Wanaharakati wa tanzania ni hatari kwa usalama wa nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati wa tanzania ni hatari kwa usalama wa nchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnyampaa, Jun 30, 2012.

 1. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kutokana na mchango wao katika kushawishi na kushabikia mgomo wa madaktari na kuushawishi umma kuamini kuwa vurugu na migomo ndio njia pekee ya kudai maslahi nadiriki kusema kundi hili la jamii ni hatari kama vikundi vya kigaidi. Nielewavyo mimi vikundi hivi vinapaswa kuishia kutoa elimu na kuishauri au kuishawishi serikali au kikundi/taasisi nyinginezo kutimiza wajibu wake na si kuegemea upande mmoja. Kwa hili la mgomo wa madaktari nilitegemea wanaharakati kuwa wa kwanza hata kabla ya mgomo kuishawishi serikali kuboresha huduma za afya na si kudandia mgomo. Ninavyofahamu hali mbaya ya huduma za afya si jambo jipya hivyo walipaswa kuingilia kati kabla ya mgomo. Iwapo wao ni watetezi wa haki za watanzania wasingeshabikia mgomo wa madaktari kwani ni mgomo umechangia watanzania mamilioni kukosa haki zao za msingi kwa wanaharakati kushabikia mgomo na kusahau mateso ya wananchi walio wengi. Wanaharakati wanapaswa kupima kati ya haki ya msingi ya kuishi ya watanzania na maslahi ya kuishi kifahari ya madaktari.
   
 2. k

  kamili JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Huyu haishi Tanzania....
   
 3. majany

  majany JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  kwenye maboresho yajayo ya Jf naomba tuone na location ya mtu.....yaan huyo haielewi kabisa Tanzania wala CCM.....
   
 4. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaharakati wanatumia mabilioni kwenye warsha na makongamano kwanini wasitumie fedha hizo wanazopata kwa wafadhili kuchangia kuboresha huduma za afya kama kweli ni wazalendo wa kweli. Mimi nipo bongo na ni mhanga wa mgomo wa madaktari
   
 5. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,864
  Likes Received: 4,246
  Trophy Points: 280
  Ndg, tueleze unataka kusema nini maana unauma na kupuliza, hata vitabu vitakatifu vinasema watu km nyie ni hatari, weka bayana we ni moto au baridi.
   
 6. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umezungumza hoja ya msingi kabisa,kwa mgomo huu wa hawa wauwaji hawana tofauti na vikundi vyote vya kigaidi ulimwengumi kwani hutumia hujuma kwa kuripua mabomu na kuuwa wananchi wasio na hatia ili waishinikize serikali kukubali matakwa yao!
  na hawa hutumia hujuma kwa kuuwa wagonjwa!
   
 7. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulifaulu vipi comprehension au ufahamu kwenye kiswahili kama unashindwa kuelewa paragraph moja tu. Yawezekana ulihudhuria remedials nyingi sana
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hivi leo ni weekend? No wonder watu mshakunywa naniiiiiiiiii!! Mambo mengi huyajui au umeyasahau!
   
 9. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahaaa. Hapana mkuu ukitaka kuifahamu vizuri shilingi lazima uigeuze upande wa pili. Ukiona upande mmoja wa sarafu lazima ugeuze upande mwingine ujue kama unafanana na ule wa kwanza. Uking'ang'ania upande mmoja huatakuwa tofauti na wamasiasa wanaoongozwa na itikadi za vyama vyao ambao huziabudu na kufungwa nazo hata kama ni mbovu bila kujua kuna itikadi zingine ambazo zaweza kuwa bora zaidi. Ni mtazamo tu usitishike
   
 10. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Do you know what your talking about?is these come from your brain or is the power of money?(nape allowance)...jiuzuru jf kwa nanufaa ya upuuzi wako huna hoja,bali njaa ndoo inakusukuma kumwaga pumba na kujaza servar
   
 11. Mnyampaa

  Mnyampaa JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati... Vipi mboma unakuwa kama wabunge wa CCM.... Shambulia kwa hoja mimi nimetoa hoja na mtazamo wangu tu kama hoja haina ukweli kwanini unapanda jazba?
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni kweli kabisa, hao wanaojidai wanaharakati wote ni magaidi tu, wao badala ya kutetea uhai wa binaadam wao wanachochea madaktari wagime na watu wapoteze uhai wao. Hao ni wa kufunguliwa kesi za uchochezi tu.

  Nasikia wengi wao ni waathirika.
   
 13. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nimekuuliza swali unanajua unacho kiongea?haya unayo yasema ni kweli yanatoka kwenye ubongo wako ama ni nguvu ya wanaokulipa posho kuja kujaza serva?HUJANIJIBU HATA MOJA
  nakuuliza tena,Kati ya serikali,Madaktari na wanaharati ni nani anawajibika kikatiba kuwapa huduma wananchi inayo bora?je unajua katiba ya sasa japo kwa ubovu iliyo nayo inazungumziaje juu ya maandamano?je kipi kitendo cha vurugu walichotumia wanaharakati kwa wananch ama kwa serikali zaidi ya serikali kumuumiza dr ulimboka?Kama unataka tuuonge kwa hoja nijb maswal yangu matano then ntaanzia hapo,ntarudi
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  mnyampaa now you are talking......na pia tukichukua definition ya TERRORISM/UGAIDI ni hali ya kuua,kuogofya,kuharibu wasio na hatia ili kupata malengo fulani ya ki-maslahi au kisiasa kutoka serikalini ama eneo fulani!
   
