Mracho Ngongoti
Senior Member
- Apr 11, 2012
- 133
- 84
Tuliporuhusu shetani awe MHISANI wetu, MFADHILI wetu, MSHAURI wetu na MWEKEZAJI wetu matokeo ni kama yanavyoonekana! Hizi ni rasharasha tu MVUA haijanyesha. Sehemu ya MUNGU akae MUNGU na si mzungu!
wanaharakati wanatumia mabilioni kwenye warsha na makongamano kwanini wasitumie fedha hizo wanazopata kwa wafadhili kuchangia kuboresha huduma za afya kama kweli ni wazalendo wa kweli. Mimi nipo bongo na ni mhanga wa mgomo wa madaktari
umezungumza hoja ya msingi kabisa,kwa mgomo huu wa hawa wauwaji hawana tofauti na vikundi vyote vya kigaidi ulimwengumi kwani hutumia hujuma kwa kuripua mabomu na kuuwa wananchi wasio na hatia ili waishinikize serikali kukubali matakwa yao!
na hawa hutumia hujuma kwa kuuwa wagonjwa!
Meneja na sio director wa tanapa analipwa tsh 4m daktari kulipwa sh 3.5 kuna tatizo gani?
Osama aliua raia wa marekani ili kushinikiza marekani itoke katika ardhi za kiislamu.....madaktari wanaua wagonjwa wakidai mshahara wa milioni tatu kwa daktari anayeanza kazi leo.....ILA NA NYIE BUNGE MNACHOCHOEA KWA KUJIONGEZEA VIPATO ....!
mnyampaa now you are talking......na pia tukichukua definition ya TERRORISM/UGAIDI ni hali ya kuua,kuogofya,kuharibu wasio na hatia ili kupata malengo fulani ya ki-maslahi au kisiasa kutoka serikalini ama eneo fulani!
Ulimsikia uamsho akimwambia daktari agome?
Wacha wewe, huu ni ugaidi na hakuna haki ya kwanza duniani ila haki ya kuishi na madaktari wanafiki wachache wanajifanya wao mungu watu kuwa wanaweza kuwaweka rehani wagonjwa na kutumia maradhi yao kujipatia maslahi yao. Hao malipo yao ni hapa hapa tena hayachukui muda mrefu.