Wanahitajika vijana wa Kike na Kiume 23 kwa ajili ya kazi ya Data entry

brobiz

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
585
775
hii fursa nimeikuta whatsapp group kama utaipenda fanya kuomba na ww mdau
TANGAZO:

Wanahitajika vijana wa Kike na Kiume 23 kwa ajili ya kazi ya Data entry katika Pilot Project ya ku-test mfumo wetu wa kukusanya taarifa za kitafiti kwa mfumo wa Computer katika Kampuni ya Doube A Company Limited, itakayodumu kwa muda wa miezi 9.

Project hii itakayofanyika Jijini Dar es Salaam itaanza kuanzia mwezi November mwaka huu mpaka mwezi July mwaka 2019.

SIFA ZA MUOMBAJI:

1.Elimu kuanzia Kidato cha nne na kuendelea.
2.Awe na umri kuanzia miaka 21 mpaka 35.
3.Awe na uwezo wa matumizi ya Msingi ya Computer(Basic Computer Skills)
4.Asiwe mwanafunzi au mwajiriwa wa mahali popote.
5.Awe na uwezo wa kufanya kazi bila usimamizi wa moja kwa moja.
6.Awe mkazi wa Dar es Salaam.

MSHAHARA:
Tsh 430, 000 kwa mwezi, na posho ya usafiri na chakula ya Tsh 8,500 kwa siku.

Kwa mwenye vigezo tafadhali tuma maombi yako kwa njia ya email ya asigwa@gmail.com ukiambatanisha Barua ya maombi pamoja na CV kabla ya tarehe 28 September mwaka huu 2018.

ANGALIZO:
Usitume nakala za vyeti vyako, kwani usahili utafanyika kwa awamu mbili.
Uwasilishwaji wa nakala za vyeti utafanyika wakati wa usahili tu.
 
Hapa naona sio tu watu kuliwa, inaweza kuwa ni njia ya kupata mawasiliano ya watu nikimaanisha namba za simu na barua pepe (email address) ili zitumike kwa marketing, wengine wanauza hizo taarifa.

Iweje shirika watumie email ya gmail? Kama ni wa kiwango hicho tayari wameshavuta ndugu na jamaa zao.

Sishauri sana watu kujiingiza kwenye mitego ya aina hii kabla ya kufanya utafiti na kujiridhisha.

Nna kila sababu ya kuamini iko namna.
 
Wakiuza taarifa watakamatwa tu... Wezi wa mtandao hawajawahi kuishinda serikali
 
:oops::oops::oops::oops::oops: Tunanyanyaswa kwenya dala dala mpaka humu, dooohh!!! Haya bhana ombeni
 
hii fursa nimeikuta whatsapp group kama utaipenda fanya kuomba na ww mdau
TANGAZO:

Wanahitajika vijana wa Kike na Kiume 23 kwa ajili ya kazi ya Data entry katika Pilot Project ya ku-test mfumo wetu wa kukusanya taarifa za kitafiti kwa mfumo wa Computer katika Kampuni ya Doube A Company Limited, itakayodumu kwa muda wa miezi 9.

Project hii itakayofanyika Jijini Dar es Salaam itaanza kuanzia mwezi November mwaka huu mpaka mwezi July mwaka 2019.

SIFA ZA MUOMBAJI:

1.Elimu kuanzia Kidato cha nne na kuendelea.
2.Awe na umri kuanzia miaka 21 mpaka 35.
3.Awe na uwezo wa matumizi ya Msingi ya Computer(Basic Computer Skills)
4.Asiwe mwanafunzi au mwajiriwa wa mahali popote.
5.Awe na uwezo wa kufanya kazi bila usimamizi wa moja kwa moja.
6.Awe mkazi wa Dar es Salaam.

MSHAHARA:
Tsh 430, 000 kwa mwezi, na posho ya usafiri na chakula ya Tsh 8,500 kwa siku.

Kwa mwenye vigezo tafadhali tuma maombi yako kwa njia ya email ya asigwa@gmail.com ukiambatanisha Barua ya maombi pamoja na CV kabla ya tarehe 28 September mwaka huu 2018.

ANGALIZO:
Usitume nakala za vyeti vyako, kwani usahili utafanyika kwa awamu mbili.
Uwasilishwaji wa nakala za vyeti utafanyika wakati wa usahili tu.

Kwa wale wanaopenda kuajiriwa changamkieni hapo...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom