Wanaharakati Wazidi kuibana Serikali-SIKIKA Yatoa Tamko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati Wazidi kuibana Serikali-SIKIKA Yatoa Tamko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsangulaKG, Jul 5, 2012.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  SIKIKA ni shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza shughuli mbali mbali zenye lengo la kuchochea upatikanaji wa huduma za afya zenye uwiano, viwango na ubora unaokubalika, gharama nafuu na zilizo endelevu. SIKIKA imekuwa mstari wa mbele kufanya tafiti katika sekta ya afya na kuhimiza utekelezaji wa sera, uwajibikaji na upatikanaji wa huduma bora nchini Tanzania.

  Kama neno ‘afya' lilivyo tafsiriwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Mwaka 1948, sera ya afya ya Taifa (Tanzania Health Policy) ya mwaka 2007, nayo pia inatambua ‘afya' kama hali ya ukamilifu wa binadamu kiakili, kimwili, kijamii na siyo tu kutokuwepo kwa maradhi.

  Afya bora ni mhimili wa maendeleo ya mtu binafsi, familia na taifa zima kwa ujumla hasa katika harakati za kuondoa umasikini uliokithiri katika taifa letu.

  Katika nchi yetu, mfumo wa utoaji huduma katika sekta ya afya umegawanyika katika ngazi tatu yaani ngazi ya afya ya msingi kama vile zahanati na vituo vya afya, ngazi ya pili kama vile hospitali za wilaya au mikoa na ngazi ya hospitali za rufaa kama vile hospitali ya Muhimbili, Mbeya, Bugando, KCMC na hospitali maalumu kama taasisi ya magonjwa ya kansa ya Ocean Road au hospitali ya magonjwa ya akili ya Milembe.

  Hospitali hizi za rufaa hushughulika na magonjwa ambayo ama yameshindikana katika hospitali za ngazi za chini au wataalamu waliopo katika ngazi hizo na vifaa vilivyopo haviwezi kutoa huduma stahili kwa magonjwa hayo.

  Hivyo basi, iwapo kutakuwa na matatizo yanayoathiri utendaji wao wa kazi wa kila siku na kwa kuwa wagonjwa walioletwa katika hospitali hizi za rufaa hawawezi kurudishwa kule walikotoka (ngazi za chini), wagonjwa hawa wasio na hatia ndiyo waumiao kutokana na matatizo hayo.

  Bofya Link hii kwa taarifa kamili: http://www.sikika.or.tz/sw/publications/read.php?uid=235


  Huu ni Mfululizo wa Wanaharakati kutoa matamko yao ya kuibana Serikali itatue Mgogoro na Madaktari kwa amani. Tamko hili la 10 pages, limetoa takwimu za kuridhisha na kuonyesha udhaifu mkubwa wa Serikali.
   
 2. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hivi mnadhani JK anasoma mambo haya? Amwachie nani safari za kimataifa?
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wanaharakati wanaibana serikali kivipi?
   
 4. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Nchi hii haiihitaji uanaharakati wala uanahabari... Inahitaji wananchi wote wajitambue na kusema sasa basi na kuingia barabarani kuidai nchi yao... tatizo tuna viazi vingi sana nchi hii
   
 5. m

  mob JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,028
  Likes Received: 511
  Trophy Points: 280
  kimsingi kwa safari yake aliyoifanya hivi karibuni kwenda burundi na rwanda unadhani hizo fedha zingelitumika vizuri si vingeliweza kununua hata CT scan moja iwekwe pale Muhimbili?
  tatizo sisi hatuna vipaumbele kabisa
   
 6. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nimekupata mkuu, ndiyo maana rais aliahirisha safari ya kikazi ili akasaini kitabu
  cha maombolezo na kuuza sura kwenye msiba wa Kanumba. Pia viongozi wote wakuu
  wa serikali kwenda kujazana msibani na kuuza sura ili warudishe umaarufu wao
  ulioanza kupotea! Ni kweli hatuna vipaumbele!
   
