Wanahitajika Waandishi na Waigizaji wenye Akili kwa ajili ya kutengeneza Movie Za Maana.

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Mwaka juzi nlimtembelea jamaa yangu mmoja tulisoma naye primary.alisisitiza sana nimtembelee kwake nikashinde siku nzima. Basi nikaenda jumamosi.ameoa ana watoto wawili. Tukiwa sebulen watoto wake wakaja wakawa wamekaa.jamaa akaamua kuwawekea movie. Aliweka bongo movie.

Nlijisikia vibaya sana na aibu kubwa.kuwa jamaa ameona na mimi ni mtoto?mbaya zaidi akawa anaangalia halaf ananisimulia. Nlivumilia kwa dk 20 baadaye nikamwomba tukakae nje.akanambia si tumalizie movie kwanza. Uzalendo ukanishinda nikasema hizo ni movie za watoto mi huwa siangalii.

Nlisikitika ile movie walikuwa wanatuchukulia sisi wote ni wapuuzi kama wao. Haina uhalisia hata kidogo. Imejaa uongo mwanzo mwisho, maneno yanayotumika na vitendo ni vya kitoto kabisa. Aliyeigiza amezaliwa na kukulia kijijini amevaa wigi la gharama,amebandika kucha na unamwona tu ni uongo.

Kijana mmoja aliigiza kama maskin amevaa saa ya gharama,ukimwangalia anasema anasukuma mkokoteni nywele kapaka dawa na anaongea kiminato. Nikajua yule kijana atapata zali tu atakuwa tajiri.ni kweli ikawa hivyo. Akawa na wapambe 10 akitaka washa sigara mmoja anatia kiberiti,mwingine anatoa sigara.wa tatu ndo anampachika sigara mdomoni.totally foolishness.

Nikawaza sana.nikakumbuka nimewah sikia kuna movie jambazi kaingia ndani ya nyumba anavua viatu asichafue kapeti, nikakumbuka movie flan nasikia kuna jini akitaka vuka barabara anaangalia kulia na kushoto anavuka wakat huo huo anadai anayemwona ni mtu mmoja tu lakin njian akipita watu wanamtizama kwa kumshangaa kuwa ni muigizaji.

Nikawaza hizi sinema hakuna watu wenye akil wa kuandika na kuongoza?hakuna watu wenye akili wa kuandika? Wallaha nakwambia ukiniweka hapo sumu na bongo movie ukanambia nichague kimoja mi ntachagua ninywe sumu nife mara moja.kuliko kuangalia bongo movie kufa kwa mateso.

Niliacha kupanda bus flan miaka ya 2000s sabab walikuwa na tabia ya kutupa adhabu abiria ya kuangalia bongo movie njia nzima.nikawaza nauli nalipa na bado naadhibiwa nikaacha kupanda hilo bus.

Waigizaji weng wa bongo movie ukiwachek upeo wa kufikiri ni mdogo sana. Wengi hawana akili. Ashakum si matusi.wanaweza kuwa wazuri au wasafi lakin upstairs hamna kitu kabisa weupe.


Walikuwepo akina muogo mchungu zaman,akina sumbi na bocha, kipindi mambo hayo na kaole.maskin sijui wakapatwa na nini....wamebak wapuuzi sana ambao inawezekana kabisa wakawa wanapata pesa kwa kupitia wapuuzi wenzao.kwangu nlishapiga marufuku kuangalia bongo na nigerian movies.
 
Back
Top Bottom