Wanaharakati na Juhudi za kuikwamua Jamii ktk Lindi la Umaskini LIVE ON STAR TV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaharakati na Juhudi za kuikwamua Jamii ktk Lindi la Umaskini LIVE ON STAR TV

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Feb 26, 2012.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [h=2][​IMG] Tunawatathmini vipi Wanaharakati NCHINI na vuguvugu la kisiasa (Live on Star TV) 12 FEBR 2012[/h]
  Habari za JUMAPILI wanaJF;

  Leo tunaangazia harakati za makundi ya Wanaharakati NCHINI katikati ya upepo huu wa siasa zinazovuma NCHINI

  Tunazungumza na
  Marcus Albany - Policy forum
  Ussu Malya - Mkurugenzi TGNP
  Zainabu Nyumba - Mjumbe baraza kuu CUF

  Tunakaribisha maoni na mtazamo wenu wanaJF kufuatia kauli za hivi karibuni kutokana na kulaumiwa Wanaharakati kuchochea vurugu.
  [​IMG]RobotArray


  Join Date : 11th February 2006
  Location : Here...!
  Posts : 8,538
  Rep Power : 100000


  [​IMG] Re: Tunawatathmini vipi Wanaharakati NCHINI na vuguvugu la kisiasa (Live on Star TV)

  Wanasemaje juu ya mfumuko wa bei wa sasa? Dar nasikia 'sado' ya nyanya iliyokuwa inauzwa 2,000 mwezi Disemba leo inauzwa 7,000!


  26 FEBR 2121

  Tunairejea mada hii kama nilivyodokeza Jumapili ya wiki iliyopita na tutaanzaia hapa kwa hoja hii ya Mkuu INVISSIBLE na hoja nyinginezo ambazo hatukuzikamilisha:

  Mada Jumapili ya leo itasomeka kama: Wanaharakati na Juhudi za kuikwamua Jamii ktk Lindi la Umaskini

  Karibuni wadau kwa mawazo, michango, na maswali.
   
 2. Imany John

  Imany John Verified User

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  aksante.
   
 3. A

  Ashoboza Kabalim Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wa SAUT Mwanza. Swali kwa mwamaharakati:
  Kwanza, kwa nini wanaharakati wengi Tanzania wamejikita katika siasa zaidi?
  Pili, mbona nguvu nyingi za wanaharakati zinaonekana mijini zaidi ya vijijini ambako haki zinakiukwa?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Binafsi ningependa kuchangia mawili matatu lakini naona ni ngumu kweli kuingia huko
   
 5. l

  lijumbete Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Natambua mchango wenu wanaharakati ombi langu; hebu jaribuni kuenda kwenye vyuo vikuu viwili ambavyo ni muhimbili na UDSM, jaribuni kuwashawishi wawarudishe vyuoni wanafunzi waliofukuzwa maana kwa hali iliyopo hata wanafunzi wenzao hawawezi kuwatetea tena
   
 6. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nasubiri mchango wako Mkuu
   
 7. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wa Arusha, watanzania wengi ni maskini, lakini wengi pia hawajui kama ni maskini, maana umaskini umekuwa ukitafsiriwa kimaghalibi zaidi na hivyo kuwafanya watanzania wengi kudhani umasikini ni kipato tu na kipato cha dola!
   
 8. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  ningependa kujua ni kwa vipi wanaharakati hawa wamefanikiwa katika harakati zao,binafsi naona wamekuwa wakihama mada moja kwenda nyingine bila kusimamia jambo moja kikamilifu.
  Wanaharakati hawa wana mikakati gani ya kumpigania mlaji au chama cha walaji,kwa mfano leo hii ukienda bar utakuta bei ya bia ni shilingi 1700+ bila kuwepo tangazo kutoka TBL,yaani wafanyabiashara wamekaa chini na kuamua bei ni hii,kama wanaharakati wanaliaje swala hili?
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Nampongeza bwana Marcus kwa kuchambua mada vizuri hakika yeye ni mwanaharakati,mimi nataka kumuuliza mbona hawaingilii hizi safari za rahisi nyingi nyingi ambazo zinatufilisi sisi watanzania ambapo hadi baadhi ya sector zinakosa mishaara?
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Pili namuuliza mbona maswala ya ufisadi hawayavalii njuga? Naona kama wanayapotezea vile,kuna swala la TBS,kondumu feki,wizi wa bil20 alizoibua cheyo,mbona mmekaa kimya kwenye maswala kama hayo ambayo ndio chanzo kinachotuingiza ktk umaskini?
   