 7. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Acha Uzembe mkuu soma chapisho kwanza!
   
 8. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Serekali inahusika kwenye UNYAMA aliofanyiwa DR Uli?Tuiachie Vyombo husika kushughulikia.

  "LAKINI TUJIULIZE"

  Serekali imefaidi kutokana na UNYAMA aliofanyiwa DR Uli? UNYAMA aliofanyiwa DR Uli, Umebadilisha kabisa Upepo wa Mgomo wa Ma Dr kwa faida ya serekali? Ni rahisi kumpata Mrithi wa DR Uli baada ya UNYAMA aliofanyiwa? Watu na Asasi mbalimbali zitajenga utiifu kwa serekali kama jibu la UNYAMA kwa DR Uli? UNYAMA kwa Dr Uli, umewapa baadhi ya viongozi wa serekali na Wabunge kujiamini na kuwa sasa IMEWEZEKANA? UNYAMA kwa Dr Uli umekuwa namna Mpya ya UTATUZI WA MATATIZO YA JAMII YA WATANZANIA?


  SEREKALI, BUNGE, MAHAKAMA NA WATU WOTE WENYE UTU TIMAMU. LAZIMA WAKEMEE, "UNYAMA" KAMA MSINGI WA UTATUZI WA MATATIZO KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. ISISITIZWE KUWA KAMWE UNYAMA HAUWEZI KUPINDUA UTU NA NCHI IKABAKI MAHALI SAHIHI PA KUISHI KWANI ITAKUWA SAWA NA KUJENGA KINACHOTOKEA SYRIA NDANI YA TANZANIA.
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Dhaifu bhana
   
 10. m

  movichboy JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 212
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Huyo mkurugenzi wa Sikika hana uanaharakati na wala uzalendo wowote, ni mbinafsi na anapenda sana kutumia migongo ya watu kujinufaisha, sana sana ni kutumia tu fursa ya mgogoro wa madaktari kuendelea kutangaza jina la asasi yake ili azidi kujinufaisha kwa pesa za wafadhili. Huyu bwana namfahamu vizuri anaitwa Irenei Kiria kabla ya sikika kuanza alikuwa anafanya kazi za kujitolea pale Amref mwananyamala za uelimishaji wa kupunguza maambukizi ya VVU kwa vijana. Mwaka 1999 alipewa fursa na vijana kwenda kusimamia network ya Kinondoni Cluster kama coordinator ambayo ilikuwa inafadhiliwa na Family Health International FHI wakati huo. Matokeo yake akauwa huo mtandao kwa ubadhilifu ikiwa ni pamoja na kuondoka na pikipiki mpya ya mradi ambayo baadaye alikuja akaiuza na kununua gari yake ya kwanza aina ya Toyota corola.

  Baadaye alirudikufanya kazi pale AMREF mwananyamala kama afisa vijana tena kwa kuwekewa kifua na mzungu mmoja alikuwa pale anaitwa Dr. Vero. Wakati anarudi pale kwenye miaka ya 2000, center ya AMREF ilikuwa very strong kwa kuwa na program nyingi sana za vijana za michezo na program za elimu. Huyu jamaa kwa roho yake mbaya alianzisha mgogoro mkubwa sana na vijana na matokeo yake akauwa shughuli za pale na kuwarubuni vijana wengine watatu kuachana na kazi za Center na kwenda kuanzisha shirika la Sikika wakati huyo lilikuwa linaitwa Youth Action Volunteers (YAV) na katiba na muundo wa asasi hiyo ilitokana na kucopy na kupaste katiba ya Center ya vijana ya mwananyamala.

