Wanaharakati waandamane kumshinikiza Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati waandamane kumshinikiza Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 25, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,499
  Likes Received: 6,856
  Trophy Points: 280
  Sielewi kwanini wanaharakati wanataka kuandamana kulilalamikia Bunge kuhusu suala la Richmond. Hadi hivi sasa Bunge na wabunge wamefanya kazi yao vizuri na kwa umahiri mkubwa. Wameenda hadi pale ambapo kimadaraka wamefikia mwisho wao. Sehemu inayofuatia ni sehemu ya Rais.

  Ni sawasawa watu wanaofanya kazi kwa kupokezana; unalima kuanzia hapa hadi pale, halafu wengine wanachukua kuanzia hapa hadi pale hadi shamba linakwisha. Tangu mwanzo wa sakata la Richmond ni Bunge pekee ambalo limekuwa likilima na kulima weee huku Rais akiangalia pembeni kana kwamba shamba halimhusu!

  Sasa wabunge wamefikia mahali na kusema tumelima tayari na tumejitahidi kulima wewe sasa tulipofikia panahitaji Rais naye alime.

  Kinachonishangaza wanaharakati wanataka wabunge waendelee kulima tu hadi mwisho na wapande, kutia mbolea na kupalilia. Mwisho wake Rais aje avune na kupewa sifa jinsi shamba lilivyopendeza. Halatu atapita na kutaka kuonekana jinsi gani alisaidia kulima!!

  Hivyo, maandamano dhidi ya Bunge na wabunge wapiganaji hayana maana kwani hadi hivi sasa hayajaangalia ukweli. Ukweli ni kwamba Bunge limefanya kazi yake na wanastahili maandamano ya kupongezwa. Anayehitaji kushinikizwa ni Rais kwani Bunge limemuachia kipande chake cha kulima.

  Kipande hicho:
  a. Kumuwajibisha Dr. Hosea wa PCCB
  b. Kuhakikisha bilioni 30 walizopakuliwa Dowans/ Richmond zinarudishwa
  c. Kutaifisha mitambo ya Dowans
  d. Kuwawajibisha wengine ambao ameachiwa na Bunge kuwawajibisha
  e. Kuliomba msamaha taifa kwa uzembe uliotokea ndani ya serikali yake na kuwapotezea muda wananchi.

  Hizo ndizo sababu kiasi za kufanya maandamano; nje ya hapo ni kutaka kuandamana ili waoneshwe mwanasesere!
   
 2. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  Mhh
  Katika yote hayo mzee MM cha rahisi ni kipengele E . cha maajabu hicho kipengele ni kigumu zaidi kwa wanasiasasa wote duniani.

  hapa tunabaki vingine vi 4. hivi wanamaehsabu bado wanafanya calcutaion ku PROVE wataalamu. Hesabu ngumu si wote tunajua if x= innocent ,y= ignorant z= guilty
  where y= tanzanian calculate the value of x and y.

  Kweli hili swali wa kulisolve ni mwalimu JK
   
 3. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #3
  Feb 25, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,068
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  wako wapi wakina okiya omtatah wetu..........kila mtu anamsukumia mwenzake kuanzisha maandaano............who dares?
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Inabidi kukubali tu...Miafrika Ndivyo Tul.....
   
 5. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 566
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hapo umenena !Kuna mijitu kazi kushinikiza tu wao hata majina yao hawataji wao akina nani!
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni Katiba ipo very fragmentation na very distortation katika mambo mengi sana na pia kama ulivyosema kuwa JK ndiye anapaswa kumshinikiza maana yeye ndiye mkuu wa mambo yote haya na Hapa ndio tatizo la msingi linanzia mzee wangu Mwanakijiji
   
 7. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Rais inajulikana wazi kuwa maamuzi mazito hawezi kuyafanya. Bunge limethubutu kwa kiasi chake hivyo wanaharakati kwa kweli wanahitajika kuwapongeza, lakini pia kuwakumbusha kuwa watu wagetegemea mambo makubwa zaidi kutoka kwao. Kama walijua toka mwanzo kuwa hawana uwezo au mamlaka yao hayaendi zaidi ya hapo walikofikia, kwanini warefushe mjadala kwa zaidi ya miaka miwili ndipo wazimike, tena ghafla kama mshumaa?
  Yafaa wakumbushwe kuwa wao na Rais ni waajiriwa wetu na njia mojawapo ya kufikisha ujumbe huo aidha ni shinikizo kwa njia ya maandamano au kupitia sanduku la kura.
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ingekuwa katika Mataifa mengine kwa suala la Richmond tu serikali iliyopo isingeweza kurudi madarakani na kama kuna mfumo wa vyama dhabiti, Ila kwetu sisi Tanzania, Vyama dhaifu na serikali dhaifu hivyo hivyo na vice versa pia
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,205
  Likes Received: 3,699
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Mzee Mwanakijiji,