 15. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MnyampaaKwa hakika hali ilipofikia sasa vikundi vyote (isipokuwa kundi la 'wasokuwa na kundi') si salama kwa usalama wa taifa letu na mustakhbali wake kesho.hata hao wanaoitwa usalama wa nini sijui bado nao si salama.., kuanzia vikundi vya dini sasa vimegeuka kuwa 'magenge' yaliyopo kwa ajili ya kulinda intresti zao ndo maana kipindi kile cha uchaguzi vikazuka vikundi vilivyoleta hoja za kipuuzi za nini sijui ni chaguo la Mungu...,sasa vimekuja vingine na mambo ya sensa..,ukija vikundi vya walinda usalama wa raia huko sina la kusema,wenye macho wanaona.Vikundi vya wanafunzi wa elimu za juu navyo ni moto unaosubiri petroli,vikundi vya wanasi'hasa' ndo usiseme ya igunga, kibaha,kwa kina siowi na mengine mengi yanakuja tutayaona,kundi la mafisadi na wanaowalinda nalo sijui tusemeje! Ukiliona kundi la vijana wasio na ajira ndio machozi yatakutoka, hivyo usitazame ishu ya madaktari ukadhani unavyodhani,tazama jinsi mfumo mzima wa nchi ulivyokwisha kuwa volatile kisha utuambie watu/kundi gani ni salama kwa usalama wa taifa
   
 16. H

  Hansen Nasli JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 881
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Kama kuna watu ni hatar kwa usalama wa nchi ni wanaharakati dunia nzima aman imeshndwa tawala coz ya hawa wapuuzi wenye maslahi binafsi,naombea atokee kichaa awaue watu hawa nawachukia sana
   
 17. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kama mtu hujui maana ya harakati ni bora utulie na usitegemee kuna harakati zipo kwa maslahi ya watawala harakati huwa zipo upande wa wanyonge daima na hapa ieleweke kuna vita kati ya CCM NA SERIKALI YAKE V/S MADAKTARI NA WANANCHI WAKE NA WALA MSIJIDANGANYE KUWA KWA KUWA UDAKTARI NI WITO KWA HIYO HAWAFAI KUPATA HAKI YA KUPATA MASLAH MBONA HAMJAWAFUNGULIA MADUKA YAO NA BEI ELEKEZ KWAO? WANAHARAKATI WATU WOTE TUSIOMTEGEMEA RIDHIWAN TUKO NANYI
   
 18. G

  Godwishes JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Nashawishika kusema usilo lijua ni kama usiku wa giza.WHY?Nakumbuka,niko Chuo,tuligoma mpaka tukarudishwa nyumbani,tatizo lilikuwa ni kushinikiza tusilipe 40% na waongeze meal allowance,lakn nilvyorudi nyumbani na kwenye vyombo vya habari baadhi ya raia walikuwa wanalaani vikali ule mgomo,sana sana 4m6.Ooh mara serikali inawasomesha bure mara unagoma,eti tunataka anasa,starehe,oh mara mtu amefukuzwa alafu ana kompyuta,tv,redio,..mi nlimaliza.Bt cku hazikuwa nying wale 4m6 walipata Admision,na wao wakalianzisha oh maisha yamepanda,cjui stat.allowance iongezwe,na taka taka nyingne.NATAKA KUSEMA NN?Humu kuna layman,hata hawajui nn wanachoongea,na hawajui Dunia inaendaje,yye kwa mtizamo wake&akili yake vimeishia hapo hapo.mf.We unafikiri hawa Madaktari au Wanaharakati ni wendawazimu kama unavyofikiri wakae tu,halafu eti tugome,oh,tuwasapoti watu wagome,oh wagonjwa wafe bila sababu ya msing?Kwa sababu we cyo dr.KAA KIMYA,we cyo mwanaharakat,KAA Kimya.Kwa nn ua..argue kumbe hujui unasema nn?We unadhani ni Kanda gani hapa TZ ambao hawana kinyongo na profshono zao?Tofaut NA HAWA WANASIASA?Na nani ana umuhimu zaid kwenye jamii ukiliganisha na Wata-aluma(laam)&Wanasiasa?Ukisema madr.ni sawa na magaidi...ohh cjui Wanaharakati cjui nn unakosea sana.Unahitaji ujifanyie maombi upate ufunuo,ufunguke ujue tz inavyoliwa na wendawazimu we ukiendelea kuliwa bila kujijua.Tuwauge mkono madr.tuwauge mkono walim,wanaharakat n.k.
   
 19. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,749
  Trophy Points: 280
  A seed must die before it germinates( kama sijakosea) vyovyote mtakavyoweza kuita harakati, ugaidi..hata wafanye umafia kiasi gani, hawawezi kutumaliza:)
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,818
  Likes Received: 36,917
  Trophy Points: 280
  Uyu anaishi china.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...