  Shirika la YAV walianzisha kwa msaada wa mama mmoja alikuwa anaitwa mama Kiwia yeye ni Mkurugenzi wa asasi ya Kimara Peer Educators ambaye alikuwa anafahamiana na mama mmoja anaitwa Eliada Maneno wakati huo alikuwa Country Representative wa shirika la kimataifa la misaada sa Southern Africa AIDS Training ambapo Kiria aliunganishwa kwa mama huyo na kupewa grants ya zaidi ya Milioni 35 wakati huo. Wakati wa kufanyiwa assessment ya kupewa pesa hizo, Kiria alijifanya yeye ni mlezi wa shirika la vijana hao kwani umri wake ulikuwa mkubwa na walibadilisha stoo ya nyumba ya national housing aliyokuwa amepangwa pale kinondoni Kasana street na kuitengeneza ionekane kama ofisi wakati wanacheza sanaa ya kupata pesa hizo.

  Ki msingi wafadhili walilidhia kutoa pesa hiyo kwa msaada mkubwa wa Mama Kiwia na Mama Maneno lakini ilikuwa ni kwa makubaliano ya kutoa cha juu kwa akina mama hao. Kwa mama kiwia ilikuwa ni kwa sharti la shirika kutumia nyumba ya mama huyo iliyopo kijitonyama kwa kupanga kama ofisi na kulipwa bei ya juu kitu ambacho kilifanyika na kwa Mama Maneno sina hakika makubaliano yalikuwaje. Mwaka 2001 pesa hiyo ilitoka lakini Kiria aliwazunguka vijana wale watatu na wengine wawili ambao alipewa na mama Kiwia wakati wa kuanzisha asasi, Kwanza alifungua akaunt kwa kujiweka yeye na mdogo wake wa kike aitwaye Mary Boniface Kiria kama signatories wa akaunti ili afuje pesa vizuri, na pia alimweka mke wake anayeitwa Jaquiline Matoro kuwa board member kinyume na sheria na taratibu.

  Baada ya shirika kukua kwa msaada mkubwa wa wenzake, alikorofishana na Mama Kiwia na kuamisha ofisi kutoka kwa mama huyo kisha kuamia makumbusho karibu na chaga bite. Akatumia pesa za asasi kwenda kujisomesha degree ya sociaology pale UDSM na alipomaliza na kurudi ofisini alikuta wenzie wameendelea kujiestablish vizuri akaona watakuwa na nguvu ya umiliki akaatengeneza mpango mzito sana wa KUWAFUKUZA wenzie ili aweze kumiliki vizuri asasi kama mali yake na baada ya kufaninikiwa alihamishia ofisi pale kinondoni ada estate. Baadaye alifanya lobbying kwa msaada wa akina Jonh Ulanga, Rakesh na wengine na kupata funds ya strategic plan ambayo zinampa kiburi mpaka leo.

  Jamaa ni mnyanyasaji mkubwa, staff turn over kwenye organization yake ipo juu sana tangu ameanzisha na anapenda sana kuwatumia wenzie kupanda juu. Aliwahi kupata kashfa mbaya sana ya lutembea na shemeji yake wakati mkewe ameenda masomoni ikiwa ni pamoja na kumpa uja uzito.

  Huyu bwana hana sifa ya kuwatetea madaktari wakati yeye mwenyewe ana matatizo.
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Jk ni mtu wa kazi syo mtu wa majungu kama ambavyo hizi NGOs zinavyotumiwa na wanasiasa kulitumbukiza taifa katika vurugu zisizo na maana.
   
 12. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,097
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja.
   
 13. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wabunge wameshindwa kuibana serikali ndio iwe wanaharakati
   
 14. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #14
  Jul 5, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Mkuu hii ni more personal au mna ugomvi naye? Maana Statement ni ya Sikika siyo ya Irenei!But umemake point zako!

   
 15. t

  theROOM JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Hawa ndivyo walivyo, wana majibu mepesi kwa maswali magumu...hawasomagi hata kidogo...Lakini yana mwisho haya yote...
   
Loading...