Wanaharakati wapeleke ombi Mahakama Kuu kuizuia tume ya polisi kuhusu Dr Ulimboka isifanye kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati wapeleke ombi Mahakama Kuu kuizuia tume ya polisi kuhusu Dr Ulimboka isifanye kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jun 30, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi:

  Nimekuwa kwa muda mrefu nafuatilia sasaka hili la Dr Ulimboka na kuundwa kwa Tume ya polisi kulichunguza. Wengi wanaona tume hii haitafanya haki kwani polisi, au vyombo vingine vya dola vimekuwa vikitajwa kuhusika. Naona Polisi wanang'ang'ania kuendelea na tume yao.

  Mie nauliza - hivi hakuna uwezekano kwa wananchi, kupitia vyama vya wanaharakati kupeleka ombi Mahakama Kuu kuizuia tume hiyo ya mapolisi isifanyekazi na badala yake iundweb tume nyingine huru?

  Mimi nadhani Mahakama Kuu, kama chombo cha kusimamia haki inaweza kabisa kutoa zuio hilo na hapo hapo ikaunda tume yake huru.

  Mnasemaje wenzangu?
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,775
  Likes Received: 6,108
  Trophy Points: 280
  Mh! Hivi muda mrefu urefu wake ni upi? Otherwsie, kwa hayo mengine una hoja.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mhhh Mkuu Zak.

  Nadhani hili lawezekana. Hatua yoyote inayohimiza haki ionekane kutendeka ni hatua nzuri. Kuna ule msemo maarufu wa kisheria -- kwamba si tu haki itendeke, bali pia iwe inaonekana ikitendeka. (Justice must not only be done, but must also be seen to be done.)

  Wanaharakati nendeni mahakamani. Tume ya Polisi kamwe haionyeshi kama haki inatendeka.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tena wapeleke haraka sana ombi la zuio hilo. My hunches tell me that they can get it. Hii issue iko clear sana, polisi wanajitahidi kulifunika ukweli usipatikane.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nami pia naliona suala hilo liko wazi kabisa. Waende mahakamani kuzuia manjagu hawa wasijitie kufanya kazi za kitaalamu.
   
 6. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,775
  Likes Received: 6,108
  Trophy Points: 280
  Mkuu mahakama zipi hizo? Za Tanzania au nyingine? Wanaweza wakafanya hivyo lakini kwa vyovyote vile POLISI watachomoa tu. Kwa sheria (Katiba) zetu Polisi ndio wenye mamlaka ya kupeleleza, kukamata, na hatimaye kufungulia mashitaka aina hizo za makosa. Amini, usiamini, hiyo ndiyo itakuwa rule ya Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Mtukufu Jaji X.

  Hapa tatizo ni sheria na Katiba. Hivyo basi kwa "uzoefu" tulioupata katika issue hii ya Ulimboka, Zombe, kule Arusha, Tarime, Tabora (kwa Mh. Magdalena Sakaya), n.k., pengine kuna haja ya kutamaza upya sheria na Katiba ili kuizuia Polisi kujiingiza katika suala ambalo moja kwa moja wanatuhumiwa kuhusika.

  Leo hii baadhi ya polisi wamejigeuza majambazi halafu ndio hao hao kutoka kituo kile kile kesho yake wanakuja kupeleleza tukio - kiroja hicho!
   
Loading...