Wanajamvi hiki chama makini ni kama odm ya nchini kenya!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanajamvi hiki chama makini ni kama odm ya nchini kenya!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Twaa, Apr 13, 2012.

 1. T

  Twaa Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanajamvi hili nalo ni jambo ambalo halipingiki ktk mtizamo wa siasa, ama kweli hali ya CDM ni kama ODM kutoka nchini kenya kwa uadilifu wa viongozi wa wao na mipango ya nchi ya kenya hapo baadae! Na pia hata viongozi wa CDM kutoka hapa nchini wapo kama wale wa ODM! IKUMBUKWE kwamba wanaODM WANAPENDA serikali za majimbo na vivyohivyo wanaCDM ndio mkazo wao ktk mtazamo wa maendeleo ya nchi yao yaani tz yetu! ODM iliibuka na ushindi mwaka 2007 lakini walipokonywa na fisadi wa madaraka Kibaki, na leo nasema hivi ''hata CCM wafanye hujuma ya aina gani lazima wataondolewa madarakani yaani CDM Itashinda 2015! na kukabidiwa dola ila kama watahujumiwa kama walivyohujumiwa ODM nakwambia patachimbika bila mzaha! Kwenu wadau na maoni yenu!
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Serikali za majimbo ni nzuri sana, kila mkoa uwe na (gavana) anaechaguliwa na wananchi. Mkoa ujipangie wenyewe maendeleo yake kwa kodi zao. Mkoa kama arusha una madini ya tanzanite lakini barabara ya kwenda huko migodini haina lami!
   
 3. engwe1980

  engwe1980 Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haswaa CDM ndiyo ODM yetu hapa Tanzania.
   
 4. m

  mwanakidagu JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yap.respect kwa kuibua wazo linganifu.cdm vs odm
   
 5. K

  Kasimpya Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Serikali ya majimbo ni nzuri kwani kila jimbo litakuwa na maendeleo kwa kutumia rasilimali llilizonazo. Vile vile viongozi wa majimbo watawajibika kwa wananchi kwani watakuwa wanachaguliwa na wananchi, hivyo kuwa na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
   
 6. m

  majiyachai Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamanda, hapo umetoka nje ya mstari kabisa. Inaelekea ODM huijui hata kidodgo. Kidogo ukijuacho ni kile kinacho pikwa na waandishi wa magazeti na kuletwa humu. Unakidhalilisha chama makini cha siasa cha CHADEMA pale unapo kilinganisha na ODM! Kwa hiyo basi, simama kwenya mada yako pasipo kukishusha hadhi Chadema.
   
 7. T

  Twaa Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kamanda sipo nje ya mada ila ukweli utabaki kua ukweli!
  Katiba ya kenya imeletwa na mchango mkubwa wa wanaODM na hata ktk kuitetea wanaODM wameitetea sana katiba iliyoandikwa na kukubalika kua katiba ya kenya!!!! Mambo ya ufisadi ODM inaongoza kwa kupiga vita ufisadi nchini kenya, je CDM hawapo hivyo? ODM wanaongoza kwa kutetea umma wa wakenya nje na ndani ya bunge la kenya je CDM hawapo hivyo??
  ODM ndio wa kwanza kugusia suala la katiba nchini kenya je CDM Hawakufanya hivyo! Hapa tanzania? tuache unafiki wa kuchangia maada!!!!
   
Loading...