Wanaharakati wa haki za binadamu, wasaidieni waliodhalilishwa kwa kupigwa hadharani na viongozi wa umma

Chendembe

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
416
462
Wapendwa kuliibuka wimbi la viongozi wa serikali kujichukulia Sheria mkononi katika awamu iliyopita. Hali hiyo, imeathiri saikolojia ya waathilika na kushindwa kujuwa cha kufanya.

Tuna sheria za adhabu kwa umma na utumishi ambazo tumejiweka na hatuna budi kuziheshimu na kuzifuata.

Vitendo hivi vikiachwa bila kushughulikiwa, vitatengeneza watawala badala ya viongozi. Pia vitakomaza TABIA ya kutotii Sheria na kuziheshimu mamlaka za adhabu tulizojiwekea.

Chonde chonde wanaharakati, tusaidieni kukomesha hili.

Naomba pia mheshimiwa Raisi kutoa vibali vya kushitakiwa watakaobainika kutende kosa hili.
Nawasilisha
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom