Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 301
(kutoka Gazeti la Habari Leo)
WANAHARAKATI wa usawa wa jinsia, haki za binadamu na demokrasia, wamedai Bunge limeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia Serikali kwa kuridhia kuzika masuala ya Richmond na Kiwira katika mkutano wake uliomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma.
Muungano wa Asasi za Kiraia zinazotetea Usawa wa Jinsia, Haki za Binadamu, Maendeleo ya Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct), umetoa tamko ambalo pamoja na mambo mengine, linawataka wanaharakati hao waandamane kwa lengo la kuonesha kutoridhishwa na Bunge hilo.
Katika kile kinachoonesha ni kuibua mjadala na mgongano wa kimawazo kati yao na wabunge, wanaharakati hao wamesisitiza kwamba uamuzi wa kulinyooshea Bunge kidole, hauwezi kuwa mgogoro, kwani chombo hicho hakiko juu ya wananchi.
Bunge haliko juu ya wananchi. Kimsingi wananchi tunataka. Huu si mgogoro, huwezi kuwa na mgogoro na mtu unayemwajibisha, alisema mwakilishi wa Shirika la Fordia, Buberwa Kaiza na kusisitiza kwamba tamko hilo halitokani na kuwaridhisha wafadhili kama ambavyo imekuwa ikidhaniwa.
Wanaharakati hao katika tamko lao lililosomwa jana Dar es Salaam na wawakilishi wanne kwa nyakati tofauti, zaidi ya kusema Bunge halikutimiza wajibu katika taarifa zilizofikishwa katika mkutano wake wa 18, hawakuweka bayana kasoro za Bunge katika kushughulikia masuala ya Richmond, TICTS, TRL, taarifa ya uchafuzi wa mazingira kwa kemikali za sumu ulioathiri binadamu katika mgodi wa North Mara na ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo la Loliondo.
Baadhi ya wanaharakati waliwasuta wabunge waliosadikiwa kuwa vinara wa kupambana na ufisadi bungeni, kuwa wameonesha kwamba kauli zao zilikuwa za kisanii, kwa kuwa wameshindwa kusimama kidete hadi mwisho kuhakikisha Serikali inawajibika si tu kwa Richmond, bali pia kwa kashfa zingine likiwamo suala la Kiwira.
Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananilea Nkya, akichangia tamko hilo, alisema, wabunge wangeendelea kusimama kidete. Hata kama wangefukuzwa chama, ingesaidia. Lakini hakuna aliyesimama hadi mwisho hatulilii kwenda bungeni.
Akisoma sehemu ya kwanza ya tamko hilo lililosainiwa na asasi hizo zinazounda FemAct, pamoja na taasisi nyingine likiwamo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kaiza alisema mfumo mbaya wa madaraka na uwajibikaji kati ya Serikali na Bunge, unaruhusu maslahi ya chama tawala kuchukua hatamu kuliko ya wananchi.
Wanaharakati hao walitaka Baraza la Mawaziri lisitokane na wabunge. Mfumo huu umedhoofisha demokrasia shirikishi ambayo ingewezesha wananchi na makundi yao kuwa na uwezo wa kuliwajibisha Bunge, wabunge na madiwani, alisema Kaiza.
Kaiza ambaye hata hivyo alikiri kwamba hata katika asasi za kiraia, wapo wanafiki wanaonyooshea vidole Serikali bila wao kumaanisha, alisisitiza kwamba tabia hiyo ni ya mtu mmoja mmoja.
Wapo maprofesa wanaochoka kuandika, wanaamua kwenda bungeni kudai posho, hata wanaharakati wapo wanaochoka. Huyo aliyechoka amepotea tunamwacha, lakini huo uangaliwe kama udhaifu wa mtu na si wanaharakati wote, alisema.
Alisema katika muktadha wa mfumo unaolimbikiza madaraka kwa walio wachache na kuvuruga uwajibikaji, ni vigumu kwa Bunge kuiwajibisha Serikali kama inavyotazamiwa.
Ndiyo maana Bunge limefunika kisiasa kashfa za Richmond, Kiwira, TRL na TICTS, ingawa kashfa hizi zimelisababishia Taifa hasara kubwa ya mabilioni ya fedha na madhara makubwa kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwafanya wawe masikini na fukara zaidi, alidai Kaiza.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Malya, alidai kuwa Sh bilioni 173 zilizopotea katika kashfa ya Richmond zingewezesha kujenga nyumba 19,211 za walimu wa shule za msingi nchi nzima. Mwakilishi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Francis Kiwanga, alisisitiza kwamba utawala uliopo haukidhi haja ya kusimamia rasilimali za nchi.
Alisema panahitajika mapinduzi makubwa na ya haraka katika mfumo wa uwajibikaji na uongozi, muundo wa sera za utawala, siasa na uchumi.
Kiwanga alisema, Uchaguzi Mkuu wa 2010 ni fursa pekee kwa wananchi kufanya mapinduzi yanayotarajiwa. Wabunge wetu wa sasa wameshindwa kutetea na kulinda haki na maslahi ya Taifa na wananchi.
Ingawa Spika Samuel Sitta hakupatikana jana kuzungumzia shutuma za wanaharakati, katika mkutano wa 18, Bunge lilipokea na kuridhia taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu mkataba baina ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni ya Richmond Development Company (LLC) pamoja na mkataba wa ubinafsishwaji wa mgodi wa makaa ya mawe, Kiwira.
Kuhusu North Mara, baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Serikali ilielekezwa kuchunguza haraka ili walioathirika na kemikali za sumu walipwe fidia.
Taarifa ya Loliondo haikufikishwa bungeni wakati TICTS na TRL hazikujadiliwa kutokana na Bunge kubaini kwamba hakukuwa na utekelezaji uliofanywa na Serikali.