Wanaharakati wamfagilia, Dk. Slaa, Mwakyembe na Selelii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati wamfagilia, Dk. Slaa, Mwakyembe na Selelii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fredrick Sanga, Feb 12, 2011.

 1. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wanaharakati wamfagilia, Dk. Slaa, Mwakyembe na Selelii

  Na Richard Makore

  11th February 2011  [​IMG]
  Mchambuzi wa masuala ya kijamii na kisiasa nchini, Jenerali Ulimwengu (katikati),Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Imelda Urio (kulia), mmoja wa waandaaji wa ripoti ya utendaji kazi wa Bunge la 9 kuanzia 2005-2010, Deusi Kibamba wakionyesah ripoti hiyo katika uzinduzi wake.  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wanaharakati nchini wameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutunga kanuni zitakazowabana wabunge washiriki kikamilifu katika shughuli za kila siku.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Wamesema baadhi ya wabunge hawahudhurii wala kushiriki kwenye mijadala wakati wakiendelea kupata mishara minono, marupurupu na posho za kila siku.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kadhalika, wanaharakati hao wamewapongeza baadhi ya wabunge waliokuwa kawenye Bunge la mwaka 2005/ 2010 akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Wilibrod Slaa, Lucas Selelii wa Nzega (CCM) na Dk.Harrison Mwakyembe Kyela kupitia (CCM) kwa jinsi ambavyo walitoa michango yao ambayo ilisaidia kuboresha utendaji wa chombo hicho.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mwenyekiti wa jopo la uangalizi wa masuala ya Bunge kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Deus Kibamba aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaamwakati wa uzinduzi wa ripoti ya utendaji wa Bunge lililopita kwa kipindi cha miaka mitano kati ya mwaka 2005/2010.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika ripoti hiyo, Kibamba alisema wabunge waliokuwa katika Bunge lililopita hawakuhudhuria vikoa vya Bunge kwa kiwango kinachoridhisha na kuwawakilisha wananchi kwenye mijadala.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema katika hali ya kushangaza unapofika wakati wa kujiongezea mishahara wabunge wote wanakuwa kitu kimoja bila kujali wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ama wale wanaotoka vyama vya upinzani.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha, alisema wabunge wa Bunge lililopita walikuwa hawahudhurii vikao vya Bunge kwa kiwango kinachotakiwa na badala yake walikuwa mstari wa mbele kutunga sheria ambayo iliwawezesha kujiongezea mishahara, kuanzisha fedha za mfuko wa jimbo ambao alisema hauwasaidii wananchi wa kawaida.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa upande wake, Mwandishi wa habari mkongwe hapa nchin amabye pia ni mwanaharakati, Generali Ulimwengu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo, alisema wabunge 70 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawana kazi yoyote ya kufanya ingawa wanalipwa fedha nyingi kama mishahara, posho na marupurupu.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alitaja aina ya wabunge ambao hawana kazi yoyote ndani ya Bunge kuwa ni pamoja na wanaoteuliwa na rais, mawaziri na wanaoshikilia nafasi za wakuu wa mikoa.[/FONT]  CHANZO: NIPASHE

  Serious people to be concidered 2015, Sio wanaolala Bungeni :msela:
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Selelii ameamua kufa na tai yake shingoni.
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Amekwenda na heshima yake, anaweza kuibukia kwingine, Aliweza Mzee Mwinyi, Seleli je?:clap2:
   
Loading...