Wanaharakati wataka JK abadili uamuzi kuhusu EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati wataka JK abadili uamuzi kuhusu EPA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Aug 28, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,137
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Wanaharakati wataka JK abadili uamuzi kuhusu EPA


  Na Gaudence Massati

  MTANDAO wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea Usawa wa Jinsia, Haki za Binadamu na Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi (FEMACT) umemtaka Rais Jakaya Kikwete kubadilisha uamuzi wake wa kuwasamehe mafisadi wa sh. bilioni 133 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), badala yake watajwe na kushtakiwa.

  Aidha FEMACT imesema, kuweka fedha zinazorudishwa katika Benki ya Rasilimali (TIB) ni hatari kwa kuwa zinaweza zisiwafikie walengwa, hivyo ni vyema kazi hiyo lingeachiwa Bunge kwa kuwa ndicho chombo chenye mamlaka ya kuidhinisha fedha za umma na kufuatilia matumizi yake.

  Hayo yamo kwenye taarifa ya mtandao huo unaoundwa na mashirika yapatayo 50, iliyosainiwa na Mratibu wake, Bibi Usu Mallya iliyotolewa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

  FEMACT ilieleza kupitia taarifa hiyo kuwa mafisadi wa EPA ni watu hatari waliofilisi nchi, hivyo ni lazima watajwe hadharani na kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

  "Tunaona kuwa kitendo cha mafisadi hao kusamehewa kabla ya sheria kuchukua mkondo wake kitafifisha vita dhidi ya ufisadi ikiwa ni pamoja na wizi wa mali ya umma na hivyo kuchafua heshima ya serikali na taifa kwa ujumla,"ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

  Mashirika ya mtandao huo yamesisitiza, mahali popote duniani ambapo vita dhidi ya rushwa na wizi wa mali ya umma vimefanikiwa ni pale penye uwazi na uwajibikaji bila kuogopa au kumuonea haya mtuhumiwa kutokana na wadhifa au nafasi yake katika jamii.

  "Tunahofu kwamba kama mafisadi wa EPA hawatashtakiwa huenda ikawa ni mwanzo wa nchi yetu kujenga matabaka ya wazi ya watu walio juu ya sheria na wengine walio chini ya sheria,"alisisitiza taarifa hiyo.

  Ilisema, wakati wa uhai wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuonya kwamba kuwaonea huruma watu dhalimu hujenga Taifa lenye tabaka jambo ambalo ni hatari kwa amani ya Taifa.

  Taarifa hiyo iliongeza kuwa sh. bilioni 133 ni fedha nyingi na kwamba kwa kutafakari fedha hizo zingeweza kuepusha wanawake zaidi ya milioni 13 wanaokufa wakati wa kujifungua kutokana na kukosa sh.10,000 tu ya kununulia vifaa muhimu.

  Pia FEMACT ilisema fedha hizo zingetosheleza kujenga mabweni mengi kwa shule za sekondari za serikali na kuepusha adha wanazopata wanafunzi hasa wasichana kutokana na kukosekana kwa mabweni mashuleni.

  Wakitahadhalisha kuhusu fedha hizo kuwekwa TIB, FEMACT ilisema kuwa iwapo mafisadi waliweza kupenya na kuiba kwenye akaunti ya EPA iliyokuwa kwenye chombo nyeti kama Benki Kuu, hawatashindwa kuingia TIB na kuiba tena ili kukidhi matakwa yao.

  Akilihutubia Bunge hivi karibuni Rais Kikwete alisema kuwa aliwapa muda hadi Oktoba 31 mwaka huu, wahusika wote wa wizi huo wawe wamerejesha fedha hizo, kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria na kwamba hadi sasa kiasi cha sh. bilioni 53 zimerejeshwa.

  Kauli hiyo ya Rais imezua mjadala mkali miongoni mwa makundi ya jamii, huku wengi wao wakionesha kutoridhishwa nayo na badala yake wakitaka mafisadi hao watajwe hadharani na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Hili ndilo tatizo la kuwa na rais muhuni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Huo ndio uhandsome anaonesha, sijui tutakula uzuri wake? Maana kuna wapumbavu walishabikia sana wakati wa uchaguzi mara ooh! handsome, mara kijana, sasa ndo tunavuna tulichopanda. Ujinga mtupu.
   
Loading...