 11. G

  Godwine JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  @wanaharakati

  zuieni wizi wa rasilimali za Taifa kwani madini,wanyama, gasi na mafuta vinaibiwa na makampuni ya kigeni na kuacha wananchi masikini wakati sisi tuna utajili mkubwa wa rasilimali hizi.


  Lakini kama Tanzania tuliumbwa tuwe masikini basi wanaharakati mnatakiwa muamasishe matumizi mabaya ya rasilimali hizi.
   
 12. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Swali. Je kuna uhusiano wowote kuhusu kuongezeka kwa mauaji kwa imani za kishirikina na umaskini? Na je nini msimamo wenu kuhusu mauaji ya songea? Na je mwisho wenu wa kutetea haki ni wapi. Hapa tungependa kupata taarifa kama mna kesi zozote dhidi ya serikali
   
 13. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mim nafikiri kama serikali ingeweza kutumia juhudi na nguvu nyingi kama inavyotumia kuzima maandamano ya amani ya wananchi kaitika kusimamia uzalishaji wangeweza kupunguza umasikini kwa kiwango kikubwa. Lakini pia jitihada zinazolenga kuwakomboa wakulima kama kilimo kwanza zinawalenga wale ambao wana uwezo zaidi, kwamfano ili ukopeshwe tracta la unahitaji kuwa na hati ya nyumba, badala ya kumtaka awe na mashamba kama dhamana, Sasa unaweza kujiuliza wakulima wangapi wana hati za nyumba? Ndo maana matrecta yamebaki kwenye yadi kama maonesho!
   
 14. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nini msimamo wa wanaharakati juu ya yafuatayo:-
  1. Madai mbalimbali ya muda mrefu ya walimu zidi ya serikali???
  2. Ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma hasa wa kada za chini ili kuendana na kasi ya ugumu wa maisha???
   
 15. O

  OMUSILANGA JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 384
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndgu Yahaya, hapa tulipofikia ,serikali imesha poteza dira. Mambo manne aliyosema Mwl Nyerere i.e uongozi bora na siasa safi hayapo tena badala yake tumeongeza mzungu,ufisadi na unafki kwa viongozi.
   
 16. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  wanaharakati wanawasaidiaje wafanyakazi wa PPF waliofukuzwa kazi kwa kupambana na ufisadi mkubwa unaofanywa na Mkurugenzi Mkuu kwa kushirikiana na Bodi?

  Walipambana ndani kuzuia ugawanaji wa kifisadi wa milioni 220 kila miaka mitatu kwa kila mkurugenzi kwa pesa za maskini wachangiaji wa mfuko. DG hupata tshs 540M kila miaka minne. Luhanjo alililea hili, CAG anafumbia macho.

  Wanaharakati mnasemaje au wafanye nini?

  Ili kuwafukuza walisingiziwa kuwa ni wachangiaji hapa JF
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye dimbwi kubwa la umaskini ni ndoto kama maamuzi magumu hayatachukuliwa na serikali. Hatua ya kwanza na ya msingi ni kupunguza gape kubwa kati ya wenye nacho na wasionacho. Hata hivyo hii hatua haitaweza kufanikiwa chini ya utawala uliopo ambao umejaa mafisadi. Madini yetu yanakwapuliwa na wageni huku watanzania tukibaki kutimuliwa vumbi. Tunahitaji mapinduzi ya kweli, Wanaharakati ongozeni mapambano.
   
 18. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #18
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ahsanteni sana wanaJF kwa michango yenu na hekima zenu tukutane Ijumaa kwa mada itakayoangazia kauli tata za wanasiasa na hatua zilizopitiliza za Jeshi la Polisi katika kushughulikia au kupambana na makundi ya wananachi wanaodai haki zao
   
 19. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tuko pamoja kiongozi, kila la kheri Yahya.
   
 20. N

  NGOWILE JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 454
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wa Dodoma,nataka kujua ni nini msimamo wa wanaharakati juu ya mfumo mbovu wa elimu nchini,mfano kuwa na elimu isiyoendana na mazingira halisi ya kitanzania? Kuwa na walmu wengi waliofeli mitihani ya sekondari? Wanafunzi wa shule za msingi kupewa mitihani ya kuchugua tu ambayo inapunguza upeo wa kufikisiuz na ubunifu n
   
Loading...