Wanajamvi wa forum hii tuiokoe tanzania.Usipite bila kuacha neno lako hapa.

LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,123
9,155
Ndugu wanajamvi wataalam wote kila fani mim nilikuwa na wazo.Tatizo la uchakachuaji mafuta imekuwa fashion sana tanzania.Nazan lingekuwa ni tatizo la kidunia mda mrefu wenzetu wangekuwa washalipatia ufumbuzi.

Mim ni fundi umeme wa magari kwa upeo na uelewa wangu kuna sensor nyingi sana ambazo huundwa kwa lengo maalumu na pindi mambo yaendavyo ndivyo sivyo haraka sana majibu hutolewa.
Ikiwa kuna fire alam,oxygen sensor,knock sensor,n.k

je haiwezekani wana taalam watanzania tusigundue sensor ambayo itakuwa inasensi mafuta na kama yataongezwa kitu cha ziada mbali na vile vilivyo unda mafuta yale basi sensor itoe signal fulan ambayo itasaidia kutoa actio ikiwezekana hata kuzima gari au kustopisha pump isioperate na kuvuta mafuta hayo yaliyo chakachuliwa.
Mfano:pETROL ni muunganiko wa x,y,z tuchukulie kwamba wachakachuaji wamechakachua na kuongeza mafuta ya taa ambayo huundwa na a,x,b so hapo kama petrol na kerosene vitachanganywa itapatikana x,y,z,a,x,b so hapo sensor ifanye kazi ya kudetect uwepo wa A na B.
na sensor hiyo iwekwe/fungwa kwenye tank la mafuta.

Je ndugu wanajamvi wa forum hii hili haliwezekani??

naliwasilisha kwenu wandugu.
 
Japo nilifeli chemistry na physics teh th teh teh Una maana gani ukisema sensor. ?

"Sensor ya kikemikali" kama litmus paper ambayo ikitengenezwa na kubuniwa mafuta yakawa hayana compsoition sahihi itabadilika rangi au sensor za ki-electronic ?
 
hilo wazo zuri sana mkuu japo sichelei kusema huyo atakayetengeneza ama kubuni hiyo sensor atahongwa na wenye masheli kutengeneza chemikali ya ku neutralize detection capability...
 
Landrover discovery 4 ina hiyo kitu...ukiweka chakachua inafunga mfuniko wwa mafuta mara moja!!
 
Sasa naamini wapo great thinkers JF. Tulifanyie kazi halafu tujuzane.
 
Hii kitu ipo kwenye gari nyingi tu mfano kuna scania R420 pembeni kabisa ya dash board kuna taa nyekundu ya square ina herufi IDC. Engine diesel control. Volvo kubwa za kisasa nyingi zina hii kitu
 
Nimerudi tena. ukweli ni kwamba uchakachuaji unaleta usumbufu na hasara kwa wenye magari na mitambo na taifa kwa ujumla. Ukweli ni kwamba inarudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa kiwango cha kutisha.
Tatizo hapa ni chombo kinachosimamia (EWURA). Kimekuwa na matamko ya kisiasa mno kuliko ya utendaji. Mwaka 2006 India walipata tatizo hili na kuchukua maamuzi ya haraka kwa kuanzisha mfumo wa kutifautisha mafuta ya ta kwa rangi "marker" ambayo huwezi kuichezea na ikichanganywa na petroli au diseli inagundulika mara moja Govt launches new tool to detect fuel adulteration - Economic Times
Kweli hili ni janga la kitaifa na itabidi kuumiza vichwa kweli kweli. Mimi gari lang halina mfumo wa kufafanua uchakachuali kwa hiyo mafuta nanunua kwa kubuni tu. Ewura walisema wataanzisha mfumo wa "marker" kabla ya Agosti na sina hakika kama kweli wamefanya hivyo. si unajua tena...
 
Japo nilifeli chemistry na physics teh th teh teh Una maana gani ukisema sensor. ?

"Sensor ya kikemikali" kama litmus paper ambayo ikitengenezwa na kubuniwa mafuta yakawa hayana compsoition sahihi itabadilika rangi au sensor za ki-electronic ?

mkuu ulivyo elewa ndiyo hivyo hivyo.

Mi namaanisha sensor ya kielectronics mkuu,lazima iwe ya kielectronic kwani utendaji wake utakuwa wa kielectronic.
 
Landrover discovery 4 ina hiyo kitu...ukiweka chakachua inafunga mfuniko wwa mafuta mara moja!!

mkuu naomba unifafanulie vizuri au kama unaweza elezea japo kwa ufupi tuu mfumo wake.
 
Ndugu wanajamvi wataalam wote kila fani mim nilikuwa na wazo.Tatizo la uchakachuaji mafuta imekuwa fashion sana tanzania.Nazan lingekuwa ni tatizo la kidunia mda mrefu wenzetu wangekuwa washalipatia ufumbuzi.

Mim ni fundi umeme wa magari kwa upeo na uelewa wangu kuna sensor nyingi sana ambazo huundwa kwa lengo maalumu na pindi mambo yaendavyo ndivyo sivyo haraka sana majibu hutolewa.
Ikiwa kuna fire alam,oxygen sensor,knock sensor,n.k

je haiwezekani wana taalam watanzania tusigundue sensor ambayo itakuwa inasensi mafuta na kama yataongezwa kitu cha ziada mbali na vile vilivyo unda mafuta yale basi sensor itoe signal fulan ambayo itasaidia kutoa actio ikiwezekana hata kuzima gari au kustopisha pump isioperate na kuvuta mafuta hayo yaliyo chakachuliwa.
Mfano:pETROL ni muunganiko wa x,y,z tuchukulie kwamba wachakachuaji wamechakachua na kuongeza mafuta ya taa ambayo huundwa na a,x,b so hapo kama petrol na kerosene vitachanganywa itapatikana x,y,z,a,x,b so hapo sensor ifanye kazi ya kudetect uwepo wa A na B.
na sensor hiyo iwekwe/fungwa kwenye tank la mafuta.

Je ndugu wanajamvi wa forum hii hili haliwezekani??

naliwasilisha kwenu wandugu.
Ewura tayari wana mitambo ya kutambua mafuta yaliyochakachuliwa, sijui kwa nini bado tatizo hili linaendelea.
Lakini, hata bila ya kuwa na mitambo hiyo, kukiwa na udhibiti mahiri wa bidhaa za mafuta, tatizo hili halitatokea.
tatizo zaidi lipo kwenye vichwa vya hawa wafanyabiashara wwetu, wanataka faida kubwa ya haraka haraka... kujitengenezea utajiri wa haraka haraka ni tatizo la kitaifa, kuanzia kwa viongozi wetu, tangu ngazi za juu kabisa, hadi kwa katibu kata
 
Hata Landcruiser V8 zina hii kitu. ngoma haiwaki kama mafuta ni ya kuchakachua. Nafikiri soon device hizi zitakua madukani kama itaonekana kuna demand.

How it works.
Kuna sensor ndani ya tanki ambayo ina detect viashiria vya uchakachuaji. kama kukiwa na viashiria hivyo based on chemical composition basi itawaka taa ya warning na garo haiwaki hadi urectify problem, normaly kwa kudrain out mafuta na kuweka mafuta safi.
 
hii sio nzuri kwa sababu inaruhusu mafuta yaingie ndio igome kuwaka.ya discovery ikisense inazuia kabisa mafuta yasiingie kwenye tank
 
kijana watu wameweka hapo juu unaweza jifunza kwa kuangalia hao wengine wamefanyaje!
 
Hata Landcruiser V8 zina hii kitu. ngoma haiwaki kama mafuta ni ya kuchakachua. Nafikiri soon device hizi zitakua madukani kama itaonekana kuna demand.

How it works.
Kuna sensor ndani ya tanki ambayo ina detect viashiria vya uchakachuaji. kama kukiwa na viashiria hivyo based on chemical composition basi itawaka taa ya warning na garo haiwaki hadi urectify problem, normaly kwa kudrain out mafuta na kuweka mafuta safi.

mkuu unaweza nijuza huo mfumo unaitwaje au sensor inayohusika kwenye mfumo huo inaitwaje??
Ili nijaribu ku google..
 
ni wazo zuri saaana, kwa bahati mbaya nilijikita sn kwenye masomo ya biashara hv mtakapotengeneza tafadhali tuwasiliane kwenye swala la soko.
 
Utafiti huo utafanywa na nani? Hapa Bogo ipo taasisi yenye uwezo wa kufanikisha swala kama hilo? Lakini siyo lazima kugundua gurudumu upya. Kama teknolojia hiyo tayari ipo taasisi yenye uwezo inaweza kuomba license kutoka kwa wagunduzi ili kuzitengeneza locally kwa lengo la kuzifanya kuwa za bei nafuu. Lakini nijuavyo mimi ili taasisi iweze kupata hiyo license lazima iwe na ushahidi wa uwezo na ubora kiuzalishaji (industrial/production capacity and quality) pamoja na kuaminika katika kulinda haki za wagunduzi (intellectual property/patent protection). Bongo tunayo taasisi kama hiyo?
 
Mkuu hii kitu ipo kwenye baadhi ya magari, unakumbuka magari ya ikulu ya JK nadhani kule moshi yaliwekwa mafuta yaliochakachuliwa na magari yakajibu palepale na kugoma kuwaka.
Sijui mfumo wake ukoje kama mafuta yanabainiwa na mtambo pale yanapoingia au yakisha ingia tank kuu kabla hayajavutwa na pump ndio yanabainiwa? lakini hii uchakachuzi hatukuanza sisi mkuu, haya ni marudio tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom