Wanajamvi wenye vyeti feki muichukue kama ilivyo japo inauma

Kuhakiki wahakiki tu. Lakini, suala la majina halina hata msaada wowote kwa sababu mtu anauhuru kisheria kuitwa anavyotaka wakati wowote akitka.

Kurudisha mishahara siyo hukuku halali kwa sababu haiko kwenye sheria yoyote ya utumishi wa umma. Mishahara hawakulipwa kwa sababu ya vyeti, walilipwa kwa sababu ya kufanya kazi. Kama walikuwa wanalipwa mishahara bila kufanya kazi ama kazi zao ziko hcini ya kiwango, kokoro hili liende hadi kwa mwajiri na wasimamizi wao wa akzi. Ni vipi waliaendelea kukaa na wafanyakazi wasioweza kufanya kazi na bado wakawalikpa mishahara? Serikalilini hakuna performance appraisal za wafanyakazi? Appraisal zao zilireport nini? Nani anazisoma na kuzifanyia kazi? Kama walikuwa appraised kila mwaka, wasimamizi wao na waajiri wao ama wakawa wazembe kama ilivyo kawaida ya serikali, au wakaridhika, nani akatwe misharahara? Hao waliokuwa wakiwalinda kazini wanaponea mlango upi katika suala zima la uwajibikaji na uwezo wa kufanya kazi zao?

Wakiwashitaki kwa udanganyifu, hapo sawa. Lakini wakiwashitaki kwa wizi wafedha kwa njia ya mishahara, lazima na wasimamizi na wajiri wao waunge bodi.

Ila tunaomba database yenye majina yote na profile fupi za watumishi wa umma, ianzishwe. Vyeti vingi vimeibiwa na watu wengi walifanya biashara yakuuza nafasi za wanauni hasa vijijini. Tutaisaidia serikali. Vinginevyo hii itakuwa ndiyo kazi hadi miaka 6 ijay.
 
Mmh... Namhurumia yule askari wa sumbawanga ambaye jina lake linaanzia herufi "P" wakati huku Mwanza tulizoea kutumia jina linaloanzia na herufi "M" kwake yeye na hiyo "P" ilikuwa ni herufi ya kwanza ya jina la kaka yake.
 
Wapendwa habari, Kwa wale ambao vyeti vyao ni feki hasa cha form four au form six na ni muajiriwa wa serikali, na wale wanaotumia majina na vyeti vya ndugu au marafiki zao, wanashauriwa kuacha kazi mara moja.. tena kwa uharaka..

Narudia acha kazi kabla hawajaja kukugundua.. ukaguzi umeanza kwa baadhi ya taasisi na mashirika ya umma..

Watu wanazimia hovyohovyo wakiulizwa kuhusu cheti cha form four na cheti cha kuzaliwa.

Kama cheti chako cha kuzaliwa nacho kimefojiwa ili kiendane na cha form four au form six yaani wewe UMEKWISHA KABISA.

Kama mfano wewe upo idara ya elimu na aliyekupa cheti au uliyempa cheti yupo idara nyingine mfano polisi au afya, basi nyote wawili mko hatarini kufungwa na kurejesha fedha zote za serikali ikiwemo mishahara ulizowahi kulipwa.

Kwa wale ambao nyumbani walikozaliwa wanajulikana kwa majina yao halisi mfano John J. Khamisi na kazini wanaitwa Petter S. Rutaza ndio hao haswaaa wanatafutwa kwa UDI na UVUMBA.

Umetengenezwa mtandao ambapo unaratibu majina na vyeti vyote. HAPA KAZI MOJA MTU MMOJA. Mtaarifu na ndugu yako inauma hasa kwa wale mnaowategemea Ndugu walio kwenye hii kasumba ila kwa kuwa tuliipenda wenyewe basi haina budi kuvumilia MUNGU yupo
Watarudisha mishahara kwa sheria ipi au ya mwendo kasi nakazi walizokuwa wanazifanya za kujenga nchi mhaaa! Nahawa wanaolinda raia je nao watakaguliwa maana uko ndio hatari watu wanamavyeo je zoezi litafika huko au manesi na wafanya kazi wengine ndio watakao onewa maana hawa ndio wanao waonea kweli
 
Wengi wetu tunafanya mzaa humu jamvini kwa kuwa haturejei madhara ya kimaendeleo yanayotokana na wafanyakazi wenye vyeti na taaluma feki.

Ebu tufikiri madhara ya afya ukipimwa na mtaalamu feki! Mfano mwingine ni leseni feki za udereva. Naamini ajali za barabarani, hasa mabasi (mbali za bodaboda) zinasababishwa na madereva wenye leseni bandia au za ndugu zao.

TUSILIONE ZOEZI HILI LA KUKAMATA WASIO NA VYETI HALALI KAMA LA UONEVU.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Mimi nina cheti cha form cha mtu mwingine lkn cheti hicho sio feki na nikakitumia kusomea certificate sasa nimeajiriwa serikali je wataweza kunibaini?Mwenye cheti hicho alishakufa na hakuwaikuajiriwa serikalini
Kajisalimishe!!niyi haswa ndio mnatafutwa.
 
Jeshi la Polisi itakuwa kiama maana nnaowajuwa binafsi mpaka sasa hawapungui 20. Hapa kazi tu
 
Wengi sana wenye vyeti feki na vyeti vinavyotumika Mara mbili, mie nawafahamu kabisa yaani hata wakisema niwataje naweza kutaja ,
 
Wengi wetu tunafanya mzaa humu jamvini kwa kuwa haturejei madhara ya kimaendeleo yanayotokana na wafanyakazi wenye vyeti na taaluma feki.

Ebu tufikiri madhara ya afya ukipimwa na mtaalamu feki! Mfano mwingine ni leseni feki za udereva. Naamini ajali za barabarani, hasa mabasi (mbali za bodaboda) zinasababishwa na madereva wenye leseni bandia au za ndugu zao.

TUSILIONE ZOEZI HILI LA KUKAMATA WASIO NA VYETI HALALI KAMA LA UONEVU.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Hata ukiwa na leseni og leseni ndiyo inayoendesha gari ha ha haa
 
Back
Top Bottom