu miamoja wamejeruhiwa huku maafisa wakuu wakijaribu kudhibiti mji huo kufuatia kile ambacho serikali ilisema ni jaribio la mapinduzi mbalo liliweza kutibuliwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Barnaba Marial Benjamin amesema kuwa vikosi vya usalama vinawasaka wanajeshi watiifu kwa Riek Machar aliyekuwa makamu wa Rais wa Salva Kiir anayedaiwa kupanga njama hiyo ya mapinduzi.
Taarifa zinasema kuwa milio ya risasi ingali inasikika mjini Juba.

Wanajeshi wa nchi gani? Mbona unaandika kwa haraka hivyo!
 
Wakijaribu wakwetu wanajua tutawajua na kumshughulikia aliyewatuma!!!
 
unatupa pressure kijana andika vitu kamili utaongeza idadi ya vifo bure
 
asante kwa taarifa ila siku nyingine uwe unaangalia na vyanzo vingine vya habari ili kuleta habari iliyokamili...sasa mimi nilijua labda wanajeshi wetu
 
asante kwa taarifa ila siku nyingine uwe unaangalia na vyanzo vingine vya habari ili kuleta habari iliyokamili...sasa mimi nilijua labda wanajeshi wetu
mweee nilikuwa nimeshtuka maana nina rafiki yangu yuko pale sinza na mumewe amekwenda huko sudani ndugu yule dada halali usingizi ni mawazo kweli kweli ndio aje akutane na hii khabari anaweza kufa ati
 
Wanajeshi wa nchi gani? Mbona unaandika kwa haraka hivyo!

Hawa ni wenyewe kwa wenye. Kulikuwa na jaribio la kupindua serikali. Baada ya kujitenga kutoka Sudan bado hawajaridhika wanazidi kugawanyika.... Ni ule msemo wa mwalimu kuwa wanzanbar wakijitenga watajiona kuna wazanzibara na wazanzibari. Sasa wao huko kuna makabila mawili nayo yanagombana
 
Mkuuu sio mpango malizia taarifa unatutisha siunajua jeshi letu la ukweli lipo uko,kuwa makini.
 
anakufa bure..kumbe kalishwa tango pori..... kwa kweli kuna haja ya kufundishana namna ya kuriport matukio....siku hizi watu huwa wanakurupuka tu...ukisoma kichwa cha thread na vilivyomo ndani tofauti......watakuja kuuwa watu siku moja hawa wanaokurupuka kuandika habari
 
Hawa ni wenyewe kwa wenye. Kulikuwa na jaribio la kupindua serikali. Baada ya kujitenga kutoka Sudan bado hawajaridhika wanazidi kugawanyika.... Ni ule msemo wa mwalimu kuwa wanzanbar wakijitenga watajiona kuna wazanzibara na wazanzibari. Sasa wao huko kuna makabila mawili nayo yanagombana
Miezi kadhaa iliyopita nilielezewa na Msudani wa "Kaskazini" kuhusu njaa,dhiki na shida zilizowakumba raia wa Sudan ya Kusini huku viongozi na wageni (Wakenya wanatajwa) wakinufaika.

Wanaamini kuwa viongozi wao wamewapandisha "mkenge" kwa kujitenga na wakaskazini,kuna mpaka "vilio" mitaani vikitaka warudi kwenye muungano.

Machafuko ya kutaka kupinduana hayawashangazi wengi wa wanaoijua hali halisi.

Ila kwa vyovyote vile muungano wao na wa-Watanazania usifananishwe.
 
Back
Top Bottom