  Naomba kukubaliana na mawazo yako kwa asilimia 100 %,lakini lazima nikiri kwamba mimi ni miongoni mwa maelfu ya watanzania tuliokuwa tukifikiri Bunge bado lilikuwa na kazi KUBWA ya kufanya kuhusiana na sakata zima la RICHMOND.

   
 10. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  Msingi wa kwanza wa kuwa na vyama dhaifu ambayo huzaa serikali dhaifu pia ni ukosefu wa elimu ya uraia. Ukosefu huu wa elimu ya uraia huzaa ukosefu wa uzalendo, na ukosefu wa uzalendo huzaa ukosefu wa uthubutu hasa wa mambo yanayodhaniwa kuwa magumu. Yote haya kwa Watanzania ni tatizo ambalo kimsingi hatulioni, na kama tunaliona basi tunashindwa namna ya kulikabili kwani tumeshazaa umimi/ubinafsi(mjukuu wa elimu ya uraia).
   
 11. Ndanda to Lomwe

  Ndanda to Lomwe Member

  #11
  Feb 25, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MM, ni kama ulikuwa akilini kwangu,mimi nimejiuliza sana kuhusu hawa wana harakati uelewa wao wa hayo mambo wanayotakiwa kuyapigania,Bunge limefanya sana kazi yake tena nzuri sana na ya kuigwa katika jamii yetu na hapa lazima tumpongeze Mh mzee 6 kwa ujasiri wake wa kusimamia kile ambacho anakiamini,tatizo letu sisi watanzania tunapenda sana kufanyiwa,kwanini tusiamke tukafanya wenyewe?Haki yetu hakuna atakaye tuletea mezani,lazima tuidai wenyewe kwa maandamano na kwenye Balot BOX.

  USHAURI KWA WANA HARAKATI NA VIONGOZI WA UPINZANI.

  Tuongozeni kishinikiza serikali kutekeleza maazimio ya bunge na sio kuandamana kulipinga bunge.
   
 12. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #12
  Feb 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,252
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mkulu nimekugongea thenksi.
  Points kwa mwanasiasa mkweli katika harakati za kutaka nafasi,aziingize na kuzifanyia kazi.
  Ila wa tz tunapenda vyepesi vyepesi muno.
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Feb 25, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,530
  Likes Received: 2,365
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kama JK anaogopa maandamano, manake atatoa his magic smile and fool and joke about everything! Hapa uzalendo unahitajika. Ajitoe great thinker mmoja (manake Zitto naona ndo basi tena), JF yoote tum-support na ndo awe catalyst. ( I am even upset with myself for not doing anything.....!)
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,626
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  Watu watafanya maandamao lakini no any action will be taken...siamini
  Kawaida ni kama mazoea ..kwetu kuko shwari kila kitu tambarareeeeee
   
 15. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #15
  Feb 25, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mpaka leo haujui ni kwanini hawezi kumwajibisha Hosea?
   
 16. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #16
  Feb 25, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uanaharakati nchini Tanzania ni aina fulani ya ajira ya kujipatia ruzuku na misaada kutoka nje kwa ajili ya kujikimu. Sidhani kwamba wana nia hasa ya kuwa 'Wanaharakati' wa kweli.
   
 17. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #17
  Feb 25, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,373
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  "miafrika ndivyo tulivyo"

  Na sasa mambo ndo hayo yameiva, JK ndo huyo anaingia kumalizia ngwe yake ya mwisho. Ili mrithi wake naye aje aseme "mwacheni mzee wetu apumzike"
   
 18. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #18
  Feb 25, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  Waandamane kwa lipi hasa,
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Feb 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,499
  Likes Received: 6,856
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu akajiuzulu, baraza la mawaziri likavunjika, uchunguzi ukafunua siri za hiyo Richmond.. kilichobakia niicha Rais...
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Feb 25, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,499
  Likes Received: 6,856
  Trophy Points: 280
  ukisoma taratibu nilichoandika kinaweza kuingia kichwani kujua ni kipi hasa waandamane kwacho.
   
Loading...